Amini usiamini ila Airtel ndio Mtandao wenye kasi zaidi ya Internet kwa sasa kupita mitandao yote

Amini usiamini ila Airtel ndio Mtandao wenye kasi zaidi ya Internet kwa sasa kupita mitandao yote

Na huu ni ukaguzi wangu binafsi kutokana na eneo nililopo. Hapa nitatoa kitu kinajulikana km customer feedback.

Awali ya yote mimi ninatumia mitandao yote ya simu yaan Airtel, Yas zamani Tigo/Zantel, Vodacom na Halotel.

Sasa kwa eneo nililopo nimejaribu kufanya tafiti zangu binafsi ili kubaini ni mtandao gani wenye kasi zaidi kupita mitandao mingine.

Niseme tu nimekua mtumiaji wa Airtel, Vodacom na Halotel kwa muda mrefu sana. Yas au Tigo/Zantel nilisimama kuitumia kidogo kwa muda.

Line niliyoipendelea zaidi kwenye Internet ni Airtel na Vodacom ila hapa katikati nikahamia Halotel kupata huduma ya Internet.

Sasa nimekaa nikaanza kukagua hapa nilipo Halotel Internet kuna muda ni majanga yaani mtandao hauna nguvu kabisa speed majanga kabisa yaani mpaka unataka kulia km tupo mwaka 1999.

Nikajaribu Vodacom ikawa ina nguvu ila inaizidi Halotel kwa kiwango fulani H+ 4G inapanda mpaka LTE inapanda 4G/LTE uzuri wa Vodacom speed ipo juu.

Nikatoa nikaweka Yas ni mseleleko yaan speed ni zaidi ya Vodacom na Halotel yaan ni fyaaaaa fyaaaa ukigusa fyaaaaa hakuna kusubiri nikasema hapa ndio penyewe.

Nikatoa Yas nikaweka Airtel yaan mpaka yale maeneo ambayo Halotel na Vodacom mtandao ulikua hausomi unasoma E ila Airtel wamo yaan ni fyaaa fyaaa faya nikibonyeza fyaaaa fyaaa faya speed ndio moto hakuna mfano yaan fayaaa shwaaa.

Kwa speed hii :

1] Airtel nimewapa 4.8/5

2] Yas nimewapa 4/5

3] Vodacom nimewapa 4/5

4] Halotel nimewapa 2.5/5

Halotel waboreshe huduma ya Internet kuna maeneo mtandao ni majanga kwa kweli mpaka line unatamani uiweke sub kabisa usiitumie.

Sasa leo nimenunua kifurushi cha Mwezi Halotel ila muda huu mtandao mpaka nilengeshe eneo yaan ni H+ tu ni ya kulenga kutafuta angle upate Internet na mnara haupandi kabisa 4G yaan ni majanga kabisa mwisho H+. Mpaka nasema ile hela bora ningeenda kununua Pepsi tu kwa Mangi ninywe nijue kimoja.

Airtel wamefunika kwenye kasi ya Internet nimekubari sio mchezo sisi tunaopemda speed km imefungwa turbo wametuweza yaan ukibonyeza shwaaaa shwaaa fayaaaa.

Halotel boresheni huduma ya Internet mnatupa tabu sana wateja wenu yaan kitu kina-load mpaka unajutia pesa zako ulizonunulia bando.

Sina mengine mengi ya kusema. Itoshe kusema nimemaliza kusema.
Possibly upo chini ya mnara
 
Kama unatumia kifaa cha zamani sawa ila kwa sasa 1 gigabit 5G ya Tigo, then 5G voda then wengine, hata kwa 4G wenye 4G lte Advance kama Tigo wapo vizuri, hapa Tigo hata naogopa ku speedtest lte advance yao, maana ni 100-200Mbps speed.
Kuna Raia wapo kama 10 wanataka kununua kifaa washee internet, Location Ni kijijini ambako voda, Yas na Airtel zinafanya Vizuri. Reccomendations wakimbilie wapi na Kwa price ipi??
 
Kuna Raia wapo kama 10 wanataka kununua kifaa washee internet, Location Ni kijijini ambako voda, Yas na Airtel zinafanya Vizuri. Reccomendations wakimbilie wapi na Kwa price ipi??
Sina uhakika mkuu kati ya Voda na Yas, kwa Airtel tuna data humu ina cap 500GB-1TB speed inashuka. Wa test mtandao wa YAS NA voda ama hata hao Airtel upi wanapata Signal nzuri na speed ya uhakika? Wa prioritize huo, 1TB ukijibana hata kama mpo 10 mna survive kila mtu 3GB kwa siku.

Alternative ni TTCL kwa mikoani kama ipo, huwa mikoani customer care ni nzuri compare na dar.
 
Aksante

Aksante, Hapo kwa Cap 500GB-1TB umeniacha gizani, Naomba mwanga kidogo mkuu.
 
N
Mfano speed ni 10mbps kwa sekunde, ukitumia gb 500 unakuwa umemaliza cap yako, wanadrop speed chini ya 1mbps, unakuwa connected ila kwa speed ndogo.
Na hio umesema ni kwa siku Post ya juu?? Yaani GB 500 per day??
 
Airtel ipo kasi sana Aise, 😋😋😋. Shida ni moja ukiwa unaongea na simu mtandao unataka
Hio inaondoka soon mzee saivi wapo Kwenye Phase test ya Kujaribu VolTE na Inaonakana iko well Operational, Mwezi wa Nne probably wata Go Live so kama simu yako ina Volte mambo yatakuwa poa.
 
Hio inaondoka soon mzee saivi wapo Kwenye Phase test ya Kujaribu VolTE na Inaonakana iko well Operational, Mwezi wa Nne probably wata Go Live so kama simu yako ina Volte mambo yatakuwa poa.
Itakuwa unyama sana mkuu, maana imekuwa changamoto sugu sana kwa sisi ambao kazi kubwa tunafanya online huku mawasiliano yakiendelea.
 
Back
Top Bottom