Am shook: for Tanzanians who dont understand simple lingua

Kiswahili ni lugha yetu rasmi, lugha ya taifa tena ambayo imetajwa kwenye katiba kabisa, lakini hata hivyo ni lugha yenye mapungufu, ni vigumu kujieleza kwa kutumia Kiswahili mwanzo hadi mwisho bila kuchakachua. Hata hiyo Tanzania bado mna vitu vingi sana vimeandikwa kwa lugha ya Kingereza, japo mnajitahidi kuegemea upande wa Kiswahili.

Nimekua hapo Dar es Salaam, nilikuja kuwasilisha ombi (proposal) kwa ajili ya mradi fulani. Sasa juzi nilipoitwa tukaja na wezangu kujieleza, aisei nilishangaa mahojiano yalikua kwenye lugha ya kingereza, dodoso zote ilibidi tujaze kwenye hiyo lugha kwa kwenda mbele.

Mwanzo nilikua nimejiandaa kujieleza kwa kiswahili japo shughuli yenyewe (monitoring & evaluation) ina misamiati ambayo tafsiri yake kwa kiswahili ni balaa. Hapa tu baadhi ya misamiati ambayo ilinipa shida kuweka kwa Kiswahili, Baseline assessment, Bias, Conceptual Framework, Cost-Benefit Analysis, Cost-Effectiveness Analysis, Triangulation, DOPA Indicators, Efficacy, Exogenous Indicator, Formative Research, Hawthorne Effect

Nilifurahi pale jamaa waling'ang'ania kwamba tufanye yote kwa Kingereza, na ndivyo ilikua hata kwa washindani wetu.
Umejieleza vizuri sana, kama ambavyo pesa zetu, yaani shilingi ya Kenya na ile ya Tanzania zilivyo na mapungufu mbele ya dolla ya Kimarekani, katika mazingira maalumu tu, ndiyo inapaswa kufanya miamala yetu kwa kutumia pesa nyingine, hasa miamala ya kiserikali, kwa mfano, haiwezikani wizara, au hata wewe mwenyewe nyumbani kwako na familia yako upange bajeti yenu kwa kutumia dola ya marekani...sukari kilogram moja dola ngapi?, unamuuliza mwanao, hivi utaeleweka kweli?.
Tatizo linakuwa kubwa zaidi pale wizara za serikali zinapotumia dollar kwa matumizi yake ya manunuzi ya ndani ya nchi kwa kisingizio kwamba shilingi zetu zina mapungufu, ama zinashuka dhamani kwa haraka sana, au kwa sababu yoyote ile, serikali ikiamua kufanya hivyo inajimaliza yenyewe kwa kuidhohofisha pesa yake yenyewe na wananchi kutoithamini pesa yao hivyo kuongezeka kwa matumizi ya pesa za nje kuliko ile ya ndani. inakubalika kupanga bajeti kwa kutumia pesa za nje katika baadhi ya miradi, hasa inayohusisha nchi za nje, kama vile miradi inayofadhiliwa na wahisani wa nje na mingineyo michache.

Lugha ya kiswahili inajitosheleza kwa zaidi ya 99%, kuendesha shughuli za ndani zote za kiserikali, kama mahakamani, bungeni na hutuba za viongozi kuwahutubia wananchi, kuendesha ibada na mambo yote ya ndani ya nchi, kama tufanyavyo Tanzania, ila katika mambo ya kitaalamu ni kweli kuna mapungufu, japo sio mapungufu ya maneno ila bado maneno ya kitaalamu mengi hayajulikani kwa watu, hivyo haileti maana kuyatumia iwapo yatashindwa kufikisha ujumbe uliokusudiwa.

Serikali yoyote ile inajukumu la kuilinda pesa yake na kusisitiza matumizi ya pesa yake kwa matumizi ya ndani kwa kuonyesha mfano kwa wananchi wake, kwa kufanya miamala yake kwa kutumia pesa yake, sio kwa kusema tu kwamba pesa ya nchi yetu rasmi ni Shilingi lakini yenyewe inalipa mishaara ya wafanyakazi wake interms of $, ndivyo inavyofanya serikali ya Kenya kwenye suala la Lugha, inajinasibu kwamba lugha ya taifa ni kiswahili, lakini shughuli zote za serikali zinaendeshwa kwa kiingereza, matokeo yake Kiswahili Kenya kinazidi kupoteza thamani yake kama vile Dollar ya Zimbabwe inavyopoteza thamani yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa Boss
Wala sio kosa lako kuangalia wikipedia ili kujua lugha rams ya taifa la Kenya ni ipi, na wala sio wewe peke yako watu wengi sana hata wakenya wenyewe wapo wanaojua kwamba lugha ya taifa la Kenya ni Kiingereza, hili linatokana na serikali yenyewe ya kuhubiri amani huku imeficha mapanga kwapani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mkenya mmja kaeleza yakuwa kiswahili pekee hauwezi kujielezea bila ya kuchanganya na kingereza, huyo jamaa MUONGO na anabahatisha kuzungumza kwa kiswahili
 
