Wakuu, kuna kitu kinaitwa "divide and conquer", yaani "tawanya utawale".
Kuna mifano mingi sana, wadau wa historia mna ushahidi.
Ukweli ni kwamba, wapo watu wa bara wengi wenye mali na familia Zanzibari, vile vile wapo watu wa Zanzibari wengi wenye mali na familia bara. Infact wapo watu wengi wenye asili mchanganyiko toka enzi za mababu na mababu zao. Huwezi kutofautisha mtu wa Zanzibari ni yupi na wa bara ni yupi. Wote ni wa Tanzania.
Amkeni!!! Propaganda za kitoto hizi.
Mfano, Wakenya huwa wanakumbukaga makabila yao wakati wa siasa tu. Ila wame intermarry kila kona, na wanapendana na kutaniana balaa.
Tujiulize. Ni nani anafaidika na propaganda hizi?!!! Amkeni!!!