Ama kweli katika siasa hakuna jambo linalotokea kwa bahati mbaya. Alaumiwe mama Abdul, vijana wa Kaunda suti, au viongozi wa chama?

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,799
Reaction score
14,215
Habari zenu wanaJF wenzangu

Wakuu kuna mambo mengine yanashangaza sana, kiasi ya kwamba sometimes mtu unajiuliza kwamba haya mambo yanayotokea huwa yanakuja tu yenyewe au kuna mtu/watu wanayapanga yatokee kwa sababu fulan.

Kwa leo naomba nizungumzie haya yanayotokea kipindi hiki cha mwezi mmoja baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kwanza kabla ya uchaguzi kulikuwa na malalamiko kutoka vyama vya upinzani kwamba wagombea wa vyama vya upinzani wamekuwa wakikatwa, au wakizuiwa kugombea kwa makusudi, ili wagombea wa CCM waweze kupita katika uchaguzi huo bila kupigwa.

Haya ya watu kuzuiwa kugombea hayajakaa sawa mara uchaguzi ukafanyika bila watu waliokatwa kimakosa kurudishwa kugombea. Inasemekana kwamba licha ya wagombea wa upinzani kukatwa lakini pia waliibiwa kura na kupelekea wapinzani kupanga namna wakavyoishinikiza serikali juu ya jambo hilo.

Sasa wakati wapinzani wanajipanga kudai haki yao ya kukatwa katika uchaguzi na kuibiwa kura. Ghafla tukasikia swala la yule bonge nyanya fulan kutaka kutekwa, mjadala ukahamia kwa bonge na kusahau swala la kukatwa na kuibiwa kura.

Wakati watu wanajadili bonge kukoswa koswa kutekwa, huku baadhi wakiwa bado wanafikiria uchaguzi, ghafla Abdul Nondo na yeye katekwa.

Wakati wote wakiendelea kuvutana kwa kujadili kuhusu utekaji huo nk ghafla linaibuka hili la Mbowe na Lisu kumaliza na kuuzika kabisa mjadala wa uchaguzi wa serikali za mitaa. Kwa sasa kila mtu kahamisha masikio na akili yake kwa Mbowe na Lisu. Walioibiwa kura na kukatwa katika uchaguzi tayari wamesahaulika.

Ndomaana nakumbuka ule msemo wa raisi wa Marekani kwamba katika siasa hakuna jambo linalotokea kwa bahati mbaya. Hii yote inawezekana ikawa ni set-up ili lile la uchaguzi lipite kimya kimya watu wakija kushtuka uchaguzi mkuu huu hapa na waliolalamika kuibiwa kura hawajajipanga.

Ok ngoja tuone mwisho wa hili game.
 
Hawana akili hiyo boss, haya yanayotekea yanatokea sio kwa ajili ya kutaka kuwatoa watu kujadili uchaguzi ule. Acha kutoa uchambuzi usioendana.
 
Ok sawa mkurugenzi
 
Back
Top Bottom