Amini, Usiamini. Nimepona Magonjwa 100+ Kwa Jina la Yesu!

Amini, Usiamini. Nimepona Magonjwa 100+ Kwa Jina la Yesu!

Setfree asante kwa ushuhuda mzuri lakini napata ukakasi mno na hiyo idadi ya magonjwa. Sidhani kama duniani kuna binadamu ameshawahi kuugua magonjwa yote hayo (kama yapo)
Kama hutajali sana je unaweza kuyaorodhesha hapa!?🙏🏾🙏🏾🙏🏾
Nimeishayataja kwa sehemu, soma replies zangu zote; ila kama wewe ni mzima, mshukuru Mungu usiseme mtu hawezi kuugua magonjwa 100. Codes za magonjwa zipo zaidi ya 55,000 hayo 100 si ni tone tu?
 
Mimi nilianza kuumwa Hasa nikilala usiku na asikia kama maumivu makali kifuani,kama moyo unataka kutoka ,plus shinikizo la juu la damu,mwanzo sikuwa na issue yoyote ya bp,basi nikawa nimeumwa mwaka mzima ,hata kazini nilikuwa siendi kivile,basi nikaendaga kupiga x-ray ,na echo,Dr akasema kwa picha ya x-ray moyo unaonkana umetanuka,na mwenye kipimo cha echo naye akanitisha sana.basi Kuna kipindi ninaomba Mungu aniponyye kwa jina la Yesu.kweli kunA kipindi nikawa sioni BP kupanda Wala nini,Wala siumwi Tena.Basi mwisho nikawa nimeumwa sana ugonjwa tuu haueleweki karibia nife.basi nilivyopona huo ugonjwa nikasema acha niende dar kwenye hospitali moja kubwa tuu nipime Kila kitu ,plus issue za heart kama nipo sawa.basi baada ya vipimo Dr kuniambia moyo wako hauna issue zozote Wala kwenye damu hakuna infection yoyote .kwa kifupi nilipona each and everything kwa jina la Yesu.
Haleluya! Mungu hana upendeleo. Leo hii watu wanakosa baraka hii ya uponyaji kwa sababu ya kutoamini. Try to imagine: mtu unamuambia "nimepona"", anasema nenda Milembe!!
Yesu alipokuwa duniani kuna mahali alienda lakini hakutenda miujiza mingi huko kwa sababu ya kutoamini kwao(Mt 13:58).
 
Sidhani kama binadamu akiwa na magonjwa 30 magonjwa kweli kama organs zake zitafanya kazi tena. Yaani hiyo idadi itatimia huku akiwa tayari ana uraia pacha wa duniani na peponi.
 
Unanipangia cha kusema, kwani mimi sijui tofauti ya magonjwa? Kikohozi na mafua ni sawa? Macho kuuma na upele puani ni sawa? Ngozi kuwasha na majipu ni sawa. Maumivu ya tumbo ni sawa na "kuendesha"?????????????????????????????????????
Hujui tofauti ya dalili na Ugonjwa.

Ugonjwa: Sinus
Dalili: Ukaumwa kichwa, Ukapata mafua, Ukatokwa na kamasi lenye harufu. n.k
 
Sidhani kama binadamu akiwa na magonjwa 30 magonjwa kweli kama organs zake zitafanya kazi tena. Yaani hiyo idadi itatimia huku akiwa tayari ana uraia pacha wa duniani na peponi.
Umesoma sentensi tatu tu ukaruka? Nimekuambia tangu ujana...
 
Huu ni ushuhuda wa kweli kabisa. Katika maisha yangu nimekuwa nikiugua magonjwa mengi ya aina mbalimbali. Kifuani, tumboni, miguuni, katika vidole, machoni, masikioni, puani, kichwani, nk, nk. Muda hautoshi kuyaeleza kwa kina. Kwa haraka haraka naweza kusema tangu ujana wangu nimeugua zaidi ya magonjwa 100. Namshukuru Mungu kwakuwa amekuwa akiniponya magonjwa kila yanaponiijia. Ninachokifanya, kila nikiumwa, namuomba Mungu aniponye kwa Jina la Yesu, kisha naweka mkono wangu juu ya sehemu inayoumwa na kuuamuru ugonjwa utoke kwa Jina la Yesu; kisha naamini kwamba imekuwa hivyo. Wakati mwingine inachukua muda kuona matokeo lakini wakati mwingine ugonjwa unatoweka saa hiyo hiyo. Maneno aliyosema Yesu ni kweli kabisa. Katika Mk 16:17-18 anasema: “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu(Yesu) watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.”

