Ameniomba hela ya chai; nimemrushia buku na 200 ya kutolea amekasirika!

Ameniomba hela ya chai; nimemrushia buku na 200 ya kutolea amekasirika!

Salaam!

Katika kusaka faraja murua, juzi kati nilikutana na mdada mmoja hivi murua kabisa. Zoezi la kubadilishana namba likaenda vizuri.

Leo asubuhi na mapema kaniomba hela ya chai; nami, kwa kuzingatia bei halisi ya maandazi huku kijijini ambayo ni tshs 100, nikamrushia buku na mia mbili ya kutolea. Nilifanya hivyo nikiamini kuwa maandazi saba na kikombe cha chai atapata.

Ajabu ni kuwa alipopokea aliniuliza kama mara tatu hivi kuwa nimemtumia au la. Nilipomwambia kuwa ndiyo nimemtumia 1,200 ili apate buku ya chai, hajajibu chochote na hapokei simu mpaka muda huu. Nikafikiri labda amepatwa na ugonjwa kumbe taarifa za kiintelejinsia zinasema ni mzima wa afya tu.

Kuna nini hapa?!!!
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mi nakula 15
maandazi waachie wengine.. wewe soft soft kula vitu lain lain..mayai mayai eeh!!.chapati za maji hiv yan vitu soft usiwe kama hawa mabint wa Chuga... usije ukaumiza utumbo bure.
Nitatuma elf 3 kwa mchanganuo huu
Egg chop 1 - 1,000/=
Chapat za maji lain 2 - 1,000/=
Maziwa fresh - 500/=
Ya kutolea - 500/=.
JUMLA 3,000/=.

HIzi ni rate za posta hapa mtaa wa Samora opposite na NBC bank
 
😀😀😀😀😀😀😀sishibi
 
Back
Top Bottom