Ama kweli tunatofautiana , Mfanyabiashara umehaso hatimae una bilioni 10, unaendelea kuhaso kumfurahisha nani ? wengine tukizipata tunastaafu mapema

Ama kweli tunatofautiana , Mfanyabiashara umehaso hatimae una bilioni 10, unaendelea kuhaso kumfurahisha nani ? wengine tukizipata tunastaafu mapema

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Ama kweli tunatofautiana. 😂

Kuna watu tayari wamevuka utajiri wa bilioni 10 zisizo na minyororo ya madeni, lakini bado haziwatoshi. Wengine tukizipata hizo bilioni 10 tu, tunastaafu mapema kabisa.

Biashara zenyewe hizi kwetu wabongo kama mnavyojua ukishatangulia warithi wanachowaza ni kuziuza kila moja asepe na chake

Off course hela haiwezi kuwa ya kutumia tu, mfumuko wa bei (inflation) utashusha thamani ya pesa, kiasi cha fedha mfano bilioni 6 inabidi kiwekezwe kwenye vitu kama Treasury Bonds za muda mrefu kama miaka kama 10.

Mwisho wa siku, utajiri si tu kiasi ulicho nacho, bali ni kiwango cha kile kinachokutosha. 💰
 
Ama kweli tunatofautiana. 😂

Kuna watu tayari wamevuka utajiri wa bilioni 10 zako na huna madeni, lakini bado haziwatoshi. Wengine tukizipata hizo bilioni 10 tu, tunastaafu mapema kabisa.

Mwisho wa siku, utajiri si tu kiasi ulicho nacho, bali ni kiwango cha kile kinachokutosha. 💰
Pesa nikama mto , uenda mbele bila kurudi nyuma

Ata ukiwa na pesa kiasi gani inabidi tu uendelee kufanya kazi kwa akili
Kwa maana mto utakauka au pesa zitaisha
 
Sidhani 😄 kuna mda mirija ya pesa inatiririka tu unastaafu vipi?

Kibongo bongo hakuna anaeweza pata tu 10 from no where bila kuuizalisha labda awe fisadi serikalini
10 Billion haifikii hata 5 million dollars

Amini kwamba kuna vijana hata wa 90s wanazo

Achana na hawa wasanii, kuna vijana wapo just quiet lakini pesa wanayo

  • Madini - nchi imejaa madini hii na yanatajirisha wengi, shida ya watu wengi wa huku nidhamu ya pesa ni zero, wanatumia pesa bila discipline
  • Utalii - Kuna pesa sana humu tofauti yao na wa madini hawana kelele
  • Logistics - watu kila siku wanahitaji kusafirisha bidhaa
  • Trading - Kariakoo ndio lango la nchi kama 7 zinazotuzunguka, kuna watu wanaagiza mizigo ya bilion na ikifika tu wanauza hata kwa faida ya bilioni 2, Gari inaenda Congo imejaa betri za simu ndogo zimenunuliwa China kwa 300 zinauzwa buku buku kwa jumla

Halafu sasa nje ya hapo ndo kuna wazee wa siasapreneurship, hao pesa wanayo ndefu sana
 
Sidhani 😄 kuna mda mirija ya pesa inatiririka tu unastaafu vipi?

Kibongo bongo hakuna anaeweza pata tu 10 bilion, from no where bila kuizalisha labda awe fisadi serikalini
Hii ni siri ambayo watu maskini hawaijui hudhani kwamba tajiri mambo yamemnyookea tu automatically hawajui kuwa huo utajiri ulipatikana kwa shida,kwa kujitoa muhanga,kwa kuvuja damu na jasho,wakirelax tu utajiri unapotea wanarudi kapuku tena.
Ndio maana matajiri hawalali usingizi wanawaza jinsi ya kuulinda utajiri wao na kuuongeza zaidi si kwamba hawapendi kula bata.
Kwa mazingira ya bongo asilimia kubwa bila kuwa kauzu,mafia huwezi kuwa tajiri utaishia kupata hela za kubadilisha mboga tu.
 
Kuna level ukifika fursa na pesa zinaanza kukutafuta..

Kingine mwanadamu ameumbwa ku adapt mazingira, jinsi unavyozidi kupata unazoea level ya maisha unayoishi na kuona kawaida... hivyo unazidi kufanya juhudi zaidi ili kupata zaidi..

Pia jinsi unavyopata zaidi ndivyo jinsi una spend zaidi...
 
