Ambao hawakumuona Mwl. Nyerere, wamemuona Dkt. Magufuli

Ambao hawakumuona Mwl. Nyerere, wamemuona Dkt. Magufuli

Usimlinganishe Hayati Mwl Nyerere na watu wasiofanana nae hata kwa 2% ya utendaji ,sie tuliyaona mengi aliyoyafanya kwa taifa na Africa bila ubaguzi wa kikabila wala kikanda.dont ever repeart such at stupid comparison
 
Tunapoadhimisha miaka 22 tangia kumpoteza Mzalendo wetu, ni dhahiri kwamba Mheshimiwa Hayati JPM ndiye Nyerere wa zama zetu.
Kama JPM ameweza kufufua mashirika ya umma, kukomesha wizi wa madini, kupitia upya mikataba ya madini, kuzuia hujuma ktk miradi ya umeme, kuhuisha reli ya kati na Tazara, kununua meli mpya, vivuko na ndege, kukomesha ujangili wa tembo, kutumbua mafisadi, kukataa maagizo ya mabeberu,
Ni Faraja kwamba Matendo ya Nyerere na Magufuli ni fundisho kwetu kuwa wazalendo, wachapa kazi na kuutetea Uhuru na kulinda rasilimali za Taifa.
Nawatakia Kumbukizi njema yenye Tafakuri kwetu
Mkuu Team JPM, kwanza naunga mkono hoja, pili kwavile sasa JPM hayupo, badili jina uwe Team Sa100.

Hili somo la JPM kama Mwalimu JKN, tulilifundisha kitambo humu
P
 
Nyerere huwezikumling

Huwezi kumlinganisha Nyerere na shetani, mwizi, muuaji, mbinafsi na katili Magufuli. Huenda huwajui wote wawili
 
Paskali acha basi Cha mto wa Mbu??
Mkuu Team JPM, kwanza naunga mkono hoja, pili kwavile sasa JPM hayupo, badili jina uwe Team Sa100.

Hili somo la JPM kama Mwalimu JKN, tulilifundisha kitambo humu
P
 
Kaburi la Nyerere limejengewa kibanda wakati kaburi la jiwe limejengewa bungalow la uhakika
 
Acheni kumfananisha Nyerere na huyo mungu wenu Ibilisi.

Tumeshaanikia maovu yake hapa Kila siku bado mnaendelea kumwabudu tu.

Haya kama una ubavu nenda TANROADS omba structure ya kipande cha barabara wakati wa upembuzi yakinifu kisha baada ya kwisha nenda kapime upana wa hiyo barabara utaona mita moja kutoka kila upande ilivyoibwa na huyo mungu wenu.

Halafu jamaa alipokuwa nyapara wa mabarabara mkandarasi kama hujampa chake kama shukrani lazima akuwekee kiwingu unyimwe tenda nyingine
 
Chato kuna Uwanja wa Ndege wa Lami lakini Butiama achilia mbali Musoma makao Makuu ya mkoa wa Nyerere Uwanja Vumbi tu.


Kwahiyo unataka kusema kwamba Nyerere alikuwa hajitambui kama Magufuli??
 
Acha uongo,Nyerere elimu ilikuwa bure kuanzia msingi mpaka chuo kikuu!Hata JPM ni mnufaika wa elimu bure ya mwalimu Nyerere!
Nyerere aliwaunganisha watanzania wote,ila huyo uliyemtaja alifanya kazi kubwa kubomoa umoja wa kitaifa!
Nyerere alichukia sana ukabila,huyo uliyemtaja aliichukia sana kanda fulani!

NB:Usimfananishe Nyerere na vitu vya ajabu!
mara zote nasema mafisadi, wauza dawa, vyeti feki, wakwepa kodi wataendelea kuwa na mtizamo hasi kwa magufuli mpaka mwisho wa dunia
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Unadhani hicho nisawa

Mwl nyerere alijisahau sana

Charity start at home
Katika vitu ambavyo sikuvipenda kwa baba wa Taifa ni pamoja na hilo...Kutokujipenda kuna sababisha kujikinai na ndiyo maana watanzania hatujipendi tinapenda vya watu zaidi...

Hii ilikiwa weakness yake kubwa...Lakini hii ilitokana na imani yake ya kikristo enzi hizo ambapo ilionekana siyo vizuri kuwa na vingi wakati wengine hawana....

On the other hand JPM aliweza ku balance, aliwapenda wa kwao na akawapenda na wengine...Ni pamoja na kuchukia wale wote ambao walikuwa kinyume na watanzania walio wengi...Kupenda ni pamoja na kuchukia uovu....

JPM ni edited version ya JKN...Hawa wawili historia itawakumbuka...Just give it time...Hata Nyerere miaka hiyo alipewa majina ya ajabu na alichukiwa sana jinsi hii hii tunavyo taka kum brand Hayati JPM; historia ni somo zuri sana...Tutaona huu mwangwi wa ndugu zetu wachache wabinafsi utadumu mpaka lini kuhusiana na JPM....

JPM is a hero the same is JKN utake au usitake, thats it!
 
Nyerere huwezikumlingg

Huwezi kumlinganisha Nyerere na shetani, mwizi, muuaji, mbinafsi na katili Magufuli. Huenda huwajui wote wawili
Hizo sifa zote ulizotoa ndivyo ulivyo wewe...Maana JPM ni kipimo cha uzalendo kwa karne yetu hii...Kama una bisha pitia comments za wa Africa wenzako mitandaoni na hata baadhi ya wazungu wale wenye moyo safi
 
mara zote nasema mafisadi, wauza dawa, vyeti feki, wakwepa kodi wataendelea kuwa na mtizamo hasi kwa magufuli mpaka mwisho wa dunia
Umejitafutia Chaka la kujificha!😃😃😃😃
 
Kwahiyo unataka kusema kwamba Nyerere alikuwa hajitambui kama Magufuli??
Kama kutokujitambua ni jinsi hiyo, yes alikuwa hivyohivyo...Ukitaka linganisha hotuba zao mitandaoni uone...Wanafanana kwa karibu kila kitu hadi kukusema hadharani bila uwoga wala kupepesa jicho!
 
Ndugu yangu, charity kwenye Mali umma? Charity IPO kwenye Mali yako tu sio Mali za taifa ....
nakuambia Ndio maana nyerere

Alijaza JESHI WAKURY NA WAZANAKI NA WAJITA HALAFU JIULIZE KWANINI WALIMU WENGI NA WANASHERI WALIKUWA WATU WA MARA

HAKUNA MTU ULIZA KANDA YA ZIWA UTAELEWA WATUMISHI WENGI WALIKUWA WANATOKEA MARA KIPINDI CHA NYERERE

HIVYI TUSIANZE KUMHUKUMU

MAGU JEMBE
 
Mkuu Gulwa , hakuna kitu kama hicho!, huo ulikuwa ni uzushi tuu wa yule kichaa wa Twitter!.
P
Uzushi gani wakati maiti zilikuwa zinaokotwa ufukweni, lissu anapigwa risasi mchana kweupe na hakuna aliyekamatwa, wakosoaji wanapotezea na kutekwa nk. Mimi ka mkristo mkatoliki ninaamini kuwa kama huna upendo, umejaa chuki na visasi hakuna jema unaloweza kuhesabiwa
 
Back
Top Bottom