Amini, Usiamini. Nimepona Magonjwa 100+ Kwa Jina la Yesu!

Amini, Usiamini. Nimepona Magonjwa 100+ Kwa Jina la Yesu!

Mtumishi utakuwa una dhambi nyingi sana, Ayubu alipigwa na shetani lakini magonjwa yake hayakufika 100+!
Elon Musk hajapigwa hata na gonjwa moja, Mwamposa, Suguye, Kakobe hawana magonjwa.
Wewe unateswa na magonjwa lukuki unamsumbua Yesu kila siku kukuponya.
Ndo maana wale aliowaponya Yesu aliwaambia "nenda umesamehewa dhambi zako. Wewe husamehewi tuu?
Mbona unajichanganya, mkuu. Kwani Ayubu aliugua kwa sababu ya dhambi? Magonjwa mengine ni kwa utukufu wa Mungu.
Yohana 11:4
Lakini Yesu aliposikia hayo, akasema, “Ugonjwa huu hautaleta mauti bali umetokea ili kudhihirisha utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu apate kutukuzwa kutokana na ugonjwa huu.”
 
100 ni tone, mkuu. The International Classification of Diseases (ICD) by the World Health Organization (WHO) is a system that categorizes diseases and health conditions. The latest version, ICD-11, lists over 55,000 unique codes for diseases, disorders, and injuries!!
Asante mkuu.
Pole sana, magonjwa 100 kwa mtu mmoja sio mchezo.
Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uponyaji.
🙏🏽🙏🏽🙏🏽🙏🏽
 
Huyo Mungu ana nguvu gani?

Huyo Mungu mwenye nguvu mbona ameshindwa na anashindwa kuwasaidia maelfu ya wanawake na watoto wanaoteseka na kufa kwa njaa, vita, magonjwa, majanga ya asili na shida mbalimbali duniani?

Huyo Mungu kama yupo, Ni Mungu mdhaifu, mjinga, mchovu, katili na bandidu na wala HANA msaada wala nguvu yeyote.

Mungu huyo hafai kabisa anastahili kufurushwa.
View attachment 3195668
Una hoja usikilizwe.
 
100 ni tone, mkuu. The International Classification of Diseases (ICD) by the World Health Organization (WHO) is a system that categorizes diseases and health conditions. The latest version, ICD-11, lists over 55,000 unique codes for diseases, disorders, and injuries!!
We binti mzuri na msomi mbona unaandika uongo?
 
#setfree mbonaa mm naomba Kila siku sipati majibu , answer me please 🙏🙏
Usichoke mkuu endelea tu kuomba yan we endelea tu kuomba ipo siku mbingu zitafunguka magorofa na magari yote utayaona yamefunguka
 
#setfree mbonaa mm naomba Kila siku sipati majibu , answer me please 🙏🙏
Suala la kukawia kupata majibu ni somo pana. Kwa ufupi niseme hivi: Mungu anasikia saa ileile tunapomuomba. Wakati mwingine majibu ya maombi yetu yanatolewa saa hiyohiyo lakini huwa yanazuiliwa. Majibu ya Danieli yalizuiliwa kwa siku 21. Soma Danieli 10:12-13. Vile vile majibu ya maombi yanaweza kuwa “ndiyo,” “subiri,” au “hapana,” kulingana na mpango wa Mungu. Na wakati mwingine Mungu anajibu kwa njia tusiyoitarajia. Kitu muhimu ni kuendelea kuishi maisha matakatifu na kuomba bila kukata tamaa na bila kunung'unika; kumbuka hata Yesu aliomba mara tatu kikombe kimuepuke! Mtume Paulo aliomba mara tatu mwiba uondoke mwilini mwake akajibiwa kwamba neema ya Mungu yamtosha! Endelea kuomba, usikate tamaa. Na pia unaweza kuongeza "gia ya maombi" kwa kuwashirikisha Watumishi wa Mungu wakuombee; ila kama nilivyotahadharisha: Mtumishi akikuambia utoe pesa ndio akuombee, mwepuke.
 
Mkuu samahani uyu ndio yule yesu wa kwenye video??
British actors, Brian deacon na Robert Powell. Ndio waigizaji wa filamu ya Yesu.

Na picha za hawa waigizaji ndizo ambazo waafrika wamezibandika majumbani kwao ukutani wakiamini kwamba ndio Yesu.

Kumbe wamepumbazwa tu.

Yesu ni fictional character. Hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.
Screenshot_20250108-110854_1.jpg
Screenshot_20250108-111051_1.jpg
Screenshot_20250108-111222_1.jpg
 
Back
Top Bottom