Huu ni uthibitisho kuwa Mungu yupo na anatenda miujiza hata leo kwa watu wanaomuamini. Kwa ushuhuda huu sikuambii usiende hospitali. La, hasha! Ukiwa na pesa, nenda. Nenda hata hospitali za nje ya nchi. Hata mimi kuna wakati huwa naenda hospitali kwa kuwa najua kwamba Mungu anaweza pia kuponya kwa kuwatumia madaktari. Hata hivyo ninapoenda hospitali bado naweka matumaini yangu kwa Mungu kwakuwa najua madaktari nao kuna magonjwa yako juu ya uwezo wao au elimu yao; na wakati mwingine nadhani huwa wanajisahau, badala ya kutia moyo wanakatisha tamaa. Kuna siku nilipungukiwa damu, nikaenda kumuona Daktari. Aliponipima na kuhakikisha damu imepungua, akaniuliza: “Damu umepeleka wapi wewe?” Usipokuwa na matumaini kwa Mungu ukiulizwa swali hilo la kuvunja moyo unaweza ukaugua mara mbili zaidi. Na kwa magonjwa niliyougua, kama kila ugonjwa ningekuwa nakimbilia hospitali, ningehitajika kuwa milionea maana ningepaswa kulipa pesa nyingi za matibabu. Namshukuru Yesu anaponya bila kulipa hata senti. Nawasikitikia wanaosema eti Mungu hayupo. Wanakosa baraka hizi za uzima.

Hata hivyo kuna vigezo na masharti ya kuzingatia ili mtu aone kikamilifu uponyaji wa Mungu kwa Jina la Yesu. Baadhi ya vigezo vimeelezwa katika Andiko hili: Kutoka 15:26. “Mungu akasema, ‘Kama mtaisikiliza kwa bidii sauti yangu mimi BWANA Mungu wenu na kuyafanya yaliyo sawa mbele yangu, kama mtayatii maagizo yangu na kuzishika amri zangu zote, sitaleta juu yenu ugonjwa wowote niliowaletea Wamisri, kwa kuwa Mimi ndimi BWANA, niwaponyaye.’” Uponyaji wa Mungu ni wa bure kwa wote wanaozingatia maneno hayo. Ukisikia Mtumishi anakuambia ulipe pesa kwanza ndio akuombee, jihadhari naye. Yesu alipowapa mamlaka wanafunzi wake ya kukemea pepo na kuweka mikono juu ya wagonjwa ili wapone, aliwaambia amewapa bure, hivyo wanapaswa kutoa huduma hiyo bure(Mathayo 10:8).

Yamkini unaumwa, umetibiwa kila mahali hujapona. Usikate tamaa. Ushuhuda huu ukutie moyo kuwa unaweza kupona kwa uwezo wa Jina la Yesu Kristo. Yote yawezekana kwake aaminiye(Mk 9:23).
Hii ni delusion
Wahi kwa psychologist kabla haujapelekwa kwa psychiatrist

 
Sio watakuwa. Bali ni WAMEBANDIKA picha za waigizaji wa uingereza majumbani kwao ukutani.

Na hili kila mkristo alijue. Kwamba hiyo picha ya Yesu aliyonayo ni picha ya Brian deacon au Robert Powell.
😂😂😂😂😂😂 mkuu ili inatakiwa siku moja tulifungulie uzi kwakweli mana sio powa kabsa
 
Hujui tofauti ya dalili na Ugonjwa.

Ugonjwa: Sinus
Dalili: Ukaumwa kichwa, Ukapata mafua, Ukatokwa na kamasi lenye harufu. n.k
Thank you for pointing that out; I understand the distinction between symptoms and a disease. However, when I shared my testimony, I wasn’t focusing on medical terminology but on how I experienced healing in my life. Whether it was the symptoms or the underlying condition, I truly believe that through prayer and faith, I found relief and restoration. My intent is not to debate definitions but to testify about what God has done for me
Aiseee😂😂😂
I see!
 
Back
Top Bottom