Am I wrong if I process divorce?

Ndo maana nimesema huyu dada ndo kamfanya mumewe awe hivo alivo. Sasa watu humu wanamshauri kuvunja ndoa, khaaa!!
 
Mbona umebadilika na wewe ndio umekuwa na makasiriko tu bila sababu that's was my opinion na Mimi niliheshimu opinion zako mwona mito tumeelewana watu huendana kulingana na taste zao na preference my preference staki hizo pigo za mtu kunichukulia mtoto eti kisa mwanaume na mtu alikataa uanze kufanya ujinga na kutelekeza familia na ada ulipi eti kisa mke uliyemkuta huvaa aina flani ya mavazi to me is childish na ninaona naishi na mtu immature hatuendani shida iko wapi?
Na hapo kunifananisha na magufuli wrong mfano kabisa hata magufuli alikuwa na taste na misimamo yake ka Mimi niliyo nayo wewe, na yoyote why muone yeye haambiliki, the only problem inayotesa watu ni kuhukumu wengine na kutaka waishi jinsi vichwani mwenu mnavotaka. Watanzania wengi wakiishi na other people from different culture huwa ni judgemental Sana, so hata magufuli usimuonee na yeye aliishi alivotakana na wewe ishi unavotaka siwezi kukuhukumu it's you mazee
 
Wewe umemuelewa vizuri sana.
Kusuluhisha ugomvi wa ndoa ambao Mwanamke ndiyo anasema ni victim inahitaji akili ya ziada.
Daah imeniuma sana, wadau wameishamuingiza chaka, kaishaondoka kwa mumewe kumbe!!

Ngoja mtaani akakutane na wazee wa fursa sasa aanze kuhesabu vichwa.

Na yule comforter anamlia timing tu
 
Hahahaha! kwamba ile kisela tu ukijisikia chochote unafanya.
 
Wala sina kasiriko hata naona tukubali kutokukubaliana tu! Kila mtu ana namna anapenda ishi maana kama hakuna compromising basi kila mtu atabaki single!

What i believe ni kuwa tofauti ndogo tunaweza zisawazisha nobody is perfect tunakutana katika 90% but hii 10% kwanini tusifanye compromising? Tukitaka kusimama na misimamo yetu then we go separate ways! Thats what i mean Cariha.

Sasa kama wewe utakuwa mtu usiyetaka ku compromise hata kidogo utaishi vipi na watu? Mke wangu is rapping ila ana akili na upendo and so generous.., i find her to be an ideal wife! Sipendi anavyogomba gomba ila it doesnt mean hawezi kuwa mke sababu ana qualities almost zote nazotaka! I find way to live with it cause i love her.

Sasa we ukitaka mtu awe perfect match by 100% utamtoa wapi ndugu yangu?

Its so rare to find mtu unayemtaka by 100% awe mrefu, handsome look, six pack, ana hela, ana life good, hachepuki, anakupa hela, haku control and sum like that! Like Yow you gotta be single for life to meet with 1
 
Nami niko namuombea jamaa ashikilie msimamo wake asiteteleke[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Unaishije na mwanamke asiye na utii kwa mumewe
Ndo hivyo waachane, hakuna kulazimishana.
 
Ila Cariha

Inatakiwa ujifunze kitu kinaitwa "Compromises"

Lazima ucheck huku na huku,sometimes misimamo usually work against yourself
I like compromises kwa situation ambazo ni win win situation Tena kuwe na strong reasons na kitu beneficial for all bana. Sababu dhahania big no kwa kweli Sasa mtu anayekwambia uvae dira uta compromise naye maana tayari ni akili ndogo
 
Unajua ni ngumu sana kwa mwanaume kumhandle mwanamke pisi kali, ana akili na anajiweza kiuchumi; wanaume wachache sana ndiyo wamefanikiwa katika hilo. Mimi nachoamini mwanamke yeyote independent especially kifikra sio rahisi kumpelekesha as majority of you hamtaki wanawake wa kuwatii; bali wanawake wa kuwapelekesha; kila kitu ndiyo mzee. Kwenu nyie utii is more of losing your self worth and your sense. As a result wengi wenu mnakuwa insecure; akikosea kidogo tu basi ushaconclude ni kwa sababu ni mzuri na ana kipato; kwani wabaya na wasio na vipato ndiyo wanyenyekevu wote? Wangapi wameoa wanawake wa kawaida kabisa na still ndoa zao zimevunjika? Utii ni tabia ya ndani kabisa ya mtu, regardless of her status. Mama Samia ni Rais, ila you can tell yule mama ni mnyenyekevu tu wa asili.