Kenya isha uzwa kwa wazungu ndo maana hotuba na bunge utumia kingereza ili mzungu aelewe siyo wanaojidhani wananchi
 
Umejieleza vizuri sana, kama ambavyo pesa zetu, yaani shilingi ya Kenya na ile ya Tanzania zilivyo na mapungufu mbele ya dolla ya Kimarekani, katika mazingira maalumu tu, ndiyo inapaswa kufanya miamala yetu kwa kutumia pesa nyingine, hasa miamala ya kiserikali, kwa mfano, haiwezikani wizara, au hata wewe mwenyewe nyumbani kwako na familia yako upange bajeti yenu kwa kutumia dola ya marekani...sukari kilogram moja dola ngapi?, unamuuliza mwanao, hivi utaeleweka kweli?.
Tatizo linakuwa kubwa zaidi pale wizara za serikali zinapotumia dollar kwa matumizi yake ya manunuzi ya ndani ya nchi kwa kisingizio kwamba shilingi zetu zina mapungufu, ama zinashuka dhamani kwa haraka sana, au kwa sababu yoyote ile, serikali ikiamua kufanya hivyo inajimaliza yenyewe kwa kuidhohofisha pesa yake yenyewe na wananchi kutoithamini pesa yao hivyo kuongezeka kwa matumizi ya pesa za nje kuliko ile ya ndani. inakubalika kupanga bajeti kwa kutumia pesa za nje katika baadhi ya miradi, hasa inayohusisha nchi za nje, kama vile miradi inayofadhiliwa na wahisani wa nje na mingineyo michache.

Lugha ya kiswahili inajitosheleza kwa zaidi ya 99%, kuendesha shughuli za ndani zote za kiserikali, kama mahakamani, bungeni na hutuba za viongozi kuwahutubia wananchi, kuendesha ibada na mambo yote ya ndani ya nchi, kama tufanyavyo Tanzania, ila katika mambo ya kitaalamu ni kweli kuna mapungufu, japo sio mapungufu ya maneno ila bado maneno ya kitaalamu mengi hayajulikani kwa watu, hivyo haileti maana kuyatumia iwapo yatashindwa kufikisha ujumbe uliokusudiwa.

Serikali yoyote ile inajukumu la kuilinda pesa yake na kusisitiza matumizi ya pesa yake kwa matumizi ya ndani kwa kuonyesha mfano kwa wananchi wake, kwa kufanya miamala yake kwa kutumia pesa yake, sio kwa kusema tu kwamba pesa ya nchi yetu rasmi ni Shilingi lakini yenyewe inalipa mishaara ya wafanyakazi wake interms of $, ndivyo inavyofanya serikali ya Kenya kwenye suala la Lugha, inajinasibu kwamba lugha ya taifa ni kiswahili, lakini shughuli zote za serikali zinaendeshwa kwa kiingereza, matokeo yake Kiswahili Kenya kinazidi kupoteza thamani yake kama vile Dollar ya Zimbabwe inavyopoteza thamani yake.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nahisi kwamba umesoma hadi chuo kikuu, pengine hata usomea mambo ya uchumi. Kama ni ukweli basi nina swali moja. Chuoni kikuu ulifunzwa kwa lugha gani kiswahili au kiingereza?
 
Swali zuri sana, kwanza mimi sijafika chuo kikuu, niliishia form six nikashindwa kupata maksi za kuingia chuo kikuu, ila nipo kwenye harakati za kupitia mfumo usio rasmi ili niweze kufika huko, mungu akiniwezesha.

Tukirudi kwenye mada, ukisoma hapo juu kwenye jibu langu la msingi kwa MK254, nimesema tunaweza kutumia lugha au pesa za kigeni pale tu ambapo kuna ulazima, pale ambapo kiswahili hakijitoshelezi kwa sasa, maeneo kama hayo ya elimu ya juu, maeneo ya Sayansi, tafiti za kisayansi ambayo kimsingi asili yake sio afrika ni huko uzunguni, wakati huohuo tujiandae na kukikuza kiswahili baadae kiweze kuziba hilo pengo, kumbuka hata hicho kiingereza kina maneno mengi yw lugha zingine kama kilatini, kiitaliani, kijerumani, hata kiswahili pia kimetumika kwenye kukikuza kizungu, neno kama safari, au bodaboda yanatumika katika lugha ya kiingereza.

