Deni la ndani la serikali:
Ili kuendeza shughuli zake serikali huwa inachukua mkopo kutoka taasisi za ndani pamoja na kutoka kwa wananchi. moja ya mfumo unaotumika ni kutoa Hatifungani kwa kiingereza tunaiita Government BOND/ Treasury Bond
Mara nyingi nikikaa na wastaafu huwaandalia njia amabzo wanatumia kuwekeza hela zao bila kuanza kuhangaika na biashara ambazo hawajawahi fanya maishani mwao
Hatifungani (mkopo kwa serikali) Hutolewa na Benki kuu ya Tanzania na huiva ndani ya kipindi cha miaka 2,5,7,10,15,20 na 25.
Mnunuzi wa Hatifungani hizi hulipwa riba (coupon) iliyopangwa kila baada ya miezi 6, nikimaanisha riba hulipwa mara mbili kwa mwaka
Kiwango cha chini cha uwekezaji katika hatifungani za muda mrefu ni shilingi 1,000,000 (Shilingi milioni moja) katika mafungu ya shilingi 100,000.
Ununuzi kupitia Benki kuu ya Tanzania (soko la awali) hufanyika kwa njia ya mnada, ambapo wawekezaji watataja bei watakayotaka kununua dhamana (pitia kwa madalali watakusaidia kwenye hili)
Soko la pili: Pia unaweza kununua Hatifungani kupitia Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)
Tuangalie Hatifungani, pamoja na ratiba yake ambapo hutoka kila mwaka wa fedha
Mfano: Ratiba ya zamani ambayo haijumuishi bond ya miaka 25
Auction Date | Bond Tenure | Coupon Rate |
| 01-Jul-20 | 10 YEARS | 11.44% |
| 15-Jul-20 | 15 YEARS | 13.50% |
| 29-Jul-20 | 20 YEARS | 15.49% |
| 12-Aug-20 | 2 YEARS | 7.82% |
| 26-Aug-20 | 10 YEARS | 11.44% |
| 09-Sep-20 | 15YEARS | 13.50% |
| 23-Sep-20 | 20 YEARS | 15.49% |
| 07-Oct-20 | 5 YEARS | 9.18% |
| 21-Oct-20 | 7 YEARS | 10.08% |
| 04-Nov-20 | 20 YEARS | 15.49% |
| 18-Nov-20 | 10 YEARS | 11.44% |
| 02-Dec-20 | 15 YEARS | 13.50% |
| 16-Dec-20 | 20 YEARS | 15.49% |
| 30-Dec-20 | 10 YEARS | 11.44% |
| 13-Jan-21 | 2 YEARS | 7.82% |
| 27-Jan-21 | 15 YEARS | 13.50% |
| 10-Feb-21 | 20 YEARS | 15.49% |
| 24-Feb-21 | 15 YEARS | 13.50% |
| 10-Mar-21 | 2 YEARS | 7.82% |
| 24-Mar-21 | 10 YEARS | 11.44% |
| 07-Apr-21 | 15 YEARS | 13.50% |
| 21-Apr-21 | 20 YEARS | 15.49% |
| 05-May-21 | 7 YEARS | 10.08% |
| 19-May-21 | 20 YEARS | 15.49% |
| 02-Jun-21 | 15 YEARS | 13.50% |
| 16-Jun-21 | 5 YEARS | 9.18% |
NB: unaponunua Hatifungani ya miaka 25 au 20 haimaanishi lazima ukae nayo miaja 20, unaweza ukakaa nayo kwa miezi 6 tu ukamuuzia mtu mwigine
Twende kwenye issue ya mama
Mama ana hela TSH 80,000,000
Bond mpya serikali iliyotoa ni ya miaka 25 yenye coupon ya 15.95% kwa mwaka hvyo basi
0.1595 x 80,000,000 = 12,760,000.00 kwa mwaka
atalipwa 2 times kwa mwaka maana yake kila baada ya miezi 6 atalipwa 12,760,000/2 = 6,380,000.oo
so thamani ambayo kwa mwezi atakayoingiza ni roughly kama 1 M
Endapo asipoiuza maana yake atakaa nayo kwa miaka 25 bila kufanya kazi yoyote atalipwa tu KUMBUKA: MALIPO NI KILAA BAADA YA MIEZI 6 NA SIO KILA MWEZI
Kuna njia pia ya kupata hela kupitia Mnada wa awali ambapo muwekezaji anaweza kununua hatifungani kwa bei pungufu lakini ikija kuuza atauza kwa bei ya juu (Hapa ananunua kutoka BOT anakuja kuiuza kwenye soko la hisa la Dar es salaam)
Jinsi ya kufanya ! wasiliana na madalali watakusaidia
Hatifungani za Muda Mrefu na za Muda Mfupi zina faida zifuatazo:
- Ni njia salama na rahisi ya umilikaji wa dhamana hizi ukilinganisha na mfumo wa umiliki kwa kutumia hati.
- Zinaweza kubadilishwa umiliki.
- Zinaweza kutumika kama dhamana.
- Kipato chake ni kizuri.