Amkeni Watanzania, nchi yetu siyo masikini; ni kikundi cha watu wachache kinaitafuna

Acheni kupumbazwa nakauli za CCM kuwa Tanzania ni maskini lipo kundi dogo ndani ya CCM linaitafuna hii nchi kwa kupeana vyeo mbalimbali katika maeneo mbalimbali.

Nchi yetu siyo maskini bali kundi la watu wachache ndani ya CCM ndiyo majizi makubwa yanayitafuna fedha za umma na kuingia mikataba mibovu katika mali asili zetu.

Wewe Mtanzania amka kataa kundi hilo la ukoo wa kambale linaloharibu nchi yetu, kubadili chama siyo kigezo cha kuwamaliza watu hao katiba mpya ni mwarobaini wa hayo yote na sheria kali ambazo zinatokana na Katiba hiyo.

Nchi yetu inaliwa mnoo amkeni amkeni Watanzania tusiburuzwe na kundi hilo amkeni
Kweli, skiingia Rais mgalatia wazungu wanakula
akiingia upande huu mwingine makucha ya waarabu, wahindi, wachina balaaa hadi unga unauzwa

hii nchi vipi?
 
Watanzania ni sawa na watu wanaolilia kwenda polar regions kwa sababu picha tu walizoona zinavutia.

Kinachowavutia kwenda na uhalisia wa kuishi huko ni vitu viwili tofauti.

Sasa wewe jichuze kuwaongoza huko wanapotaka kwenda uone kasheshe lake. Mjomba lawama zote utapewa katikati ya safari ukishaanza kuwalaza kwenye matent na baridi, kuwapeleka kuvua samaki kwenye mto wa barafu.

Yaani shida kidogo wewe uliewapeleka huko ndio tatizo hufai ata kidogo wakati wao wenyewe ndio walikufuata wanataka kuishi Antarctic.

Hao ndio watanzania wanataka mabadiliko isipokuwa hawajui safari yenyewe ikoje.

Ndio, Magufuli alikuwa na mapungufu yake, lakini kitu ambacho kaonyesha dunia na hasa waafrica hatuko tayari kwa mabadiliko.

Watanzania wanadhani ipo siku mafisadi wataamka tu na kuwa na huruma nao, bila ya kiongozi mmoja wa kupambana nao kuwabadili tabia.
Una uhakika kuwa yeye miongoni mwa wanaCCM hakuwa fisadi?

Ni mapungufu gani hayo aliyokuwa nayo yaliyokuwa nafuu kwetu kuliko ufisadi? Imekuwa kawaida kumuelezea magufuli “pamoja na mapungufu yake …” Yapi?

Ninachojua kivutio kikuu cha CCM ni fursa za wizi/ufisadi unaosimamiwa na dola chini ya chama hicho (KLEPTOCRACY). Ndivyo ilivyokuwa mwanzo hadi sasa. Na tutaendelea kushuhudia hujuma hizo za dola mpaka tuwe serious - kama tutaamka na kuwaondolea guarantee ya kuongoza nchi.
 
Acheni kupumbazwa nakauli za CCM kuwa Tanzania ni maskini lipo kundi dogo ndani ya CCM linaitafuna hii nchi kwa kupeana vyeo mbalimbali katika maeneo mbalimbali.

Nchi yetu siyo maskini bali kundi la watu wachache ndani ya CCM ndiyo majizi makubwa yanayitafuna fedha za umma na kuingia mikataba mibovu katika mali asili zetu.

Wewe Mtanzania amka kataa kundi hilo la ukoo wa kambale linaloharibu nchi yetu, kubadili chama siyo kigezo cha kuwamaliza watu hao katiba mpya ni mwarobaini wa hayo yote na sheria kali ambazo zinatokana na Katiba hiyo.

Nchi yetu inaliwa mnoo amkeni amkeni Watanzania tusiburuzwe na kundi hilo amkeni
Screenshot_20220625-110005.jpg
 
Watz tunapandikizwa uoga tangu utoton kwa hyo akili zetu zna ufinyu wa mawazo. Mfano mtu uko chuoni anatishiwa usiponunua notes basi nakufelisha sasa mtu kama huyo atakua na uwezo wa kuhoji kweli?
 
Una uhakika kuwa yeye miongoni mwa wanaCCM hakuwa fisadi?

