Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono

Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono

Habari ndugu zangu wana jamiiforums,

Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Rais wetu JPM kwa yote makubwa aliyoyafanya na anayoendelea kuyafanya ambayo hayakuwahi kufanyika hapa nchini

Sifa zake zinatosha kabisa kuitwa Rais Bora barani Afrika.

Jana wakati kikao cha bunge kikiendelea my kessy (mbunge wa ccm alikuja na hoja ya kumtaka mh rais aendelee kukaa madarakani baada ya muda wake kuisha.

Hoja yake ilipewa nguvu na spika wa bunge mh job ndugai pale aliposema kwa vyovyote mh rais ataendelea kubaki mdarakani hata asipotaka ( watamshinikiza ) .
Mimi Kama raia wa Tanzania napingana na hoja hiyo kwani mh rais kwa kinywa chake mwenyewe alitamka ya kwamba hataweza kufanya kitu Kama hicho.
Wasiwasi wangu unakuja kwanini wamlazimishe mh rais wetu mpendwa While hataki?

Kuna Nini nyuma ya pazia?
Ninashauri hao waheshimiwa wanaotaka kulazimisha mh rais abaki madarakani wachunguzwe huenda wakawa na ajenda za siri ambazo wanaona akija mtu mwingine hawataweza kuziendeleza.
Mods msifute Uzi wangu sahihisheni palipo na makosa.
 
Rais Magufuli anafanya kazi kubwa na nzuri wazo la kumuongezea muda ni wazo zuri sana
 
Atawaachia wengine akimaliza 10 years! Hata Mh.Rais mwenyewe analitambua hilo.
 
Hii nchi sio ya wapiga mapambio wachache..wasituletee ubepali wa zama za utawala wa rumi.
 
Ukitaka kujua kama hiyo agenda ya siri ipo anza na sheria za kujilinda wanazopeleka bungeni

Wengine huko ndani ya CCM utakuta utendaji wao haumridishi Mh Rais unafikiri wafanye nini kama siyo kumsifia kwa kipindi hiki kifupi kilichobaki?

Na wafikiri leo wana rais mzuri je wa kesho akiwa mbaya unaanza kumpunguzia miaka? Hakuna mtu atakayeishi milele
 
Hayo yote Ni matokeo ya Kodi zetu
Wewe ulitaka asijenge ili azile?
Tumia akili.
Miaka yote tulikuwa hatulipi kodi? Hivi huwa mnapelekaga akili wapi? Ukute hata kodi enyewe hulipi ukinunua kitu hudai risiti halafu unakuja hapa kujinadi eti kodi zetu, kwani kodi tumeanza lipa awamu ya JPM tu. Hawa wapinzani wao hawapati ruzuku mbona hawana ofisi yenye hadhi.
 
Hawa jamaa bwana hawaoni hata haya

Nchi hii inawatu ml 60s ina maana katika watu wote hao hakuna wengine wenye uwezo wa kuiongoza nchi mpaka wafikie hatua ya kubadili rasimu ya katiba ili jiwe aendelee kutawala ?
 
Kuna watu wana unafiki wa kiwango cha juu sana kweli adui hajawahi kutoka mbali na Ring yako
 



"Kuna watu ni wanafiki Katiba siyo Msaafu, muda wowote inabadilishwa na siyo Rais wa kwanza kuongezewa muda, atake asitake alazimishwe haiwezekani kumuachia nafasi, naulizwa kila siku baada ya Magufuli nani anafuata mimi nasema anaongezewa muda"- Ally Kessy (CCM).

Spika Ndugai ajibu hivi

“Mheshimiwa Keissy ngoja twende uchaguzi mkuu, turudi, na mimi naamini sote tunarudi. Hilo ulishikie uwe nalo moyoni, tutarudi hapa [bungeni] salama, azimio hilo utakuja kulileta wewe Mzee Kessy na litapita kwa kishindo, atake asitake [Rais Magufuli] tutaongeza muda,” Job Ndugai

Hawa watu kwanamna nyingine hawalitakii mema taifa hili, kwann hawapiganii mfumo bali wanakomaa kumuongeza mda mtu binafsi?
Je hawajiuulizi ikitokea Mungu akampenda zaidi nchi itaelekea wapi?
Kwa mtazamo wangu mfumo bora ndio bora kwa maendeleo yetu kuliko one man show.
 
Hawa hawatanii wanaweza kumuongezea muda kweli.
 
Nimeshangazwa na uelewa wa wabunge hawa kuongelea swala la kubadili Katiba kimasihara. Wamuogope Mungu na kuheshimu katiba na Watanzania. Ni dhambi kumtukuza na kumsujudu mwanadamu anaepita.
 
Back
Top Bottom