Ambao mna marafiki huwa mnawapataje?

Ambao mna marafiki huwa mnawapataje?

Ukiona shule zote umesoma kuanzia chekechea hadi vyuo hujawahi kuwa na rafiki wa maana endelevu awe mwanafunzi au mwalimu ,kanisani na misikitini ukawa huna pia rafiki endelevu wa maana ulimpata huko ,uende seminar bado huna,mtaani unakoishi huna rafiki jirani wa maana sababu hujali kuwa part ya society mtaani , au kazini huna au kwenye biashara huna business friends wa maana ujue wewe kwenye hii dunia hufai kuishi

Hata kuoana watu wa maana huwapati bar ni area respectable
Hebu fafanua 'areas respectable' kama zipi?
 
Good morning jf....
Tusio na marafiki tukutane hapa😔

Kuna hili swala nimekua nikijiuliza hivi karibuni, baada ya kuona sasa uzee umeanza kupiga hodi. Najiona umri umetangulia mbele halafu maisha ni kama nayaacha nyuma, ni kama naishi tofauti na umri wangu. Nimesogea umri wa kuozesha, kuondokewa na wapendwa (waliozeeka) na kukutana na mambo mengi ambayo nadhani yanahitaji watu....ila bahati mbaya sasa hao watu ndio sina.

Natamani kuwa na marafiki kuwa na watu, watu wa faida, watu ambao wanaweza kushare ramani za maisha, watu ambao tunaweza kupanga safari kwenda vituo vya wahitaji tukawape misaada, watu ambao nikihitaji kumwagilia moyo najua wapo, watu ambao nikikwama najua watakuwepo, kina mama wenzangu huwa wana vyama umuhimu wa vyama naujua ila mi hata chama sijawahi kuwa nacho....naishi mwenyewe mwenyewe tu hadi nawaza si nitakosa wa kunizika mie mwisho nizikwe na manispaa.

Wenye marafiki mnawapataje???
Tuanze kuwa pen pal, wakati nazitathmini tabia zako mbaya
 
Nimeshawahi kuambatana na watu tuliosoma nao lakini niliwa-'drop' baada ya kuona tukikutana 'live' au kwenye 'groups' za WhatsApp ni 'full' mashindano na kuonyeshana nani kafanikiwa na nani kaanguka. Hakuna lolote la maendeleo..🙁
 
Yaani mtu unakuta hana waliocheza nao wakiwa wadogo kijijini au mtaani hana rafiki wa maana hata mmoja haiwezekani.

Mtoto asome mfano shule za kulipia ambako watoto wa vigogo husoma kuanzia wa private sector, Serikalilini,mahakamani na bungeni nk halafu akose rafiki wa maana endelevu huyo bwege
Mkuu inategemea marafiki wa aina gani na wanaokufaa kwa nini.. marafiki wengi ni 'wapigaji tu'.. Anataka umfae yeye na yeye hatakufaa.. Utapata 'marafiki' wengi tu ukiwa na kitu..
 
Nipo post #83 sijaona bado aliyeweza kufafanua ni ipi hasa tofauti ya kufahamiana na mtu na kuwa rafiki na mtu?kwani hivyo viwili vina tofauti?au labda itabidi siku nimtamkie mtu ktk wale tunaofahamiana wewe ni rafiki yangu au yeye anitamkie,tutaelewana kweli si itakuwa ndo mwanzo wakuonana mapunga?hii inanichanganya kiasi nashindwa kujua hata mimi nilikosimamia!

Nafahamiana na watu wengi na tunaheshimiana ila sasa how nitajua huyu ni rafiki huyu siyo rafiki wakati normally tunaenda sawa?mimi ni mtu wakujifungia huwa sipendi kuzurura sipendi starehe sipendi sherehe though nachangia sana hii inaweza kuwa sababu ya mimi kutojua yupi rafiki yupi siyo rafiki?
Rafiki ni mtu ambaye unaweza kumtendea wema bila wewe kutarajia kurudishiwa wema..
Unaweza kumwazima fedha bila maandishi na usijali hata kama hakurudisha lakini akakupa 'uongo' mzuri kama sababu.. 😀
Mtu ambaye anaweza kubeba shida yako kama yake hata kama hana hela..
Mtu ambaye ukipata shida angalau atashauri suluhisho..
 
Dah ukimpta mtu sahihi kwa urafiki utaenjoy sana
Back in days huko primary nilikuwa na rafiki yangu DON dah jamaa alinikubali na mimi nilimkubali sana, baadae tukapoteana kidogo tukakutana tena sekondari
Tulipendana kiasi cha hata ndugu kujua urafiki wetu .
Ila mambo ya chuo haya ndiyo mwanzo wa kuanza kupotezeana kiaina na rafiki yangu
Niko chuo A na yeye chuo B basi ukaribu ukawa mbali kidogo ila mkoa mmoja

Weekend tukawa tukiwa na time tunameet pale Sudan hotel kwa sasa pale sudan_temeke

Ila tukaanza kupoteana katika itikadi mwenzangu akawa tofauti na mwanzo.

Basi nikahama mkoa , yeye akabaki mkoa huo ila mawasiliano nikawa naforce mimi
Mwisho nikapoteza ila namkumbuka sana mwanangu sana tu ila ndiyo vile nabalance shobo tu.
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuwa na marafiki na kuzoeana, Tanzania hii wengi tumezoeana ila sio marafiki, unaowaita marafiki unaweza kuta wanakuombea mabaya zaidi ya unavoweza kufikiri
 
Back
Top Bottom