Amini usiamini, hii ndio thamani ya kichoma taka inayodaiwa na mafundi wa Wizara ya Afya

Nakushauri hili bandiko lako ulipeleke Twitter watakusaidia kum tag Waziri Ummy Mwalimu, kiukweli hii haikubaliki kabisa
 
Kula Ni Kula Ubaya Ni Kukomba Mboga Ama
Kupasua Chungu!!!

Kichoma Taka Hoyee!!
 
Nashauri bageti ijayo watenge kama 2tr za kuiba tu ili tuwe tunajua za kuiba nazo zimo kwenye bajeti
Na wasione aibu kuitangaza maana hawaoni aibu kuiba

Sasa hiyo Incinerator wangeagiza toka china wangepata mpaka kama mashine 3 tofauti kwa hela hiyo
Ila maadamu wameruhusiwa kula kidogo sawa
Yaani kidogo 80%
 
Kwanza hakuna Kichoma Taka kinachojengwa kwa kutumia Matofari ya Cement.....!!!
 
Mbona jaman gharama zinalingana, fanya mahesabu kama ifuatavyo:
  • Gharama ya ujenzi mpaka kukamilika 4m.
  • Ulaji wa urefu wa kamba 10m
  • Gharama nyingineno 2m
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Aiseew
 
Mafundi wa Wizara ya Afya wanaidai kata ya Ipera kiasi cha Tsh. 16,900,000 baada ya kujenga kichoma taka yaani "Medical waste incinerator" Katika Kituo cha afya Ipera.

Kituo hiki kipo Kata ya Ipera wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.

Kwa mujibu wa maelezo ya Diwani wa kata ya Ipera Mh. Festo Myuguye ni kwamba mafundi wa wizara ya Afya ambao walipendekezwa na wizara kujenga kichoma taka hicho wamemueleza kuwa kichoma taka hiki kimegharimu kiasi cha TSh. 16,900,000/= (Milioni kumi na sita na laki tisa.

View attachment 2161663View attachment 2161664

Mwonekano wa kichoma taka (medical waste incinerator) kilichopo kata ya Ipera wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma chenye thamani ya Tsh. 16,900,000/=
"Ndugu zangu hicho ndio kichomea taka kilichotokea kituo Cha afya Ipera. Kina sintofahamu kwani mafundi wametoka wizarani lakin gharama ya ujenzi ni milioni kumi na sita laki Tisa kwa mtazamo wa kawaida thamani ya fedha na mradi tunaona havilingani" Amesema Festo Myuguye, diwani wa kata ya Ipera.

Maelezo ya diwani ni kwamba awali walitafutwa mafundi ambao wangeweza kujenga kwa Tsh. 1,300,000/= (Milioni moja na laki tatu tu.

Lakini likatoka agizo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuwa ujenzi huo utafanywa na mafundi wa Wizara na si vinginevyo.

Kama una maoni au utaalam kuhusu ujenzi wa miundombinu ya namna hii, maoni yako ni muhimu sana. Karibu.

Kosa kubwa sana walilolifanya ni kutumia matofali ya saruji badala ya matofali ya kuchoma, matofali ya saruji hayahimili moto.
 
Back
Top Bottom