Mnatukimbilia sisi wenye sura za wajomba, na shape za kina babu + mangumbaru: kwa sababu mnahisi hatuna options nyingine, zaidi ya kuwatii. Ni wale wanawake ambao mnajua hawatongozwi sana, unamfanya utakavyo na yeye hatoondoka kwa sababu hana huwezo wa kujihudumia; in short hatuna options. Hata wanawake wengi wanaonyanyaswa na mnawaita wavumilivu; wengi si wavumilivu kweli kwamba ndiyo asili yao; ni vile hawana pa kwenda, bora tu abaki hapohapo ambako ana uhakika wa kula ugali, ila siku akipata pa kwenda atatoka ndukiii. Utii au uvumilivu wa design hii, ni wa kinafiki na ni wa muda tu. Hakuna raha kama mwanamke anajiweza afu bado anakutii; raha kichizi.

Mume wa huyu dada hajiamini na hamwamini mkewe, anawaza kuchapiwa tu muda wote. Anachokitaka yeye ni kumfubaza mke wake ili asionekane kwa wengine. Bahati mbaya, mzuri ni mzuri tu hata akivaa gunia; chukulia mfano yule muigizaji Batuli, most of times anavaa nguo za heshima and yet wakware udenda unawatoka. Ndiyo huyo bwana anajikuta mara leo nyoa, kesho suka, ooh vaa dera; hivi unalijua trako la ndani ya dera wewe, si bora tu avae vitenge? Na kwa mwanaume asiyejiamini, hata ufanyaje hatokuona mtii. Kila siku anakuja na jipya ana anataka umfuatishe tu kama bendera; yeye mwenyewe hajui hata anachokitaka kwa mkewe afu bado mke amtii aseeeeeee

Mahusiano yoyote kucompromise lazima kuwepo, ili angalau tukutane mahali fulani pazuri. Lakini pia, unapomuhitaji mwenzako abadilike/kupunguza kitu fulani; jua itachukua muda kutokea au penginepo lisitokee kabisa. Imagine mdada ambaye maisha yake yote anavaaga mawigi, leo all of a sudden unamtaka atupe mawigi chini; do you think ni rahisi hivyo? Na ni bora hata sisi huwa tunawasikiliza; jikute sasa unamwambia mume wangu acha kitu fulani au rafiki fulani si mzuri kwako; afu yeye hivyo vitu awe anaviona kwake havina madhara; utajua haujui. So kuna muda tuwape watu nafasi ya kuona mambo kwa jicho tunaloliona sisi, ikishindikana tunajifunza kuwachukulia madhaifu yao as long as hayatuletei madhara. You will never please an insecure person, neverrrr.

 
Kumbe upo?
Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Jamaa ana matatizo ya psychology either kutoka katika malezi ya familia yake baba na
mama, au

katika ndoa mleta mada kamsababishia, au kutokana na madhaifu yake binafsi yanayomtesa.

Mwanamke mzuri, mwenye elimu ya juu, kazi ,nzuri ,kipato cha kutosha akikutana na na mwanume asiyejiamini mwenye insecurities nyingi nyingi lazima matatizo yatokee kwenye mahusiano!!



Kushindwa kwake kujiamini kunamfanya kujihisi anakosa kuheshimiwa... ndio maana anatumia mabavu..

Je ni vitu gani unahisi vinamfanya ashindwe kujiamini kama mwanaume kwenye mahusiano yenu ya ndoa???

Kipato-kabla/baada?
Sex?
Upo kama mke au umesimamia msimamo wa 50/50 ?
 
Mama alipigwa hadi kulazwa? alinyanyaswa kihisia na kimwili? Unajua kuna vitu watu tumezoea sababu tumekua tukiviona tangu wadogo so tunaona kawaida..unless uliyaona hayo nyumbani, huwezi kuchukulia hili kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…