Ameniomba Msamaha lakini ameniwekea Masharti

Ameniomba Msamaha lakini ameniwekea Masharti

clearmind

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2013
Posts
813
Reaction score
1,913
Miezi michache iliyopita, nilitengana na mwenzi wangu wa muda mrefu baada ya kusitisha kuota mahari nyumbani kwao na kuamua kumsaidia rafiki yangu ambae alikuwa kwenye changamoto fulani za kimaisha.

Nilipomjulisha kwamba nitaahirisha kutoa mahari, hakukubali na aliniomba tuachane. Nilikubali na kumtakia kila la kheri lakini pia nikamsihi kwamba kama atafikiria uamzi wa tofauti basi nitakuwa tayari kumpokea.

Jana alinipigia simu na kuomba msamaha. Alijutia sana, hatimae, nikaamua kumsamehe. Jambo gumu ambalo bado linaniumiza kichwa, ni yeye kutaka mimi niwaombe ndugu zake na wazazi wake msamaha kwa kutokupeleka mahari kwa muda tuliopanga.

Kabla sijatoa maamuzi, naombeni ushauri. Hili jambo ni sawa?
 
Ila wewe mbona ishu yako ndogo ..mimi kuna mwana yeye sio tu aliahirisha ila hata manzi ake hakumwambia..Kikeni huko wamejiandaaa kishenzi mavyakula na vilaji kama unavyojua wachaga!.. e bwana eeh!!. Mshkaji hakutokea kabisaaaaaa wala manzi ake hakumwambia kitu yan ilikua bonge la soo na aibu kwa dem..ndugu jamaa walishajaa kupokea mahali na kumwona jamaa ila ikawa tee!!.

Wanawake sas wasivyo na akil wakat mwingine, manzi aliporud dar wakaendelea kuishi na mshkaji..sijui waliyamaliza vp? 😂😂😂
 
Kweli hatuna akili....duuuh
 
Ila wewe mbona ishu yako ndogo ..mimo kuna mwana yeye sio tu aliahirisha ila hapa manzi ake hakumwambia..Kikeni huko wamejiandaaa kishenzi mavyakula na vilaji kama unavyojua wachaga!.. e bwana eeh!!. Mshkaji hakutokea kabisaaaaaa wala manzi ake hakumwambia kitu yan ilikua bonge la soo na aibu kwa dem..ndugu jamaa walishajaa kupokea mahali na kumwona jamaa ila ikawa tee!!.

Wanawake sas wasivyo na akil wakat mwingine, manzi aliporud dar wakaendelea kuishi na mshkaji..sijui waliyamaliza vp? 😂😂😂
😄 mapenzi yana nguvu sana aisee. Mimi niliagwa kabisa kwamba nisahau lakini anataka arudi na masharti juu!
 
Miezi michache iliyopita, nilitengana na mwenzi wangu wa muda mrefu baada ya kusitisha kuota mahari nyumbani kwao na kuamua kumsaidia rafiki yangu ambae alikuwa kwenye changamoto fulani za kimaisha. Nilipomjulisha kwamba nitaahirisha kutoa mahari, hakukubali na aliniomba tuachane. Nilikubali na kumtakia kila la kheri lakini pia nikamsihi kwamba kama atafikiria uamzi wa tofauti basi nitakuwa tayari kumpokea. Jana alinipigia simu na kuomba msamaha. Alijutia sana, hatimae, nikaamua kumsamehe. Jambo gumu ambalo bado linaniumiza kichwa, ni yeye kutaka mimi niwaombe ndugu zake na wazazi wake msamaha kwa kutokupeleka mahari kwa muda tuliopanga.! Kabla sijatoa maamzi, naombeni ushauri. Hili jambo ni sawa?
Umemkosea na umempa fedheha kwa familia yake, na Umevunja Ahadi..!!!

Kama ni mimi ningeshakublokilia mbali everywhere kuanzia kwenye Moyo,nafsi,akili etc

Unaonekana hauna msimamo wala clear vision, Mwanaume mwenye Vision habadili plans zake kwa changamoto za ghafla, huyo Dada ningemjua ningemshauri akusahau angaalie maisha yake
 
Jamaa ulichemka Sana

We endekeza tu maneno ya watu kukataa ndoa na kuleta ujana. Kitu unasahau ni kuwa Hao unaowaona marafiki zako leo hutakuja kuwaona kesho ukiwa unaumwa unavaa pampers.

Ujana huwa unawasumbua Sana, stori nyingiiiii ila hamjui ya mbele yenu.

Wewe ulijitolea kuacha kutoa mahali na kujenga familia yako ambayo kimsingi ndio rafiki wako wa kweli na kumsaidia mshkaji, subiri sasa utakuja kuona Nani Atakuwa upande wako katika maisha yako.
 
Jamaa ulichemka Sana

We endekeza tu maneno ya watu kukataa ndoa na kuleta ujana. Kitu unasahau ni kuwa Hao unaowaona marafiki zako leo hutakuja kuwaona kesho ukiwa unaumwa unavaa pampers.

Ujana huwa unawasumbua Sana, stori nyingiiiii ila hamjui ya mbele yenu.

Wewe ulikitolea kuacha kutoa mahali na kujenga familia yako ambayo kimsingi ndio rafiki wako wa kweli na kumsaidia mshkaji, subiri sasa utakuja kuona Nani Atakuwa upande wako katika maisha yako.
Kabisa mkuu
 
Ni kweli ulikosea mkuu
Kuna binadam wengine wana historia ndefu sana katika maisha yetu. Niliamua kumusaidia na sikuona sababu ya huyu mpenzi wangu kupaniki na kuomba tuachane. Leo anaporudi na masharti ya kwamba niombe msamaha nyumbani kwao, naona kama ananikoroga kichwa tu.
 
Back
Top Bottom