Ally Mayay amekosa endorsment (kuungwa mkono) asubiri Mamlaka ziamue

Chaguzi kwenye mashirikisho/vyama vya mpira wa miguu zimejaa figisu hadi FIFA kwenyewe.

Viongozi wanaondolewa kwa kashfa siyo chaguzi anzia kwa Sepp Blatter,Michel Platini,Jamal Malinzi etc

Karia bila kumtafutia zengwe watasubiri sana.
 
Kama umekosa udhamini ni dhahiri ungeisumbua tu Tume ya Uchaguzi kujaza wagombea, maana hata kura usingepigiwa. Kama hadharani hujapata wadhamini, basi kwenye kura ambayo ni ya siri usingefikiriwa kabisa
Utahira wenu ndio umetufikisha hapa!!, unawezaje kuanza kutafuta wadhamini wakati uchaguzi haujatangazwa?, unawezaje kuwa mgombe mmoja uliyepata udhamini pekee yako?. Utaratib wa kijinga mnaushadadia wapuuzi nyie..
 
Mdau wa soka Ally Mayai Tembele ambaye alichukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais wa shirikisho la soka Nchini (TFF) amesema hata yeye amekosa endorsment hivyo anasubiri mamlaka ziamue.

"Nimekosa Endorsement, kwa sababu nilichukua fomu nilipaswa kuirejesha.Kwa sasa imekuwa ngumu.Zamani chama cha soka kilikuwa na uwezo wa kuwaendorse watu zaidi ya mmoja lakini kwa sasa ni mmoja tu, tusubiri mamlaka zitaamua nini."

Ally Mayayi tangu zamani unajua ya kwamba watu wa TFF (zamani FAT) HAWAKUTAKI na HAWAKUPENDI kwenye mpira wao. Na huu ni ushuhuda wa wewe kukosa endorsement. Kwanini unawang'ang'ania wenye mpira wao!?
 
Mi mpaka sasa hivi sielewi utaratibu ni nini mpaka haya yote yanatokea
Yule mpuuzi ametengeneza kanuni za kumfanya kuwa rais wa maisha wa TFF jambo ambalo halikubaliki hata kidogo. Amehudumu mihula miwili, alitakiwa kuwaachia wengine nao waongoze.

Ila bahati mbaya anelekea kuifanya TFF kuwa mali yake. Na kwa sababu ni kada mtiifu wa ccm, hakuna hatua zozote zile atakazo chukuliwa. Ujinga mkubwa sana huu.
 
Hizo kanuni zimewekwa lini? Kama si kipindi hiki cha uchaguzi, basi wa kulaumiwa ni Wagombea wenyewe. Kama waliona kanuni hizo ni mbaya walipaswa miaka angalau miwili kabla wapigenie zibadilishwe.
Hata uchaguzi uliopita, kilio kilikuwa ni hiki hiki! Baada ya hapa, watasahau. Uchaguzi mwingine ukifika, tutaanza kuyasikia mayowe tena, ya ' HIZI TARATIBU NI MBAYA'!!
 
Yule mpuuzi ametengeneza kanuni za kumfanya kuwa rais wa maisha wa TFF jambo ambalo halikubaliki hata kidogo. Amehudumu mihula miwili, alitakiwa kuwaachia wengine nao waongoze.

Ila bahati mbaya anelekea kuifanya TFF kuwa mali yake. Na kwa sababu ni kada mtiifu wa ccm, hakuna hatua zozote zile atakazo chukuliwa. Ujinga mkubwa sana huu.
Kwani ata ao wanaogombea si makada watiifubwa ccmm
 
Bongo huwa hakuna kitu kinaitwa chaguzi za haki, zipo chaguzi za taratibu na kanuni...
 
Yule mpuuzi ametengeneza kanuni za kumfanya kuwa rais wa maisha wa TFF jambo ambalo halikubaliki hata kidogo. Amehudumu mihula miwili, alitakiwa kuwaachia wengine nao waongoze.

Ila bahati mbaya anelekea kuifanya TFF kuwa mali yake. Na kwa sababu ni kada mtiifu wa ccm, hakuna hatua zozote zile atakazo chukuliwa. Ujinga mkubwa sana huu.
Ndio maana nilikua nashangaa mbona chaguzi nyingine hiki kitu hakikuwepo na sikuwahi kukisikia. Kumbe ni kanuni mpya

Karia must GO
 
Ila raisi wa yanga na wasimba si walikubaliana kwenye mkutano mkuu kuwa karia apite bila kupingwa
Ndio nami nasema apite bila kupingwa kafanya makubwa sana kwa mpira wetu
Afcon level zote tumeingia
Futsal tunaenda world cup
Under 17 girls tulienda
Caf League finals mbili
Ligi inapata "endorsement"za kutosha
Angalau kumekuwa na uwazi wa mchezo
 
Kama umekosa udhamini ni dhahiri ungeisumbua tu Tume ya Uchaguzi kujaza wagombea, maana hata kura usingepigiwa. Kama hadharani hujapata wadhamini, basi kwenye kura ambayo ni ya siri usingefikiriwa kabisa
Siyo kweli...

Ukweli usemwe tu kwamba kipengele cha udhamini hakina mashiko zaidi ya kunyima watu fursa ya kugombea
 
Ally Mayayi tangu zamani unajua ya kwamba watu wa TFF (zamani FAT) HAWAKUTAKI na HAWAKUPENDI kwenye mpira wao. Na huu ni ushuhuda wa wewe kukosa endorsement. Kwanini unawang'ang'ania wenye mpira wao!?
Karia katumia strategy mbaya kusema kweli. Yeye angechukua endorsement 5 tu nyingine akawaachia wagombea wengine. Halafu akacheza na wajumbe wote wampigie kura yeye.

Haya makelele yasingekuwepo!! Sasa yeye kafanya figisu za wazi wazi hizi
 
Uchaguzi Mkuu wa TFF unategemea sana "watu wa mpira".
 
K
Ally Mayayi tangu zamani unajua ya kwamba watu wa TFF (zamani FAT) HAWAKUTAKI na HAWAKUPENDI kwenye mpira wao. Na huu ni ushuhuda wa wewe kukosa endorsement. Kwanini unawang'ang'ania wenye mpira wao!?
Kumbe Kuna watu wana hati miliki ya mpira wa bongo 🤔🤔
 
Bora teeth karia kuliko huyu teeeth Mayay ila all in all serikali wanaharibu mpira wetu kwa kuingiza watu wao.
 
Back
Top Bottom