Amini usiamini, hii ndio thamani ya kichoma taka inayodaiwa na mafundi wa Wizara ya Afya

Amini usiamini, hii ndio thamani ya kichoma taka inayodaiwa na mafundi wa Wizara ya Afya

Wolle Melkas Fernando

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2016
Posts
253
Reaction score
360
Mafundi wa Wizara ya Afya wanaidai kata ya Ipera kiasi cha Tsh. 16,900,000 baada ya kujenga kichoma taka yaani "Medical waste incinerator" Katika Kituo cha afya Ipera.

Kituo hiki kipo Kata ya Ipera wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.

Kwa mujibu wa maelezo ya Diwani wa kata ya Ipera Mh. Festo Myuguye ni kwamba mafundi wa wizara ya Afya ambao walipendekezwa na wizara kujenga kichoma taka hicho wamemueleza kuwa kichoma taka hiki kimegharimu kiasi cha TSh. 16,900,000/= (Milioni kumi na sita na laki tisa.

WhatsApp Image 2022-03-23 at 9.26.41 AM.jpeg
WhatsApp Image 2022-03-23 at 9.26.25 AM.jpeg

Mwonekano wa kichoma taka (medical waste incinerator) kilichopo kata ya Ipera wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma chenye thamani ya Tsh. 16,900,000/=
"Ndugu zangu hicho ndio kichomea taka kilichotokea kituo Cha afya Ipera. Kina sintofahamu kwani mafundi wametoka wizarani lakin gharama ya ujenzi ni milioni kumi na sita laki Tisa kwa mtazamo wa kawaida thamani ya fedha na mradi tunaona havilingani" Amesema Festo Myuguye, diwani wa kata ya Ipera.

Maelezo ya diwani ni kwamba awali walitafutwa mafundi ambao wangeweza kujenga kwa Tsh. 1,300,000/= (Milioni moja na laki tatu tu.

Lakini likatoka agizo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuwa ujenzi huo utafanywa na mafundi wa Wizara na si vinginevyo.

Kama una maoni au utaalam kuhusu ujenzi wa miundombinu ya namna hii, maoni yako ni muhimu sana. Karibu.

WhatsApp Image 2022-03-23 at 9.25.36 AM.jpeg
 
Acheni watumishi wachini wale kwa urefu wa kamba..mgejua wanasiasa naavyotupiga hela msinge wanyooshea vidole watumishi wachini..hata takukuru wanaonea tu watumishi wa chini ila wanasiasa hata hawawagusi.

Wakati ndio wapigaji wakubwa wa hela za walipa kodi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Cha msingi sana hakikisha watoto wako wamekula na wameshiba, ukianza kufuatilia hayo utakufa kwa presha.
Mafundi wa Wizara ya Afya wanaidai kata ya Ipera kiasi cha Tsh. 16,900,000 baada ya kujenga kichoma taka yaani "Medical waste incinerator" Katika Kituo cha afya Ipera. Kituo hiki kipo Kata ya Ipera wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma. Kwa mujibu wa maelezo ya Diwani wa kata ya Ipera Mh. Festo Myuguye ni kwamba mafundi wa wizara ya Afya ambao walipendekezwa na wizara kujenga kichoma taka hicho wamemueleza kuwa kichoma taka hiki kimegharimu kiasi cha TSh. 16,900,000/= (Milioni kumi na sita na laki tisa.

View attachment 2161663View attachment 2161664
Mwonekano wa kichoma taka (medical waste incinerator) kilichopo kata ya Ipera wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma chenye thamani ya Tsh. 16,900,000/=

"Ndugu zangu hicho ndio kichomea taka kilichotokea kituo Cha afya Ipera. Kina sintofahamu kwani mafundi wametoka wizarani lakin gharama ya ujenzi ni milioni kumi na sita laki Tisa kwa mtazamo wa kawaida thamani ya fedha na mradi tunaona havilingani" Amesema Festo Myuguye, diwani wa kata ya Ipera.

Maelezo ya diwani ni kwamba awali walitafutwa mafundi ambao wangeweza kujenga kwa Tsh. 1,300,000/= (Milioni moja na laki tatu tu. Lakini likatoka agizo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuwa ujenzi huo utafanywa na mafundi wa Wizara na si vinginevyo.

Kama una maoni au utaalam kuhusu ujenzi wa miundombinu ya namna hii, maoni yako ni muhimu sana. Karibu.

Kwa uhakika naweza sema, hicho kidude gharama yake ni milioni 5 hadi 6
 
Back
Top Bottom