Ameniomba Msamaha lakini ameniwekea Masharti

Ameniomba Msamaha lakini ameniwekea Masharti

Ila wewe mbona ishu yako ndogo ..mimi kuna mwana yeye sio tu aliahirisha ila hata manzi ake hakumwambia..Kikeni huko wamejiandaaa kishenzi mavyakula na vilaji kama unavyojua wachaga!.. e bwana eeh!!. Mshkaji hakutokea kabisaaaaaa wala manzi ake hakumwambia kitu yan ilikua bonge la soo na aibu kwa dem..ndugu jamaa walishajaa kupokea mahali na kumwona jamaa ila ikawa tee!!.

Wanawake sas wasivyo na akil wakat mwingine, manzi aliporud dar wakaendelea kuishi na mshkaji..sijui waliyamaliza vp? [emoji23][emoji23][emoji23]
Kama mtu hataki kuoa si aende tu straight,sio kukalisha watu wazima halafu unapotelea mitini,au kama kuna sababu umeiona kwa mwenio na huwezi kuivumilia si uweke wazi? Ukiona mwanaume anafanya hivyo vituko HAJIAMINI
 
Kuna binadam wengine wana historia ndefu sana katika maisha yetu. Niliamua kumusaidia na sikuona sababu ya huyu mpenzi wangu kupaniki na kuomba tuachane. Leo anaporudi na masharti ya kwamba niombe msamaha nyumbani kwao, naona kama ananikoroga kichwa tu.
Bas endelea kuringa.Pole Kwa mwanamke mwenzangu aisee
 
Ni sahihi. Omba msamaha kwa ndugu na jamaa zake.

Omba msamaha uwape tarehe nyingine ya kwenda kutoa ama uende na mahali mkononi unaomba msamaha na unawakabidhi.
 
Jamaa ulichemka Sana

We endekeza tu maneno ya watu kukataa ndoa na kuleta ujana. Kitu unasahau ni kuwa Hao unaowaona marafiki zako leo hutakuja kuwaona kesho ukiwa unaumwa unavaa pampers.

Ujana huwa unawasumbua Sana, stori nyingiiiii ila hamjui ya mbele yenu.

Wewe ulikitolea kuacha kutoa mahali na kujenga familia yako ambayo kimsingi ndio rafiki wako wa kweli na kumsaidia mshkaji, subiri sasa utakuja kuona Nani Atakuwa upande wako katika maisha yako.
Pampasi za kutoka wapi? ni busara sana kutokufikiria mambo ya namna hiyo. Una uhakika kwamba nikiumwa yeye ndo atakua msaada? let's be objective,,,
 
Umemkosea na umempa fedheha kwa familia yake, na Umevunja Ahadi..!!!

Kama ni mimi ningeshakublokilia mbali everywhere kuanzia kwenye Moyo,nafsi,akili etc

Unaonekana hauna msimamo wala clear vision, Mwanaume mwenye Vision habadili plans zake kwa changamoto za ghafla, huyo Dada ningemjua ningemshauri akusahau angaalie maisha yake
Aaah weweeee..sie wanaume bwana angalau tunaokotanaga kwenye maisha ndio maana akaona bora amsaidie mshkaji.Nyie mnalipwa mahali na bado tukiingia humo ndani full magubu na masokomoko kutuloga juu af mwisho wa siku mnatukimbia.

Ila washkaji kuna time hawawez kukutupa inategemeana na history yenu.

Af ukiona jamaa akafanya hivyo inawezekana kabisaaa kuna namna wewe sio kivileee..yan una mizingua
 
Jamaa ulichemka Sana

We endekeza tu maneno ya watu kukataa ndoa na kuleta ujana. Kitu unasahau ni kuwa Hao unaowaona marafiki zako leo hutakuja kuwaona kesho ukiwa unaumwa unavaa pampers.

Ujana huwa unawasumbua Sana, stori nyingiiiii ila hamjui ya mbele yenu.

