Amkamata mkewe akichepuka, aponyokwa. Mtoto asiye wake afariki

Anayejua kuwa huyo alikuwa mpenzi wake tu na sio mke wake ni yeye muoaji, maana mke wako ndio mpenzi wako na si vinginevyo.
Taratibu za mke zinajulikana iwe kimila , kidini na kiserikali , nje cha hapo Kwa kigezo ya dini yake ni mzinzi , worst enough kaangukia Kwa single mother , huyo lazima afurahi tuu hamna namna
 
800adc8d1a4863a21fb64185b7984db4.jpg
 
Kwa wingi wa mikasa ya single mothers hapa jf!! Nawasihi dada zangu mjishauri sana kabla ya kuzaa na mtu..
Mikasa ni mingi sana na yote ina jadili kama single mothers ni watu hatari sana.
 
Hapa itakuwa boyfriend mpya na mother wameona wampe msala mlokole. Wauwe msabato anawekwa jela nao wanakulana kwa raha.

Pia single mother anasoma nyuzi za jf amechoka nazo kapata sababu ya kuondoa mtoto na kubaki kivyake.
Kabisa yaaN kwangu mm naamini hiko kiti hata kama n mm siwez fanya msala wa kwenda jelahalafu nisikimbie ni kitu ambacho hakiwezekani hapo mwanaume na mwanamke uyoaliefumaniwa inawezkana wamekula njama kumpoteza msabato
 
Yani alioa Single mothers Sio
Haaa haaaa Single mothers hawezi kupendeka mpk kuolewa
 
Kila siku humu single maza single maza,vijana bado wamekaza mafuvu.
Sasa si bora hiyo jumamosi angekuwa anaenda kazini tu,
Hivi hawa wanawake wote inakuwaje unaangukia kwa mtu wa hovyo?
 
Daaah mpe pole Sana mwamba hizo mambo ni hatari Sana mpe imani na mtie Sana moyo.
Ila usiache kutu update kila hatua
 
Guten Abend.

Leo nimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kushikiliwa kwa kijana mmoja niliyekuwa naye kwenye project moja ya afya nchini. Alikuwa 'Index Tester'. Kijana mmoja ambaye hakika aliipenda kazi na kuifanya kwa bidii. Zaidi, alikuwa mnyenyekevu mwenye misimamo thabiti. Naam, alikuwa ni Msabato. Kwenye dili zilizokuwa zinaangukia Jumamosi zenye posho nene, hakuwahi kuthubutu kuacha siku yake ya ibada kwa ajili hiyo.

Kila iitwapo leo tumuombe Mwenyenzi Mungu atuepushie na mabalaa na kadhia za ulimwengu. Kijana huyu kwa sasa yupo rumande akisubiri kesi yake kunguruma mahakamani.

Kijana huyu miezi kadhaa iliyopita aliamua kuishi na mpenzi wake. Kwa bahati mbaya au nzuri, mpenzi wake huyo alikuwa na mtoto mdogo wa mwaka mmoja na miezi kadhaa. Waliendelea kuishi bila shida. Binti alikuwa akionesha tabia za kutokuwa mwaminifu kwa mwenzake.

Wanasema za mwizi ni 40, lakini palipo na arobaini balaa ndipo huchanua. Bahati mbaya sana, balaa badala ya kumchanulia mwizi na mchepukaji, likachanua kwa kijana mpole na mkamata ugoni.

Akiwa kazini, jamaa anapewa taarifa kwamba mpenzi wake yupo mahali anangonoka na mwenzake. Kwa pupa, jamaa kafika eneo la tukio. Wawili hao wanamponyoka na kufanikiwa kukimbia. Binti alimuacha mtoto nyumbani akiwa kalala. Baada ya kukimbia, akarudi kwao kwenda kutafuta suluhu na msamaha.

Binti anarudi asubuhi kumfata mwanae, kwenda huko kwa wazazi wake. Asubuhi mapema, jamaa akaondoka kuwahi kwenye majukumu yake. Alimuacha mtoto akiwa amelala. Akiwaaga majirani kuwa mama yake atafika muda si mrefu.

Asalaleeh!. Mama anafika na kumkuta mwanae kafariki. Na anadai lazima atakuwa kauwawa na mpenzi wake usiku. Taarifa zafika polisi, jamaa kaenda kubebwa mzobe mzobe akiwa anahudumia wateja wake. Hajui hili wala lile, moja kwa moja polisi kwa tuhuma za mauaji.

Polisi bado wanaendelea na Uchunguzi. Sijapata kufahamu postmortem ilisemaje.

Lakini, hii imenitafakarisha sana. Sijapata kufahamu ukweli wa tuhuma husika. Ila kwa kadri ya ninavyomfahamu, sidhani kama ataweza kufanya huo upuuzi.

Kama kweli kafanya, basi adhabu na iwe juu yake. Vijana jitafakarini katika kuamua kuoa ama kuishi na mwanamke mwenye mtoto. Kama unadhani hutoweza kudhibiti hasira zako, basi achana na mwanamke wa watu. Lamba asali, tembea. Usijibebee mzinga wenye nyuki wakali. Na visasi viwe juu ya wahusika, si watoto. Hawana hatia hata kidogo.

