joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Umejieleza vizuri sana, kama ambavyo pesa zetu, yaani shilingi ya Kenya na ile ya Tanzania zilivyo na mapungufu mbele ya dolla ya Kimarekani, katika mazingira maalumu tu, ndiyo inapaswa kufanya miamala yetu kwa kutumia pesa nyingine, hasa miamala ya kiserikali, kwa mfano, haiwezikani wizara, au hata wewe mwenyewe nyumbani kwako na familia yako upange bajeti yenu kwa kutumia dola ya marekani...sukari kilogram moja dola ngapi?, unamuuliza mwanao, hivi utaeleweka kweli?.Kiswahili ni lugha yetu rasmi, lugha ya taifa tena ambayo imetajwa kwenye katiba kabisa, lakini hata hivyo ni lugha yenye mapungufu, ni vigumu kujieleza kwa kutumia Kiswahili mwanzo hadi mwisho bila kuchakachua. Hata hiyo Tanzania bado mna vitu vingi sana vimeandikwa kwa lugha ya Kingereza, japo mnajitahidi kuegemea upande wa Kiswahili.
Nimekua hapo Dar es Salaam, nilikuja kuwasilisha ombi (proposal) kwa ajili ya mradi fulani. Sasa juzi nilipoitwa tukaja na wezangu kujieleza, aisei nilishangaa mahojiano yalikua kwenye lugha ya kingereza, dodoso zote ilibidi tujaze kwenye hiyo lugha kwa kwenda mbele.
Mwanzo nilikua nimejiandaa kujieleza kwa kiswahili japo shughuli yenyewe (monitoring & evaluation) ina misamiati ambayo tafsiri yake kwa kiswahili ni balaa. Hapa tu baadhi ya misamiati ambayo ilinipa shida kuweka kwa Kiswahili, Baseline assessment, Bias, Conceptual Framework, Cost-Benefit Analysis, Cost-Effectiveness Analysis, Triangulation, DOPA Indicators, Efficacy, Exogenous Indicator, Formative Research, Hawthorne Effect
Nilifurahi pale jamaa waling'ang'ania kwamba tufanye yote kwa Kingereza, na ndivyo ilikua hata kwa washindani wetu.
Tatizo linakuwa kubwa zaidi pale wizara za serikali zinapotumia dollar kwa matumizi yake ya manunuzi ya ndani ya nchi kwa kisingizio kwamba shilingi zetu zina mapungufu, ama zinashuka dhamani kwa haraka sana, au kwa sababu yoyote ile, serikali ikiamua kufanya hivyo inajimaliza yenyewe kwa kuidhohofisha pesa yake yenyewe na wananchi kutoithamini pesa yao hivyo kuongezeka kwa matumizi ya pesa za nje kuliko ile ya ndani. inakubalika kupanga bajeti kwa kutumia pesa za nje katika baadhi ya miradi, hasa inayohusisha nchi za nje, kama vile miradi inayofadhiliwa na wahisani wa nje na mingineyo michache.
Lugha ya kiswahili inajitosheleza kwa zaidi ya 99%, kuendesha shughuli za ndani zote za kiserikali, kama mahakamani, bungeni na hutuba za viongozi kuwahutubia wananchi, kuendesha ibada na mambo yote ya ndani ya nchi, kama tufanyavyo Tanzania, ila katika mambo ya kitaalamu ni kweli kuna mapungufu, japo sio mapungufu ya maneno ila bado maneno ya kitaalamu mengi hayajulikani kwa watu, hivyo haileti maana kuyatumia iwapo yatashindwa kufikisha ujumbe uliokusudiwa.
Serikali yoyote ile inajukumu la kuilinda pesa yake na kusisitiza matumizi ya pesa yake kwa matumizi ya ndani kwa kuonyesha mfano kwa wananchi wake, kwa kufanya miamala yake kwa kutumia pesa yake, sio kwa kusema tu kwamba pesa ya nchi yetu rasmi ni Shilingi lakini yenyewe inalipa mishaara ya wafanyakazi wake interms of $, ndivyo inavyofanya serikali ya Kenya kwenye suala la Lugha, inajinasibu kwamba lugha ya taifa ni kiswahili, lakini shughuli zote za serikali zinaendeshwa kwa kiingereza, matokeo yake Kiswahili Kenya kinazidi kupoteza thamani yake kama vile Dollar ya Zimbabwe inavyopoteza thamani yake.
Sent using Jamii Forums mobile app