Ambao hatujawahi kuchanjwa chale wala kwenda kwa waganga licha ya kuishi kwenye mazingira yenye uchawi sana tukutane hapa

Waliokuwa wanachanjwa walikuwa wanatiwa unga wa mkaa wa dry cell za National Panasonic na Philips
 
Totoo na chale vina tofauti Gani?

Tattoo zote ni uchawi bila kusahau Hina wapakayo women ktk miili Yao, ndomana majanga hayawaishi.
Hina inapakwa nakufutika, haina maumivu wala haiachi athari katika mwili tofauti na tattoo
 
Niliwahi kuwa na rafi yangu tulipokuwa tnajifunza maisha,kila tukianzisha dili anasema twende kwa mganga,nilikataa tokea miaka hiyo,sikuwahi kwenda kwa mganga wala kuchanjwa mpaka hapa nilipofika na nina nafuu ya maisha.
 
Acha kutudanganya, hebu angalia hapo kichwani karibu na utosi uone kama hamna chale tatu.

Mengine yalifanywa na wazazi wetu pasi kujua.

Mengine yamefanywa na wachawi tukiwa tumelala.
Mchawi kama kukuganga au kukuroga,uchawi unaaminiwa na mtu aliyetokea familia lozilozi,kama wewe wanao lazima wawe vigagula maana unamwambia mtu anaejijua mwenyewe kuwa"ACHA KUTUDANGANYA",inaonekana imani yako ni haba kwa muumba.
 
Sina chale wala kitu kinachoitwa kinga sijui ya kiroho lakini naamini ulinzi nliokua nao umeniweka salama mpaka Leo maana nakumbuka miaka mitatu nyuma Luna sehemu nlienda kwenye sherehe nlipigwa kombora ambalo kwa akili zangu za pombepombe nlibeba hicho kitu nkaenda nacho nyumbani nkakichambua vizuri kwenye mwanga nkaona ni majani tu mabichi yamechanganjwa na uchafu unapatikana kwenye utumbo mpana sijui wa kiumbe gani nkaweka kando nkalala asubuhi nkafagia kwa sala na kuendelea na maisha Ila ingenikuta wenyewe walinambia ilikua naenda kupooza kabisaaaaaaaaa
 
Pole sana na hongera sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…