Wewe ulikitolea kuacha kutoa mahali na kujenga familia yako ambayo kimsingi ndio rafiki wako wa kweli na kumsaidia mshkaji, subiri sasa utakuja kuona Nani Atakuwa upande wako katika maisha yako.
Uyu ni mtoto bado yuko kwao akikua ataacha anaonyesha typically hajitambui na hana muelekeo sahihi katika maisha

Sifa ya mwanaume ni kua na clear vision na uwezo wa kupredict what will happen in nearly future before hujafanya maamuzi

Kuendelea kumshauri ni kupoteza mda
 
Miezi michache iliyopita, nilitengana na mwenzi wangu wa muda mrefu baada ya kusitisha kuota mahari nyumbani kwao na kuamua kumsaidia rafiki yangu ambae alikuwa kwenye changamoto fulani za kimaisha. Nilipomjulisha kwamba nitaahirisha kutoa mahari, hakukubali na aliniomba tuachane. Nilikubali na kumtakia kila la kheri lakini pia nikamsihi kwamba kama atafikiria uamzi wa tofauti basi nitakuwa tayari kumpokea. Jana alinipigia simu na kuomba msamaha. Alijutia sana, hatimae, nikaamua kumsamehe. Jambo gumu ambalo bado linaniumiza kichwa, ni yeye kutaka mimi niwaombe ndugu zake na wazazi wake msamaha kwa kutokupeleka mahari kwa muda tuliopanga.! Kabla sijatoa maamzi, naombeni ushauri. Hili jambo ni sawa?
Nafikiri una umri mdogo/ hauna ustaarabu au hujapevuka kiakili.

Kama ulipata dharura kama hiyo ulitakiwa utumie busara ya kutuma wazee au mshenga akaombe ukweni waahirishe hiyo siku....na sababu kuu mmepata dharura inayohitaji pesa.

Jifunze ustaarabu naona kama unajiona spesho sana.
Hujui kesho yako huenda mkeo au nduguze watakuvusha eneo flani.

Unaweza kuwachukulia poa...haya ni maisha tu...unayemchukulia poa kesho kibao kinakugeuka
 
Ila wewe mbona ishu yako ndogo ..mimi kuna mwana yeye sio tu aliahirisha ila hata manzi ake hakumwambia..Kikeni huko wamejiandaaa kishenzi mavyakula na vilaji kama unavyojua wachaga!.. e bwana eeh!!. Mshkaji hakutokea kabisaaaaaa wala manzi ake hakumwambia kitu yan ilikua bonge la soo na aibu kwa dem..ndugu jamaa walishajaa kupokea mahali na kumwona jamaa ila ikawa tee!!.

Wanawake sas wasivyo na akil wakat mwingine, manzi aliporud dar wakaendelea kuishi na mshkaji..sijui waliyamaliza vp? 😂😂😂
Tuna nafasi yetu special mbinguni
 
Nafikiri una umri mdogo/ hauna ustaarabu au hujapevuka kiakili.

Kama ulipata dharura kama hiyo ulitakiwa utumie busara ya kutuma wazee au mshenga akaombe ukweni waahirishe hiyo siku....na sababu kuu mmepata dharura inayohitaji pesa.

Jifunze ustaarabu naona kama unajiona soesho sana.
Hujui kesho yako huenda mkeo au nduguze watakuvusha eneo flani.

Unaweza kuwachukulia poa...haya ni maisha tu...unayemchukulia poa kesho kibao kinakugeuka
Aisee
 
Kakosea sana yani. Tena kwa Mila zetu wabantu, anatakiwa achapwe viboko na mjomba
Kawadharau sana wazazi wa binti. Halafu kakosa busara, kawaida jambo kama hilo humwambii binti, unatuma wazee. Mahari huwa haimalizwi. Unatuma wazee hata na elfu hamsini wazee wanajua namna ya kuhandle haya mambo na wangemshauri nn cha kufanya. Bora wasioe tu.
 
Back
Top Bottom