Ambao mna marafiki huwa mnawapataje?

Hebu fafanua 'areas respectable' kama zipi?
 
Tuanze kuwa pen pal, wakati nazitathmini tabia zako mbaya
 
Nimeshawahi kuambatana na watu tuliosoma nao lakini niliwa-'drop' baada ya kuona tukikutana 'live' au kwenye 'groups' za WhatsApp ni 'full' mashindano na kuonyeshana nani kafanikiwa na nani kaanguka. Hakuna lolote la maendeleo..🙁
 
Mkuu inategemea marafiki wa aina gani na wanaokufaa kwa nini.. marafiki wengi ni 'wapigaji tu'.. Anataka umfae yeye na yeye hatakufaa.. Utapata 'marafiki' wengi tu ukiwa na kitu..
 
Rafiki ni mtu ambaye unaweza kumtendea wema bila wewe kutarajia kurudishiwa wema..
Unaweza kumwazima fedha bila maandishi na usijali hata kama hakurudisha lakini akakupa 'uongo' mzuri kama sababu.. 😀
Mtu ambaye anaweza kubeba shida yako kama yake hata kama hana hela..
Mtu ambaye ukipata shida angalau atashauri suluhisho..
 
Dah ukimpta mtu sahihi kwa urafiki utaenjoy sana
Back in days huko primary nilikuwa na rafiki yangu DON dah jamaa alinikubali na mimi nilimkubali sana, baadae tukapoteana kidogo tukakutana tena sekondari
Tulipendana kiasi cha hata ndugu kujua urafiki wetu .
Ila mambo ya chuo haya ndiyo mwanzo wa kuanza kupotezeana kiaina na rafiki yangu
Niko chuo A na yeye chuo B basi ukaribu ukawa mbali kidogo ila mkoa mmoja

Weekend tukawa tukiwa na time tunameet pale Sudan hotel kwa sasa pale sudan_temeke

Ila tukaanza kupoteana katika itikadi mwenzangu akawa tofauti na mwanzo.

Basi nikahama mkoa , yeye akabaki mkoa huo ila mawasiliano nikawa naforce mimi
Mwisho nikapoteza ila namkumbuka sana mwanangu sana tu ila ndiyo vile nabalance shobo tu.
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuwa na marafiki na kuzoeana, Tanzania hii wengi tumezoeana ila sio marafiki, unaowaita marafiki unaweza kuta wanakuombea mabaya zaidi ya unavoweza kufikiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…