Sasa kama aliamuru watu wapigwe risasi, wauawe na kuwekwa kwenye sandarusi, kufilisi watu, kufukuza watu kazi, kufunga watu midomo n.k kwanini watu wasifunguke baada ya yeye kutwaliwa kule kuzimu? Mfalme Herode na Filauni hadi leo wanatajwa kwa ukatili wao ingawa walishakufa maelfu ya miaka sembuse huyu aliyekufa juzi? Kwanini Mkapa, Nyarere ambao walitangulia kabla yake hawatajwi kama yeye? Ukifanya mabaya utayavuna hata kama umekufa ndiyo utaratibu wa dunia, kama wewe ulifaidi kipindi cha mwenda zake una kazi ngumu sana ya kumtetea mbele za watu walioumizwa nae.
Unadhani familia na wazazi wa Ben Saanane ambao hata maiti ya ndugu yao hawakuiona kwa ufedhuli wa huyu nduli wanajisikiaje wakilisikia jina la huyo mfalme wa chato? Familia ya Azori Gwanda nao unadhani watamfurahia? Ndundu Lissu aliyepigwa risasi kwenye nyumba za serikali zenye kila aina ya ulinzi camera zikachomolewa, walinzi wakapelekwa likizo bado wakamnyima haki za kutibiwa wakaona haitoshi wakamfukuza na ubunge n.k.
Hivi ingekuwa nawewe umepitiwa na risasi kwenye korodani kwa amri ya huyu mtukufu wa chato ungekuja na utetezi hapa wa kumtetea? Sasa kama kimekuuma nenda kachimbe kaburi karibu yake jifukie!