Ni mapungufu gani hayo aliyokuwa nayo yaliyokuwa nafuu kwetu kuliko ufisadi? Imekuwa kawaida kumuelezea magufuli “pamoja na mapungufu yake …” Yapi?

Ninachojua kivutio kikuu cha CCM ni fursa za wizi/ufisadi unaosimamiwa na dola chini ya chama hicho (KLEPTOCRACY). Ndivyo ilivyokuwa mwanzo hadi sasa. Na tutaendelea kushuhudia hujuma hizo za dola mpaka tuwe serious - kama tutaamka na kuwaondolea guarantee ya kuongoza nchi.
Kwa nchi kama Tanzania ufisadi aupo CCM tu, ni sehemu ya maisha ya kila siku.

Kila mtu anachota kwa nafasi yake tofauti ni viwango na fursa; mwenyekiti wa mtaa atabugia michango ya wenzake; na kutaka kitu kidogo kabla ajapiga sign barua yako ya serikali vinginevyo kila ukienda atakwambia yupo busy. Kila ukubwa wa nafasi unakuja na ongezeko la fursa.

Kwa ivyo kusema Magufuli was clean ni too optimistic tofauti walau yeye alikuwa anajaribu kubadili culture ya kila mtu kuwa mwizi na watu walishaanza kuogopa.

Kwa raia yeyote kwenye nchi kama hiyo akiambiwa achague serikali ya wezi wachache huko juu ambao ubadhirifu wao mpaka ifanyike special audit ili ubainanike au uchague serikali ambayo kila mtu mwizi ata mwenyekiti wa mtaa kuandika sign na kupiga muhuri wa utambuzi kwenye form za serikali bila ya kumpa elfu 10 kila ukienda atakwambia yupo busy njoo kesho.

Ni hivi uwezi fananisha serikali ya Magufuli na mtu mwingine yeyote ata enzi za Nyerere watu walikuwa wanaiba; tofauti ya hao wawili na wengine ni jitihada za wazi za kupambana na hizo tabia kuwa sehemu ya maisha kwa kila mtumishi wa chama na serikali.

Mapungufu ya Magufuli kwa upande wangu ni kujaribu ku impose his personal moral views kwa kila mtu kwa kutumia nguvu za nafasi yake mfano kukataa chanjo za COVID, kuingilia utaratibu wa kangomba; among other things.
 
Umeongea ukweli..bila kuamua kwa damu na jasho tutabaki tunalia na kulalamika.

#MaendeleoHayanaChama

Damu na jasho la nani? Hata kuandamana mnaogopa halafu unaongelea kumwaga damu. Ni Wazanzibari pekee tunajua kupigania haki zetu. Nyie ni keyboard warriors tuu.
 
Watanzania ni sawa na watu wanaolilia kwenda polar regions kwa sababu picha tu walizoona zinavutia.

Kinachowavutia kwenda na uhalisia wa kuishi huko ni vitu viwili tofauti.

Sasa wewe jichuze kuwaongoza huko wanapotaka kwenda uone kasheshe lake. Mjomba lawama zote utapewa katikati ya safari ukishaanza kuwalaza kwenye matent na baridi, kuwapeleka kuvua samaki kwenye mto wa barafu.

Yaani shida kidogo wewe uliewapeleka huko ndio tatizo hufai ata kidogo wakati wao wenyewe ndio walikufuata wanataka kuishi Antarctic.

Hao ndio watanzania wanataka mabadiliko isipokuwa hawajui safari yenyewe ikoje.

Ndio, Magufuli alikuwa na mapungufu yake, lakini kitu ambacho kaonyesha dunia na hasa waafrica hatuko tayari kwa mabadiliko.

Watanzania wanadhani ipo siku mafisadi wataamka tu na kuwa na huruma nao, bila ya kiongozi mmoja wa kupambana nao kuwabadili tabia.
WATANZANIA WALIOWENGI NI WAPUMBAVU SANA WANATAKA KWENDA MBINGUNI ILA WANAOGOPA KUFA😡
 
Watz tunapandikizwa uoga tangu utoton kwa hyo akili zetu zna ufinyu wa mawazo. Mfano mtu uko chuoni anatishiwa usiponunua notes basi nakufelisha sasa mtu kama huyo atakua na uwezo wa kuhoji kweli?
TUNA TAIFA LILILOJAA WAOGA NA WAPUMBAVU WENGI SANA😡
 
Back
Top Bottom