Amestaafu na kupewa shilingi milioni mia moja. Anaomba msaada

Amestaafu na kupewa shilingi milioni mia moja. Anaomba msaada

Hati fungani au bank ndo sehemu nzuri ila kwangu mm hati fungani ndo chagua zuri. Rate kubwa na kila miezi sita unapata gawio lako na pia unaweza kuuza ukitaka na baada ya mda kusiha unarudishiwa fedhha yako yote yote
Vodacom juzi kati walitangaza hawatatoa gawio la faida kwa maana wamepata hasara. Sasa hizo fixed bank deposits na hati fungani haziwezi kuja kusema maneno kama hayo?
 
Mama yangu mkubwa amestaafu na kupewa milioni mia moja. Amechukua milioni 20 na kugawia watoto pamoja na kurekebisha nyumba yake kwa maana tayari alikuwa amekwisha jenga. Sasa amebaki na milioni 80 alikuwa anataka kuziweka bank ili asizitumie vibaya.

Alikuwa anataka bank iwe inamlipa kiaso cha 700,000 kila mwisho wa mwezi kutoka katika hiyo milioni 80 yake. Je kuna bank hapa Dar inatoa huduma hiyo. Hataki kufungua biashara nyingine kwa maana tayari anayo mabucha mawili ya nyama Ubungo na Sinza.

Msaada please.
Kampe Mr. Chicken( kuku), biashara yake imesha halalishwa sahivi
Labda utapata hiko kiwango
 
Ni rahisi sana mwambie aweke fixed deposit kwenye bank either crdb au nmb au Tanzania postal bank ambayo itamlipa 14% na hela yake itabakia pale pale atakuwa anakula faida tuu ndo kitu wanafanya wastaafu wengi kuweka fixed deposit ndo solution ya hii kitu hela tabak tuu na yeye atakuwa anapata faida tuu
 
Yaani unakuwa na hela alafu haujui uzifanyie nini[emoji17][emoji17].
 
Aangalie riba ya kuwa na fixed deposit kwa miezi sita kisha mwaka wanatoa asilimia ngapi. Hiyo pesa ataipata baada ya miezi sita au mwaka kutokana na muda wa fixed deposit yake.
 
Kwanini wakati nao pia wanategemea ku reinvest hiyo pesa ili kumpa mteja wao faida, na biashara kuna kupata na kukosa?
Tembelea stockbroker yoyote posta watakuelezea kiasi cha chini kuwekeza. Hawa ni unaowakopesha ni Bank of Tanzania. Wana process zao lakini hakuna hasara kwa mkopeshaji
 
Mwambie atupie mkeka mmoja matata amuue arsenal na manure atakula bingo moja matata.
 
Hati fungani haziwezi kuja na matamko ya hasara. Bank siwezi fafanua mana sina ujuzi nazo
Hatifungani za serikali haziwezi kuja na matamko ya hasara kwa sababu fedha hizo haziingizwi kwenye biashara - bali zinakopwa na serikali.

Serikali duniani kote, hata huku kwetu, huheshimu sana madeni ya hatifungani. Watachelewesha malipo tele mengineyo wakiwa na upungufu wa pesa - lakini si malipo ya hatifungani.
 
Mkuu mwambie aingie kwenye Beeting niwe nampa odds 1.50 tunaweka 1m tunapata faida laki 5 kwa siku njoo DM tuyajenge
 
Huyu mama ndio mfano halisi wa wazazi wa kiAfrica yani unataka kufungia 80M as if hauna ndugu na jamaa wanashida husikute ata watoto bado wanaitaji boost kwenye maisha yao. Nimeshindwa kuelewa uelewa wa wazee wetu wa kiAfrica yani huu ubinafsi ndio unaturudisha nyuma sana.

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
Fanya kaz mzee, acha kupenda mteremko
 
Ningemshauri atulie kwanza,yaan akili ikae sawa sawa kwanza .afanye Kama vile hazipo .

Kama n mzee wa tungi,atenge million 2 ya kuweka heshima bar[emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom