Almanusura nipoteze vidole vyangu viwili vya mkono.(Angalizo! Nimeambatanisha na picha ya majeraha)

polesana ,ushukuru sugu ya mikono yako

lakini ,nimewaza kama ungekuwa ndani ya kiwanda fulani...spati picha
Hako kamashine ukikaangalia kako innocent ila ukijichanganya kidogo tu unakunjwakunjwa kama bales za mitumba ...Asee mdau Ni Mungu tu alikuwa nami.. leo sijui ingekuwajee.😪. Ila hawa ndugu zetu wakenya ni kama tu wamevurugwa na maisha.. mjinga huyu kidogo anifanye nife kizembe
 
todai fidia ,mshenzi kweli huyo
 
Ni kweli hata mimi nlizingua... mimi nilikuwa Operator tu maana kimashine ni automatic..sasa kwenye minor settings inabidi nizifanye mwenyewe...Next time itabidi nizangatie precautions zote.. nimejifunza in Hard way.
Usiamini mtu
 
Mkuu kuna kitu kinaitwa LOTOTO ( lock out tag out try out) mkuu unapofanya matengenezo ya kazi yoyote ya machine na mko zaidi ya watu 2 Fanya LOTOTO .Mkuu wewe ndo mzembe ulipaswa kwenda kudesconnect hiyo machine kabla hujaanza kufanya hayo matengenezo, mkuu usimuamini MTU yeyote mnapofanya kazi kwenye mashine.LOTOTO
 
Mashine ilikuwa imezimwa ... sasa kwa vile hiki kijimashine ni automatic sijui wameongea kilugha chao huko muda gani mpuuzi akabonyeza button pasipo ruhusa huko mimi niko kwa mbele naset nyuzi anyway nitafuata huu ushauri wako.🙏🙏
 
Siku zote huwa nasema kukaa karibu na mpumbavu au mwendawazimu ni hatari kwa afya na maisha yako.

Mtu kuwa mjuaji ni dalili ya wehu na uwendawazimu, si mtu anastahili ufanye kazi nae. Ukikaa na mtu smart hata kama anakuzidi, hawezi kuhatarisha maisha yako kizembe kwa sababu ya upumbavu wake.
 
Kuna jamaa huwa namuona anatembea Juu ya conveyor kwa kujiamini wakati hajamtaarifu operator, asipobadilika kuna siku atakipata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…