Vijana msidhani kutoa pesa ndio kipimo cha upendo, tena kutoa pesa kwa mtu ovyo bila bajeti. Mtu anasema hilo teni kitu gani wakati hana uwezo wa kuzalisha hilo teni.
Lakini pia kama tutajifunza kuishi kwa bajeti hizi mambo hazitatusumbua. Tatizo letu tunaishi tu ili mradi, hatuangalii maisha ya kesho. Hawa hawa wadada wakiona umepigika wanakukimbia.
Usitumie pesa zako kizembe, bila mipango, usipeleke pesa zako sehemu ambayo haina faida kwako. Kesho yako inategemea sana maamuzi yako ya leo, unaweza kuona 10k ndogo kama wadada wengi wanavyoenda kujibrand, ila hiyo 10k ukijumlisha na nyingine utaona faida yake baadae.