PreGE2025 Amani Golugwa: Hilda Newton bado hajapatikana, Tunachofahamu alichukuliwa na polisi

PreGE2025 Amani Golugwa: Hilda Newton bado hajapatikana, Tunachofahamu alichukuliwa na polisi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
View attachment 3315188
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema jumla ya majeruhi 21 waliodaiwa kukamatwa na polisi wakati wa kusikiliza kesi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu kwa njia ya mtandao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana Aprili 24, wametambuliwa, hata hivyo, kada wao Hilda Newton hajulikani alipo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 25, 2025 jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), Amani Golugwa amesema kuwa Hilda Newton aliyekuwepo mahakamani hapo akifuatilia kesi hiyo alikamatwa na polisi.

Jana Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alipotoa taarifa za usalama wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo, hakueleza wala kutaja makada wa Chadema waliokamatwa.

Golugwa amesema, “Kama ofisi za chama hatuna taarifa zozote zinazoonyesha Hilda Newton yuko wapi, tunachofahamu ni kwamba, alichukuliwa na polisi, lakini jana katika taarifa iliyotolewa na Muliro (Jumanne Muliro- Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, hakutaja watu walio kwenye mikono ya polisi.

“Pia alitoa taarifa ya mtu mmoja aliyeokotwa kwenye ufukwe wa Coco Beach, taarifa kuhusu Hilda Newton haikutolewa, kwa hiyo mpaka muda huu, sisi ofisi ya chama, hatujui Hilda Newton yuko wapi. Tunachojua ni kwamba polisi walimchukua pale Kisutu, sasa kama walimpeleka Ununio au kituo gani, hatujui,” amesema.

Majeruhi 21

Kuhusu majeruhi 21, Golugwa ametaja majina ya wanachama wao 18 waliodaiwa kukamatwa na Polisi walipokuwa wakielekea kufuatulia kesi hiyo akisema waliteswa kwa kupigwa marungu na wengine wamevunjika miguu na mikono kabla ya kutupwa pori la Mabwepande na wengine ufukwe wa Coco Beach.

Waliotajwa ni pamoja na Makamu Mwenyekiti (Zanzibar), Said Mzee anayedaiw akupigwa mwili mzima, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Ally Juma ambaye naye amedaiwa kupigwa marungu kwenye uti wa mgongo na kuvunjwa mguu wa kulia na mkono wa kushoto.

Soma Pia: Sintofahamu yatawala CHADEMA: Siku ya Pili Kada Hilda Newton hajaonekana

Wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa Fedha wa chama hicho, Tito Kitalika anayedaiw akuwa na hali mbaya kutokana na kipigo alichopata na Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti, Lucas Ngoto aliyevunjwa mguu na Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni, John Pambalu ambaye pia anadaiwa kuvunjwa mguu.

Wengine ni Peter Alex, Emmanuel Severine, Bwire G Bwire, Elizabeth Mangosho, Taliflo Mussa Mussa, Emmanuel Modest Mwihawa, Nasra Said (mwandishi wa habari), Ramadhan Kilengo, Pendo Jonas Kileo, Twaha Mwaipaya, Raphael Makalla mzee wa miaka 70, aliyeteguka mguu.

Wengine ni Shaaban Kirita aliyeokotwa kutoka Coco Beach baada ya kuokolewa na wasamaria wema na Erick Zakaria Bulega.

Amesema majeruhi wengine watatu waliokotwa pori la Mabwepande na msamaria mwema aliyewapeleka hospitali na kuwagharamia matibabu.
Siyo Mabwepande safari ijayo wengine watakutwa misitu ya Katavi, hawataki kufanya kazi wanataka kitonga, nyumbu kwl madaraka hayapatikani kwa njia hiyo
 
Dah wasije wakampoteza binti wa watu like azory, saanane, soka etc
 
Siyo Mabwepande safari ijayo wengine watakutwa misitu ya Katavi, hawataki kufanya kazi wanataka kitonga, nyumbu kwl madaraka hayapatikani kwa njia hiyo
Na mbaya zaidi wanaowatukana majukwaani ndio wanawatandika hasa hasa vunja miguu,vunja mikono,pasua kichwa,fanyia chochote hapo watu Tanzania ya amani iwepo,watu tunafanya biashara tunamajukumu mnakuja kutuletea mambo yenu huku tunadaiwa Kodi,watoto wanadaiwa ada,watu tule kwa amani,ningekuwa ni askari wangeipataaaaaa hakika
 
Back
Top Bottom