Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
Inashangaza sana kwa mwanamke mwenye ndoto ya kuolewa na kuitumikia familia yake kuanza kuweka vikwazo kama anavyoviweka huyu binti
Amepata mwanaume ambaye yuko kwenye mstari mnyoofu wa maisha, ana biashara yake ya kukidhi maisha. Halafu anaambiwa aolewe naye anaanza kuleta vigezo vya umri, mara eti anahitaji aolewe kihalali, ifanyike harusi, mwanaume akajitambulishe ukweni akiwa na kitenge cha mama. Kwa tetesi ninazozisikia ni kuwa ili mtoto aolewe inatakiwa mahali ya Tsh. Milioni tatu 😂😂😂😂
Yaani unapata mwanaume wa kukuoa zama hizi unaleta maringo! Zama za vijana wa kataa ndoa!!? 😂😂 Tena mtu amejijenga vya kutosha! Ee Mola tunusuru, dunia ina vioja vya kila namna
Enyi wanawake wa nchi hii, jaribuni kukua kifikra. Ndoa si maembe mabichi kama ilivyokuwa zamani, kama kweli anania ya kujilipua kwenye hili janga la maumivu, mpe nafasi hiyo mara moja. Ndoa ni bahati siku hizi
Mwenzenu anajikita malaika huku. Tunasubiri aikanyage vyema miaka 30's aende kukanyaga mafuta, afie huko huko kwa msongamano