Amini, Usiamini. Nimepona Magonjwa 100+ Kwa Jina la Yesu!

Mbona unajichanganya, mkuu. Kwani Ayubu aliugua kwa sababu ya dhambi? Magonjwa mengine ni kwa utukufu wa Mungu.
Yohana 11:4
Lakini Yesu aliposikia hayo, akasema, “Ugonjwa huu hautaleta mauti bali umetokea ili kudhihirisha utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu apate kutukuzwa kutokana na ugonjwa huu.”
 
Asante mkuu.
Pole sana, magonjwa 100 kwa mtu mmoja sio mchezo.
Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uponyaji.
🙏🏽🙏🏽🙏🏽🙏🏽
 
Una hoja usikilizwe.
 
We binti mzuri na msomi mbona unaandika uongo?
 
#setfree mbonaa mm naomba Kila siku sipati majibu , answer me please 🙏🙏
Usichoke mkuu endelea tu kuomba yan we endelea tu kuomba ipo siku mbingu zitafunguka magorofa na magari yote utayaona yamefunguka
 
#setfree mbonaa mm naomba Kila siku sipati majibu , answer me please 🙏🙏
Suala la kukawia kupata majibu ni somo pana. Kwa ufupi niseme hivi: Mungu anasikia saa ileile tunapomuomba. Wakati mwingine majibu ya maombi yetu yanatolewa saa hiyohiyo lakini huwa yanazuiliwa. Majibu ya Danieli yalizuiliwa kwa siku 21. Soma Danieli 10:12-13. Vile vile majibu ya maombi yanaweza kuwa “ndiyo,” “subiri,” au “hapana,” kulingana na mpango wa Mungu. Na wakati mwingine Mungu anajibu kwa njia tusiyoitarajia. Kitu muhimu ni kuendelea kuishi maisha matakatifu na kuomba bila kukata tamaa na bila kunung'unika; kumbuka hata Yesu aliomba mara tatu kikombe kimuepuke! Mtume Paulo aliomba mara tatu mwiba uondoke mwilini mwake akajibiwa kwamba neema ya Mungu yamtosha! Endelea kuomba, usikate tamaa. Na pia unaweza kuongeza "gia ya maombi" kwa kuwashirikisha Watumishi wa Mungu wakuombee; ila kama nilivyotahadharisha: Mtumishi akikuambia utoe pesa ndio akuombee, mwepuke.
 
Mkuu samahani uyu ndio yule yesu wa kwenye video??
British actors, Brian deacon na Robert Powell. Ndio waigizaji wa filamu ya Yesu.

Na picha za hawa waigizaji ndizo ambazo waafrika wamezibandika majumbani kwao ukutani wakiamini kwamba ndio Yesu.

Kumbe wamepumbazwa tu.

Yesu ni fictional character. Hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…