Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pale nadhani wakimfanya kama anakua patakuwa hamna mtu wa kuigiza. Hapo itakuja kuonyeshwa labda ameshakuwa mkubwa kabisa.Haha hapa kwetu ndivyo tulivyo maa. Waaris bonge la tamthiliya ila nachukia mtoto hakui tangu alipotimiza miaka 7 haongezeki
Hahaha uongo wa mtoto wa miaka saba kuwa na akili kiasi kile loh. Wild flower mimi sikuimalizaga, hiyo sister's revenge ilikuwaga inaoneshwa saa tano usiku ikarudishwa saa moja kasoro ni fire ila inaelekea kuisha nadhaniPale nadhani wakimfanya kama anakua patakuwa hamna mtu wa kuigiza. Hapo itakuja kuonyeshwa labda ameshakuwa mkubwa kabisa.
Ina uwongo mwingi ila saa 3 kamili lazima niwe kwenye Tv. Ikiisha naunga na wildflower japo nilishaangalia ya Novela E ila ninapenda pia ya kiswahili sana sana Sehemu za Emilia.
Mwenza siku hizi nimekuwa mvivuuu wa kuangalia tv sijui hata tamthilia gani zinaendelea duniani.Mwenza sema
Habari,
Najua mtasema huku hawapo ila naamini wenzangu na mimi wapo maana kwenye msafara wa kenge na mamba wamo.
Startimes wameturahisishia sana tusiojua kizungu, kwa sasa sisi tunaangalia
A sister's revenge (Chinese)
Waaris (Indian)
Village boy (Indian)
Wild flower (wafilipino)
Hizi zote zinaoneshwa channel ya St Swahili (kasoro Village boy)
Wewe unaipenda ipi? Nani humpendi? Nani unampenda?
Uzi tayari
Tunatofautiana boss, wote hatuwezi kuwa busy kama weweNajiuliza mtu mtu unapataje muda wa kuangalia tamthiliya zote hizo, maana wengine masaa24 yanaisha haraka kama masaa10, hata taarifa ya habari tu tunaona kwa bahati kwa nadra itokee tu nimekaa sehemu na ishu nyingine halafu TV iko on.