Ni aibu nchi huru yenye mamlaka yake ya kujitawala kiuchumi kutumia pesa ya nchi nyengine katika shughuli zake za ndani, ukiona nchi yoyote ile huru, inatumia pesa ya nchi zingine zaidi ya 20% katika mzunguko wa ndani, ujue hiyo nchi inapoteza udhibiti wa uchumi wake, sio kwamba imependa, mfano mzuri ni Zimbabwe, baada ya uchumi wa Zimbabwe kuparagqnyika walilazimika kuruhusu matumizi ya Randi ya SA, na $,

Tanzania inafanya juhudi kubwa sana yw kukikuza Kiswahili, katika kikao cha bunge kilichopita wqlizindua Kamusi kubwa ya Kiswahili ambayo ina maneno mengi yakutosha kukiwezesha Kiswahili kutumika kufundishia chuo kikuu masomo yote, lengo ni kutumia kiswahili kote nchini, tuzidi kupunguza matumizi ya kiingereza zaidi ya sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Twende mbele turudi nyuma. Hata WaTz hatuongei kiswahili fasaha.
Tusijikute sie ndio wajuvi wa lugha hii
Dada Van, hapa hatuzungumzii ufasaha wa lugha, tunajikita zaidi kwenye ukubwa wa wigo wa matumizi ya Kiswahili, naweza nikakisia kwamba kwa huku tanzania coverage ya kiswahili ni universal, nikimaanisha kimetapakaa zaidi ya 95% ya eneo la nchi, ukija kwenye ufasaha wa lugha yenyewe unapungua sambamba na muinuko toka usawa wa bahari, hali hii ya ufasaha inafanana kati ya Kenya na Tanzania, kadri unavyoiacha bahari, ufasaha wa lugha nao unapotea.

Hapana naona kama kuwabeza wakenya na kiswahili lakini je wewe unaongea kiswahili fasaha?
Si bora kingereza kinacho eleweka kuliko kiswahili cha kuunga unga na maneno ya kingereza ndani yake
 
Hujaelewa mukhtadha mzima wa mazungumzo yetu, hata hao wwkenya wenyewe ninakuhakikishia wamenielewa nini ninamaanisha, nitamuomba MK254, au Tony 254 anisaidie kukuelewesha ninachomaanisha, lakini wataweza tu kukusaidia kama lengo lako ni kuelewa dhumuni la mazungumzo yetu si vinginevyo, ila kama upo kiushabiki nw kiubishani zaidi, hapa sio sehemu muafaka kwako.

Wewe ndio ulianza ni quote. Mimi nilichangia Uzi kama member mwingine yoyote. Wewe ndio ukajaribu kunielekeza kama vile sijui njia. Na ukanipeleka ambako sikua naenda.

Kwahyo sijui ni nani ambaye hajaelewa
 
Hizo salamu za mzunguko ni za wazazi wetu enzi za ujima.

Wewe ndiyo umeleta mzunguko.

Hiyo sentensi "Beef ni ya nini mnayo hivi na kenya" ni mzunguko mno na hauna maana kisemantiki, ungeandika tu "Mna ugomvi gani na Kenya?"
Just like I said 'arrogance substitutes ignorance'.
Waeza address the issue na sio kujaribu shambulia mpinzani.
Cha kustaajabisha wangwana ni ukimhoji mKenya yeyote atakwambia waTanzania wana Kiswahili kizuri, bila kubisha. Ni muhimu kuelewa na kujua kua Kiswahili kama lugha, kabila na tamaduni ni zao la Mombasa, ikiwa ni mchanganyiko wa lugha na desturi za waGiriama na waArabu. Ni muhimu pia kuelewa pale mswahili ina maana ya mwAfrika mweusi nchini Tanzania; Kenya mSwahili ni mtu wa kabila la waSwahili, kutoka pwani ya Kenya.
So ndugu, the fact of the matter is this; mTanzania amgobea kwa Swahili kumliko mKenya no beef, no issues.
 
Umejieleza vizuri sana, kama ambavyo pesa zetu, yaani shilingi ya Kenya na ile ya Tanzania zilivyo na mapungufu mbele ya dolla ya Kimarekani, katika mazingira maalumu tu, ndiyo inapaswa kufanya miamala yetu kwa kutumia pesa nyingine, hasa miamala ya kiserikali, kwa mfano, haiwezikani wizara, au hata wewe mwenyewe nyumbani kwako na familia yako upange bajeti yenu kwa kutumia dola ya marekani...sukari kilogram moja dola ngapi?, unamuuliza mwanao, hivi utaeleweka kweli?.
Tatizo linakuwa kubwa zaidi pale wizara za serikali zinapotumia dollar kwa matumizi yake ya manunuzi ya ndani ya nchi kwa kisingizio kwamba shilingi zetu zina mapungufu, ama zinashuka dhamani kwa haraka sana, au kwa sababu yoyote ile, serikali ikiamua kufanya hivyo inajimaliza yenyewe kwa kuidhohofisha pesa yake yenyewe na wananchi kutoithamini pesa yao hivyo kuongezeka kwa matumizi ya pesa za nje kuliko ile ya ndani. inakubalika kupanga bajeti kwa kutumia pesa za nje katika baadhi ya miradi, hasa inayohusisha nchi za nje, kama vile miradi inayofadhiliwa na wahisani wa nje na mingineyo michache.