Kama hajatenda, basi Mungu na amnusuru na tuhuma hizo. Vijana msikubali kukaa na watoto wa watu, pelekeni kwa bibi zao. Maana lolote likitokea, mtuhumiwa wa kwanza ni wewe. Kwa kudhani kwamba mtoto si wao, muuaji ni wewe. Mpaka haki ije ipatikane, basi umesota sana.
Gute nacht meine Bruder
 
Kuchomoka kwenye hiyo kesi ni ngum sana.

Ikizingatiwa wasabato wengi ni watu wa Musoma kitu ambacho kinaongeza uzito wa tuhuma.

Hata Kama si mtu wa Musoma lakini wasabato wengi wana mambo ya hovyo Sana wakikasirika.
Wala hakuna ugumu hapo.

Kama wakipatikana wataalamu wazuri wakapima vizuri, inawezekana kabisa kujua ni muda gani mtoto alikufa na alikufaje.
 
Guten Abend.

Leo nimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kushikiliwa kwa kijana mmoja niliyekuwa naye kwenye project moja ya afya nchini. Alikuwa 'Index Tester'. Kijana mmoja ambaye hakika aliipenda kazi na kuifanya kwa bidii. Zaidi, alikuwa mnyenyekevu mwenye misimamo thabiti. Naam, alikuwa ni Msabato. Kwenye dili zilizokuwa zinaangukia Jumamosi zenye posho nene, hakuwahi kuthubutu kuacha siku yake ya ibada kwa ajili hiyo.

Kila iitwapo leo tumuombe Mwenyenzi Mungu atuepushie na mabalaa na kadhia za ulimwengu. Kijana huyu kwa sasa yupo rumande akisubiri kesi yake kunguruma mahakamani.

Kijana huyu miezi kadhaa iliyopita aliamua kuishi na mpenzi wake. Kwa bahati mbaya au nzuri, mpenzi wake huyo alikuwa na mtoto mdogo wa mwaka mmoja na miezi kadhaa. Waliendelea kuishi bila shida. Binti alikuwa akionesha tabia za kutokuwa mwaminifu kwa mwenzake.

Wanasema za mwizi ni 40, lakini palipo na arobaini balaa ndipo huchanua. Bahati mbaya sana, balaa badala ya kumchanulia mwizi na mchepukaji, likachanua kwa kijana mpole na mkamata ugoni.

Akiwa kazini, jamaa anapewa taarifa kwamba mpenzi wake yupo mahali anangonoka na mwenzake. Kwa pupa, jamaa kafika eneo la tukio. Wawili hao wanamponyoka na kufanikiwa kukimbia. Binti alimuacha mtoto nyumbani akiwa kalala. Baada ya kukimbia, akarudi kwao kwenda kutafuta suluhu na msamaha.

Binti anarudi asubuhi kumfata mwanae, kwenda huko kwa wazazi wake. Asubuhi mapema, jamaa akaondoka kuwahi kwenye majukumu yake. Alimuacha mtoto akiwa amelala. Akiwaaga majirani kuwa mama yake atafika muda si mrefu.

Asalaleeh!. Mama anafika na kumkuta mwanae kafariki. Na anadai lazima atakuwa kauwawa na mpenzi wake usiku. Taarifa zafika polisi, jamaa kaenda kubebwa mzobe mzobe akiwa anahudumia wateja wake. Hajui hili wala lile, moja kwa moja polisi kwa tuhuma za mauaji.

Polisi bado wanaendelea na Uchunguzi. Sijapata kufahamu postmortem ilisemaje.

Lakini, hii imenitafakarisha sana. Sijapata kufahamu ukweli wa tuhuma husika. Ila kwa kadri ya ninavyomfahamu, sidhani kama ataweza kufanya huo upuuzi.

Kama kweli kafanya, basi adhabu na iwe juu yake. Vijana jitafakarini katika kuamua kuoa ama kuishi na mwanamke mwenye mtoto. Kama unadhani hutoweza kudhibiti hasira zako, basi achana na mwanamke wa watu. Lamba asali, tembea. Usijibebee mzinga wenye nyuki wakali. Na visasi viwe juu ya wahusika, si watoto. Hawana hatia hata kidogo.

Kama hajatenda, basi Mungu na amnusuru na tuhuma hizo. Vijana msikubali kukaa na watoto wa watu, pelekeni kwa bibi zao. Maana lolote likitokea, mtuhumiwa wa kwanza ni wewe. Kwa kudhani kwamba mtoto si wao, muuaji ni wewe. Mpaka haki ije ipatikane, basi umesota sana.
Kama baya umeandikiwa kamwe kulikwepa hutoweza, maisha ni fumbo kikubwa ni kuamua kuishi tu, vita ya maisha na unabii hatuna uwezo wa kuyasemea, bunafsi nafanya kila jema lililo mbele yangu .

NB: Hata jambo jema hua na matokeo hasi wakati mwingine.

Kama hayajaamua kukuta waweza jivika gamba lenye sura ya ushujaa.
 
Back
Top Bottom