Amestaafu na kupewa shilingi milioni mia moja. Anaomba msaada


Tunatunza mzee wetu amegonga 82 sasa hela yake alinunua hisa za NMB na Alijenga nyumba zake 2 za kupangisha zinamsaidia sana kwenye matibabu, kupata diet nzuri safari za kuja dar kwenye checkup kila baada ya miezi 3 au 4 na kumlipa mwangalizi wake na huduma zingine.

Siku akiondoka amesha andika wosia wake vile fedha yake na mali zingine zitakavyo gawanya

Sidhani kama familia ingeweza kugharamia hayo yote kama na yeye angekuwa kapuku, tunaona familia nyingi jinsi wazee wanavyoteseka kwa kukosa ungalizi na inakuwa mbaya zaidi kama mzee hakuwa amejiweka sawa suala la kiuchumi.

Angefanya ujinga huo unausema wewe sidhani kama angefikia hapa alipotamani kufika.
 
Nenda FINCA wana riba mpaka asilimia 14. Kwa kiasi hicho anaweza pokea mpaka milioni moja na point kwa mwezi. Pia kuna makubaliano

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hata mimi nimewaza kitu kama hicho. Mtu umeshazeeka halafu eti hela unataka kuzifungia bank ili usizitumie vibaya. Labda kama ataishi milele.
 
Mwambie anunue BOND za BOT kwa milioni 80 atakuwa anapata milioni moja kila mwezi na akitaka kuuza anauza wakati wowote.
Hivi nyie watu mnakaririshwa ama,hata hati fungani za Serikali nazo zina risk kama business zingine tena mbaya zaidi kwenye Serikali ya awamu hii.
 
Ili asipate pressure na mabiashara akafa mapema mama wa watu...hyo pesa 70m ai fix..atafute bank kubwa kubwa za uhakika wakutofilisika..CRDB.NMB...anegotiate nao wampe % nzur angalau 9%-10%..ingawa 10 sjui...ila kwenye bank zingne njaa njaa..kupata hyo 10-14 zipo...nakumbuka niliwai fix kias kadhaa enz hzo access bank walikua na 14%....nilikua navuta kama 1.2m kwa miez mi3...sasa tatzo za hiv vibank haviaminik.vinaweza tangaza mufilisi muda wowote...BOA bank pia uhakika..

Hyo 10m..afungue duka la chakula limkeep busy..aweke mpesa tigo pea airtel money etc mitung ya gas etc..atulie..
 
Wachache sana watakuelewa katika hili,ukiangalia takwimu za watu matajiri duniani utajiri wao sehemu kubwa umetokana na urithi kutoka kwa wazazi au ndugu.
Yani mzazi ana 80M anataka akaweke fixed huku ana watoto ambao anaweza akakaa nao chini kama familia wakatumia hiyo hela na kufanyia biashara wakasahu kabisa umasikini.wazazi wa kiafrika ni zaidi ya tatizo.
 
Mie Mama yangu alistafu mwaka Juzi alipata 92.5 M tupo watoto 4 moja mwanafunzi nikamwambia Mama tukopeshe hizo pesa sisi 3 tufanye tufanyie biashara tuondokane na umasikini,kilichotokea hakuna hata moja aliyopewa hata shilingi 100.
Leo hii kila siku ananiomba hela ya kula!
 
Hivi nyie watu mnakaririshwa ama,hata hati fungani za Serikali nazo zina risk kama business zingine tena mbaya zaidi kwenye Serikali ya awamu hii.
Mkuu,

Kwa uzoefu wangu wa kuwa na hatifungani za serikali kwa miaka kadhaa, hadi hivi sasa - hawajawahi kuchelewa tarehe yakulipa. Kulinganisha risk yake na business nyingine sio sahihi.
 
Unataka agawe pesa, baada ya miaka miwili aanza kuomba omba pesa kwa watu and then afe kwa stress. Kwanza huyu ana akili, awekeze hizo pesa zake mahala pazuri amalizie uzee wake bila shida ndogo ndogo. Hawezi msaidia kila mtu.
 
Huyo mstaafu hata afanyeje hiyo hela itatumika na itakata tu. Kuna laana fulani wastaafu lazima wapitie ya kupata hela nyingi na mwisho kuishia kuwa tegemezi kwa watoto wao na mwisho kufa wakiwa hawana hata sh, 100. Yeye ni nani aruke hizo stages
Not always the case mkuu usiwafungie watu kwenye box, kuna wastaafu kibao wako mtaani na maisha yanakwenda poa. Bi mkubwa anabiashara tayari ya bucha kulingana na maelezo ya jamaa, it's a good sign. Apate watu sahihi tu wa kumuelekeza pa kuwekeza hatakufa njaa
 
Nadhani kuna aina za fixed account zina hizo features, ukishaifungua unaweka standing order kuwa some amount iwe inatumwa kwenye specified account at specified interval.
 
Amakweli penye miti hakuna wajenzi.
 
Mwambie anikopeshe Mimi halafu mwisho wa mwezi nitakuwa namlipa Milioni mbili km faida na pesa yake itabaki pale pale.Asiwe na wasiwasi maana tutaandikiana mbele ya Wanasheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…