Ally Mayay ateuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo

Ally Mayay ateuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
IMG-20220920-WA0006.jpg


Ikukupendeza uwe Azam kuichambua Yanga ikipokea kipigo cha Al Hilal,kama sehemu ya kutuaga fans wako. Namaanisha tushiriki wote kuusindikiza mwili wa marehemu mtarajiwa toka Sudan
 
Katika kuimarisha utendaji kwenye Sekta ya Maendeleo ya Michezo Nchini na kufuatia maelekezo ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, ya kufanya maboresho ili kuongeza tija, Wizara inamtambulisha, Bw. Ally Mayay Tembele kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini wakati taratibu nyingine zikiendelea.

Bw. Mayay ambaye ni Afisa Mwandamizi katika Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini, amehamishiwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuruhusiwa kukaimu majukumu haya kwa mujibu wa kibali cha Ofisi ya Rais Utumishi kupitia barua yenye kumbukumbu namba CCD.273/311/01/W/45 cha tarehe 15 Septemba 2022.

Uteuzi huo wa Bw. Mayay ambaye anachukua nafasi ya Bw. Yusuph Omary Singo aliyepangiwa majukumu mengine unaanza leo Septemba 20, 2022.

Wadau wa Michezo wanaombwa kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake.
1663661284928.png
 
Back
Top Bottom