Acha uongo wee Kolo! Mtikila hajawahi kwenda Zanzibar kutafuta wadhamini kwa sababu alisema hawezi kwenda nchi jirani kutafuta wadhamini. Mtikila aliwashangaa wanaokwenda Zanzibar kutafuta wadhamini wakati wao ni Watanganyika! Mtikila alikuwa Mtanganyika halisi!FIFA wanatumia utaratibu huu, na katiba za wanachama wa FIFA zinalazimika kufuata hivyo. Hata uchaguzi wa Rais wa nchi yetu ni lazima upate wadhamini kadhaa kutoka pande zote za muungano. Mtikila aliwahi kukosa wadhamini kutoka Zanzibar 😃
Ndicho na mími najaribu kueleza Watu. Kanuni hata kama mbovu lakini ni za muda mrefu. Mgombea aliye serious alitakiwa kupambana mapema na si kusubiri wakati wa uchaguzi kusubiri hurumaAli Mayay aligombea uchaguzi uliopita akakutana uso kwa macho na hizo kanuni za hovyo yeye pamoja na wagombea wengine. Sasa maajabu ya Musa wamekaa kimya umefika wakati wa uchaguzi wamekurupuka tena wamekutana na vigingi vile vile. Niliwaambia hapa JF kuwa siku hazigandi waanze presha na vurugu (zisizoumiza) wakati ule ule ili kufika uchaguzi mwingine hizo kanuni za hovyo ziwe zimeondolewa lakini hawakunisikia. Na alipopewa nafasi BMT ndio akawa kama kanyamzishwa mazima mpaka anapoibuka tena sasa hivi wakati uchaguzi unakaribia.
Nimkumbushe tu Ali Mayay na wagombea wenzake kuwa sio kila wakati utaratibu unaleta mabadiliko bali wakati mwingine vurugu nzuri zile zisizoumiza zinaleta mabadiliko kwa mtu kutaka au kutokutaka. Kwa hiyo huyo Karia bila vurugu zisizoumiza nawaambieni hatatokaa hapo TFF.
Huo utaratibu uko hivyo miaka mingi nyuma sio mpya.Na kama ungekua na mapungufu wangekuja na hoja zakuubadilisha ila wanakaaga kimya .Kimsingi ni utaratibu mbovu kwa dunia ya leo kwasababu hautoi wigo mpana wa wagombea kushindana.🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Nilikuwa nawaambia vigezo vya TFF ya karia ni vigumu mnoo...sasa yako wapi.
Vile vigezo vipo calculated.
Ukivisoma juu juu unaviona ni rahisi.
Karia ni mafia...
Upo sahihi mkuu wanguHuo utaratibu uko hivyo miaka mingi nyuma sio mpya.Na kama ungekua na mapungufu wangekuja na hoja zakuubadilisha ila wanakaaga kimya .Kimsingi ni utaratibu mbovu kwa dunia ya leo kwasababu hautoi wigo mpana wa wagombea kushindana.
Anamaanisha amekosa mtu wa kumu endorse sawa?Anamaanisha nini anaposema endorsement?