Ama kweli tunatofautiana. 😂

Kuna watu tayari wamevuka utajiri wa bilioni 10 zisizo na minyororo ya madeni, lakini bado haziwatoshi. Wengine tukizipata hizo bilioni 10 tu, tunastaafu mapema kabisa.

Biashara zenyewe hizi kwetu wabongo kama mnavyojua ukishatangulia warithi wanachowaza ni kuziuza kila moja asepe na chake

Mwisho wa siku, utajiri si tu kiasi ulicho nacho, bali ni kiwango cha kile kinachokutosha. 💰
Levels.

Hiyo hela kuna nyumba Oysterbay hujanunua bado.
 
Levels.

Hiyo hela kuna nyumba Oysterbay hujanunua bado.
Niliona Jay Z na Beyonce wanaishi kwenye nyumba ina thamani ya $200 million Sawa na bilioni 529.4 kwa Tshs.. hio ni nyumba tu....

Sasa uwe na hizo bilioni 10 kwa ukijiona tajiri Kuna siku unatembelea kwa mtu unakuta hizo bilioni 10 zipo parking(magari). Unaanza kujiona masikini.. unatamani na wewe upate zaidi...

Haya maisha ya ajabu sana...
 
Levels.

Hiyo hela kuna nyumba Oysterbay hujanunua bado.
There is always gonna be a thing your money cant buy, hata Elon ni tajiri na kuna kampuni kama Twitter aliweza kuinunua lakini hana pesa ya kuinunua google, microsoft, apple, n.k.

ila 10 Billion doesnt sound that bad kustaafu haso za bongo especially ukishafika 40
 
Niliona Jay Z na Beyonce wanaishi kwenye nyumba ina thamani ya $200 million Sawa na bilioni 529.4 kwa Tshs.. hio ni nyumba tu....

Sasa uwe na hizo bilioni 10 kwa ukijiona tajiri Kuna siku unatembelea kwa mtu unakuta hizo bilioni 10 zipo parking(magari). Unaanza kujiona masikini.. unatamani na wewe upate zaidi...

Haya maisha ya ajabu sana...
Lazima kutakuwa na kitu ambacho hutaweza kununua kwa pesa uliyonayo, ni jambo la kuweza kuishi ndani ya kipato chako na bilioni 10 ukiwa nayo hata ukiishi kwenye nyumba ya milioni 500 mbona poa tu.
 
There is always gonna be a thing your money cant buy, hata Elon kuna vitu hawezi kununua.

ila 10 Billion doesnt sound that bad kustaafu haso za bongo especially ukishafika 40
As long as kuna njia ya kuzizungusha katika investment hata passive.

Lakini kama ni kuzitumia tu, labda kwa standard ya maisha ya chini sana.

Pia, unatakiwa kuwa pdoductive kufanya generational wealth, zisiishie kwako tu, kuwe na kitu cha kuziendeleza hata kwa vizazi.

Things add up, inflation creeps up, lifestyle changes with more money.

Ila sijui, labda kibongobongo ukikaa hapo ndani tu.
 
Ajabu ukistaafu na hio miaka 40, ukifika 50 unajiona mjinga kwanini usingekomaa pengine ungefika mbali zaidi..
Labda wewe ujione mjinga, nchi zilizoendelea, kuna kitu inaitwa FIRE (Financial Independence, Retire Early)

Watu wana jiwekea mikakati ya ku retire mapema wakiwa na 40, cha muhimu pesa tu za kuwa sutain waishi maisha flani mazuri hadi uzee.
 
Mkuu hiyo hela wengine wanachangia chama
1000199333.jpg
 
Lazima kutakuwa na kitu ambacho hutaweza kununua kwa pesa uliyonayo, ni jambo la kuweza kuishi ndani ya kipato chako na bilioni 10 ukiwa nayo hata ukiishi kwenye nyumba ya milioni 500 mbona poa tu.

Suala ni ku spend..
Ni kitu kigumu sana kuwa na bilioni 10 halafu uishi kama mtu mwenye milioni 100...

Bilioni 10 hata private jet ya maana hupati..

Lakini elewa ukipata hio pesa pasipo kuendelea kujituma utafilisika ndani ya muda mchache unless uishi below average... na kuishi below average ni kipaji.. si kila mtu anacho...

Kuna mifano mingi sana ya watu walioshinda lottery hadi dola milioni 100 na baada ya miaka michache wakafilisika...
 
Back
Top Bottom