Ambao huwa tunasubiri majibu mpaka wapenzi wetu wanaoa au kuolewa na watu wengine, tukutane hapa

Jombaa πŸ™ŒπŸ™Œ... Ulichukua uamuzi gani?
 
Mambo ya kuchomeshwa mahindi hayo...hadi anaoa/ kuolewa we unakua unasubiri nini kufanya hivo?!
Dada Evelyn Salt huwa inatokea upo unatumikia ahadi yake labda alikwambia atakuwa tayari kuingia katika ndoa baada ya mwaka mmoja, lakini unakuta hata mwaka haujaisha ashaolewa/ kuoa na mtu mwingine
 
🀣🀣🀣 Dada sio uzembe, ni katika kutunziana ahadi.... Chukulia mfano ww ni mtu wa ofisini na ni ngumu kufatilia mtu wako upande wa pili anafanyaje au yupo na nani... Kwa vyovyote vile utabaki na ahadi tu ya kuwa baada ya muda fulani mambo yatatiki! Sasa bana, mara paap kaoa/kuolewa 😁😁😁😁

Na kama ujuavyo wapo watu wanaweza kukuigizia hapa usijue hata kidogo! Hivi hujawahi ona mwanamke mpaka anaolewa hajulikani km ashawahi kuwa na mtoto? Unakuja kujua baadae sana!

Si uzembe bali kuigiza ndo kunaficha vingi
 
Katika kipindi ambacho watu wengi huwa wanaachwa ni hiki wakiwa chuo.... Wadada walio wengi hushindwa kuwavumilia wenza wao...
 
wanasema fimbo ya mbali ...
 
asiyekuwepo na lake halipo
 
usiyachukulie serious mapenzi. yawaze usiku ukiwa huna la kufanya
 
bora yule dada aliolewa aisee ,maana ndoa ingeyumba. kanenepeana kapoteza mvuto kabisaa
 
Hili Likitokea kwa Girls huwa maumivu Sana ila kwa Boys kawaida na ukiona msichana ameamua kuangalia upande mwingine jua alishakuchunguza akaonana huna future hivyo akaamua aangalie upande mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…