Amini usiamini, hii ndio thamani ya kichoma taka inayodaiwa na mafundi wa Wizara ya Afya

unapoongelea incenerator unaongelea collection ya vitu,kunakuwa na kichomea taka,shimo la jivu(ash pit),sharps pit na shimo la kutupia makondo(placenta pit).

Gharama ya 1.3m kujenga incenerator ambayo ni acceptable ni uongo.

wizara ina mchanganuo wa ujenzi wa kila kitu katika vituo vya afya
 
Chifu hangaya yupo bize kufungua mabomba ya maji.

Watumishi wake wakizidi kujipimia kwa urefu wa kamba zao.
Kwani kipindi cha jiwe, upigaji ulikwisha?mala ngapi naye alikuwa akilalamika juu ya upigaji?!
 
Ni sawa kabisa maana teknolojia ya kutengeneza hicho wameuziwa na Elon Musk tena kawauzia kabla hata yeye mwenyewe hajaizindua
 
Wahandisi watusaidie labda kimejengwa kwenda chini ....!

Nchi hii ngumu Sana, hivi hakuna uwezekano wa kuuliwa nchi nzima halafu Mungu akaleta watu wapya hapa Tanzania.....!
 
Kiongozi hana mda na hayo mambo kutwa kucha anawaza uchaguzi wa 2025
 
Mkuu hayo mambo Mimi yalinishangaza Mwaka 2019 wilayani Rufiji mkoani Pwani kata ya Mkongo .

Niliona kichomea Taka na kucheki gharama zake ni Million 15 na point zake nikabaki najiuliza tu kwakua mimi sio fundi au cha ajabu Mkuu wa wilaya akapitisha Maisha yakaendelea
 
Mafundi wa Wizara ya Afya wanaidai kata ya Ipera kiasi cha Tsh. 16,900,000 baada ya kujenga kichoma taka yaani "Medical waste incinerator" Katika Kituo cha afya Ipera. Kituo hiki kipo Kata ya Ipera wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma. Kwa mujibu wa maelezo ya Diwani wa kata ya Ipera Mh. Festo Myuguye ni kwamba mafundi wa wizara ya Afya ambao walipendekezwa na wizara kujenga kichoma taka hicho wamemueleza kuwa kichoma taka hiki kimegharimu kiasi cha TSh. 16,900,000/= (Milioni kumi na sita na laki tisa.

View attachment 2161663View attachment 2161664
Mwonekano wa kichoma taka (medical waste incinerator) kilichopo kata ya Ipera wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma chenye thamani ya Tsh. 16,900,000/=
"Ndugu zangu hicho ndio kichomea taka kilichotokea kituo Cha afya Ipera. Kina sintofahamu kwani mafundi wametoka wizarani lakin gharama ya ujenzi ni milioni kumi na sita laki Tisa kwa mtazamo wa kawaida thamani ya fedha na mradi tunaona havilingani" Amesema Festo Myuguye, diwani wa kata ya Ipera.

Maelezo ya diwani ni kwamba awali walitafutwa mafundi ambao wangeweza kujenga kwa Tsh. 1,300,000/= (Milioni moja na laki tatu tu. Lakini likatoka agizo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuwa ujenzi huo utafanywa na mafundi wa Wizara na si vinginevyo.

Kama una maoni au utaalam kuhusu ujenzi wa miundombinu ya namna hii, maoni yako ni muhimu sana. Karibu.

Hata lile banda langu la mbwa lina afadhali
 
Mimi swali langu tu wizara ina mafundi? Yani hiki kichanja si mafundi wa hapo kijijini wanajenga bila shida yoyote?

Swala la kula mimi sina tatizo nao wacha wale mzunguko wa ela urudi mtaani.

Magufuli alikuwa anakula peke yake na wateule wake wachache tu.
 
Mafundi wa Wizara ya Afya wanaidai kata ya Ipera kiasi cha Tsh. 16,900,000 baada ya kujenga kichoma taka yaani "Medical waste incinerator" Katika Kituo cha afya Ipera. Kituo hiki kipo Kata ya Ipera wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma. Kwa mujibu wa maelezo ya Diwani wa kata ya Ipera Mh. Festo Myuguye ni kwamba mafundi wa wizara ya Afya ambao walipendekezwa na wizara kujenga kichoma taka hicho wamemueleza kuwa kichoma taka hiki kimegharimu kiasi cha TSh. 16,900,000/= (Milioni kumi na sita na laki tisa.

View attachment 2161663View attachment 2161664
Mwonekano wa kichoma taka (medical waste incinerator) kilichopo kata ya Ipera wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma chenye thamani ya Tsh. 16,900,000/=
"Ndugu zangu hicho ndio kichomea taka kilichotokea kituo Cha afya Ipera. Kina sintofahamu kwani mafundi wametoka wizarani lakin gharama ya ujenzi ni milioni kumi na sita laki Tisa kwa mtazamo wa kawaida thamani ya fedha na mradi tunaona havilingani" Amesema Festo Myuguye, diwani wa kata ya Ipera.

Maelezo ya diwani ni kwamba awali walitafutwa mafundi ambao wangeweza kujenga kwa Tsh. 1,300,000/= (Milioni moja na laki tatu tu. Lakini likatoka agizo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuwa ujenzi huo utafanywa na mafundi wa Wizara na si vinginevyo.

Kama una maoni au utaalam kuhusu ujenzi wa miundombinu ya namna hii, maoni yako ni muhimu sana. Karibu.

Kula kwa marefu ya kamba
 
Kama mafundi wa wizara inawezekana jamani,kuna posho zao wenyewe wanaita posho ya kazi maalumu......ukichanganya na jinsi vifaa vilivyopanda bei inawezekana lakini.....
 
Hahaahahahah.. daah! Kichomea taka million 16?? Kwahiyo DT, DMO, Afisa manunuzi, Mkurugenzi walipitisha muhtasari kiroho safi..

hebu tuzionee huruma fedha za nchi jaman
 
Chamsingi kimeshajengwa na kimekamilika [emoji817] ,na Kiko standard.hayo mengine achana nayo!!

watu tuna stress za namna gani tunaweza kununua mafuta ya russia kwa malipo ya rubble !!

halafu unatuchanganya na vitu vidogo2
 
Aya Ni Majungu Tu...Baada Ya Kutokuwepo katika mlologo,Hii ni national Cake,Wacha Watu Wapate kulingana Na Professional Zao.

Acha Majungu,Nenda Shule uwepo.

Medical attendat Hapa..
 
Back
Top Bottom