Lugha ya kiswahili inajitosheleza kwa zaidi ya 99%, kuendesha shughuli za ndani zote za kiserikali, kama mahakamani, bungeni na hutuba za viongozi kuwahutubia wananchi, kuendesha ibada na mambo yote ya ndani ya nchi, kama tufanyavyo Tanzania, ila katika mambo ya kitaalamu ni kweli kuna mapungufu, japo sio mapungufu ya maneno ila bado maneno ya kitaalamu mengi hayajulikani kwa watu, hivyo haileti maana kuyatumia iwapo yatashindwa kufikisha ujumbe uliokusudiwa.

Serikali yoyote ile inajukumu la kuilinda pesa yake na kusisitiza matumizi ya pesa yake kwa matumizi ya ndani kwa kuonyesha mfano kwa wananchi wake, kwa kufanya miamala yake kwa kutumia pesa yake, sio kwa kusema tu kwamba pesa ya nchi yetu rasmi ni Shilingi lakini yenyewe inalipa mishaara ya wafanyakazi wake interms of $, ndivyo inavyofanya serikali ya Kenya kwenye suala la Lugha, inajinasibu kwamba lugha ya taifa ni kiswahili, lakini shughuli zote za serikali zinaendeshwa kwa kiingereza, matokeo yake Kiswahili Kenya kinazidi kupoteza thamani yake kama vile Dollar ya Zimbabwe inavyopoteza thamani yake.
Sent using Jamii Forums mobile app
I think you have used a wrong analogy yo justify your claim..there is a lot of currency out there superior to the dollar,like the pound but we mostly use the dollar not because our shilling has some problems..just that its easier to use the dollar since its mostly used all over the world just like english..we can communicate with a lot of people out there using english than any other language not that kiswahili is inferior.
We are taught all other subjects in english and learn kiswahili as a subject ..it therefore makes sense when we feel comfortable to communicate in English than swahili but am sure in a sitting exam we will beat most of you..kuongea, we dont care much
 
Hapana naona kama kuwabeza wakenya na kiswahili lakini je wewe unaongea kiswahili fasaha?
Si bora kingereza kinacho eleweka kuliko kiswahili cha kuunga unga na maneno ya kingereza ndani yake
Hii kauli yako nimeitasfri kama vile umeona lengo langu ni kuwabeza wakenya, kwa sababu umeitoa katikati ya mchango wangu, au ulikua unamlenga nani unayeona kama vile anawabeza wakenya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I think you have used a wrong analogy yo justify your claim..there is a lot of currency out there superior to the dollar,like the pound but we mostly use the dollar not because our shilling has some problems..just that its easier to use the dollar since its mostly used all over the world just like english..we can communicate with a lot of people out there using english than any other language not that kiswahili is inferior.
We are taught all other subjects in english and learn kiswahili as a subject ..it therefore makes sense when we feel comfortable to communicate in English than swahili but am sure in a sitting exam we will beat most of you..kuongea, we dont care much
Unataka kuzungumza nini, mbona sikuelewi?.. Nani amezungumzia kuhusu uimara wa pesa?, nani kazungumzia matumizi ya pesa za kigeni Kenya. Soma vizuri mtiririko wa haya majadiliano kwa makini, ukielewa uje kivingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Just like I said 'arrogance substitutes ignorance'.....

Kenya mSwahili ni mtu wa kabila la waSwahili, kutoka pwani ya Kenya.
So ndugu, the fact of the matter is this; mTanzania amgobea kwa Swahili kumliko mKenya no beef, no issues.
Kwenye filamu ya Rambo 2 kuna better version quote inasema "Pride is a poor substitute for ignorance"

Sikumbuki nilipomshambulia mpinzani, nimekijadili alichokileta mezani.

Hii "amgobea" ni neno la kiswahili ambalo sijawahi kulisikia?
 
Unataka kuzungumza nini, mbona sikuelewi?.. Nani amezungumzia kuhusu uimara wa pesa?, nani kazungumzia matumizi ya pesa za kigeni Kenya. Soma vizuri mtiririko wa haya majadiliano kwa makini, ukielewa uje kivingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani sio wewe uliyesema hatufai kutumia dollars kwa kisingizio cha kua shillingi ya tz na ke ina mapungufu....mbona unaruka mchana peupe?umeingiza mpaka zimbabwe mahali kama sijakosea
 
Back
Top Bottom