Amini, Usiamini. Nimepona Magonjwa 100+ Kwa Jina la Yesu!

Hakuna kitu kibaya kama kiburi cha uzima,it's as if hakuna Mungu,cha ajabu mtu huyo huyo anayebisha hapa kila Jumapili yuko kwenye ibada......
Umenena vema, mkuu. Jumapili wako ibadani; lakini kwakuwa macho ya mioyo yao yametiwa giza, hata wakisikia, hawaelewi
 
Kwamba umeponywa hautaumwa tena? Vipi wanaopana bila hata kuamini hayo mambo ya Mungu?
Yeye Yesu yuko wakati wowote na mahali popote. Siyo kwamba siumwi ila nikiumwa ninajua wa kumwendea kupata uponyaji. Yeye ni mponyaji wangu na atendelea kuniponya na siyo hayo tu amenikirimia mambo makubwa zaidi ambayo ni uzima wa milele. Siku zangu zikifika mwisho hapa dunani atanipokea kwenye ufalme wake wa milele. Hayo ndiyo makubwa zaidi ya uponyaji. Ninakushauri ukate shauri leo kumpokea huyu mwamba Yesu akupe uzima wa milele. Si unaona watu wanavyokufa ndugu yangu. Fanya haraka sana usije kuchelewa. Tafuta wachungaji wanaohubiri wokovu wakuombee na siyo manabii wa kukupa maji na mafuta. Watumishi wa kweli wanatumia neno la Mungu (biblia) tu kukuombea tena bure.
 
Huwa mna shida kubwa sana ya akili , sijakuomba uniletee mahubiri , kama hauna jibu ungepiga kimya tu
 
We unajua "instant healing" au unaisikia tu? Hizo nutrients ukila unapata instant healing? Biology yako ulisoma wapi, mkuu. By the way, mpe mtu mwenye pepo bubu au kiziwi nutrients zote unazojua uone kama ataongea au kusikia. Lakini kwa jina la Yesu, ni instant healing. Hakuna kusubiri mtu ale eti saltwater fish/enriched breads. Jina la Yesu liko juu ya majina yote ya magonjwa. Ila shetani amewapofusha watu wasijue siri hii. Matokeo yake watu wanateswa na mapepo wanazunguka hospitali zote India, Uingereza na Marekani, wanarudi bila uponyaji.
Mathayo 9:32-33: Walipokuwa wakitoka, tazama, watu walimletea(Yesu) mtu aliyekuwa bubu mwenye pepo. Na pepo alipotolewa, yule bubu alinena; makutano wakastaajabu, wakisema, 'Jambo kama hili halijapata kuonekana katika Israeli.'
 
Hatushangai kusikia kwamba huamini. Hata Waisraeli, Yesu alikuja kwao, wakamuona "live" lakini hawakumwamini.
 
Uliyapima kabla hayo magonjwa 100+?
 
Kama una matege kwanini ungojee kupata instant healing wakati unajua kabisa Vitamin D inahitajika ? Sasa unampa kiziwi nutrients ili aweze kusikia wakati huenda anahitaji hearing aids ?

Kwanini tuna complicate mambo ambayo yapo straight forward kabisa..., ila kama ni kitu Psychological na mind over matter works hata ukimwambia alete kuku mweusi na wewe ku recite Abracadabra za kutosha uneweza kumuaminisha kwamba all is well (Placebo); na mtu alikuwa anasikia maumivu ya kichwa akajiona amepona...
 
Uliyapima kabla hayo magonjwa 100+?
Nipoteze pesa za nini kupima, mkuu? Nikienda hospitali ndio wananipima. Lakini kama nilivyosema magonjwa mengi nimepona kwa muujiza baada ya kuyakemea kwa Jina la Yesu.
 
Nipoteze pesa za nini kupima, mkuu? Nikienda hospitali ndio wananipima. Lakini kama nilivyosema magonjwa mengi nimepona kwa muujiza baada ya kuyakemea kwa Jina la Yesu.
Aiseee..!!! Sasa naelewa kwanini umesema "amini usiamini".
 
Nipoteze pesa za nini kupima, mkuu? Nikienda hospitali ndio wananipima. Lakini kama nilivyosema magonjwa mengi nimepona kwa muujiza baada ya kuyakemea kwa Jina la Yesu.
Kwahio unashauri hata zile Hospitali tuzigeuze kuwa Makanisa, Mahekalu na Misikiti ?
 
Hakuna kitu kibaya kama kiburi cha uzima,it's as if hakuna Mungu,cha ajabu mtu huyo huyo anayebisha hapa kila Jumapili yuko kwenye ibada......
Yamkini mtoa mada ni muongo sana, uongo wake hautukatazi kwenda kusali
 
Nimeshaandika sana humu kama mnaleta shuhuda za uponyaji leteni shuhuda za amputees (waliokatwa mikono au miguu) walioponywa. Hayo mengine mazingaombwe tu!
 
Nimefurahia kiingereza chako japo sijui kama mtoa mada amekuelewa. Seems like you was whistling the wind!😆
 
Narudia kuuliza tena hii imani yenu ya uponyaji imeishia hapo tu? Vipi kuhusu kuwaponya amputees? Mbona hamjibu??? Maana hapo ni kama Mungu wenu hawezi!
 
Hii ni delusion
Wahi kwa psychologist kabla haujapelekwa kwa psychiatrist
I acknowledge your perspective but dissent; what you designate as a 'delusion' epitomizes my profound existential encounter with faith and divine intercession—domains beyond the purview of psychology or psychiatry to adequately delineate or encapsulate.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…