Amnesty International and Human Rights Watch: Hali ya ukandamizaji wa vyombo vya habari, watetezi wa haki za binadamu na vyama vya upinzani waongezeka

Amnesty International and Human Rights Watch: Hali ya ukandamizaji wa vyombo vya habari, watetezi wa haki za binadamu na vyama vya upinzani waongezeka

Kabla hamjatoa hizi comment muwe mnaangalia hizo nchi mnazoshabikia zinafanya mabaya mangapi na hawaguswi na the so called Mahakama ya Kimataifa. Libya imefanywa nini na je walioifanya hivyo wamechukuliwa hatua gani? Iraq, Afghanstan na nchi nyingine nyingi tu wameziharibu lakini kimya. Huko huko Marekani watu weusi wanauwawa mchana kweupe lakini haya yanayojiita mashirika ya upuuzi yamekaa kimya wala darubini zao hazimuliki huko.

Kila nchi inautamaduni wao jinsi ya kuishi, wengine wanapenda kuwa wakimbizi, wangine kupigana risasi, wengine ubaguzi, wengine wanaishi kwa chuki kwa sababu wamekosa Uhuru, Amani, na upendo muda mrefu hawakuipata. Na yote haya yanatokana na kunyanyaswa, kukosa ajira, rushwa, uwongo, chuki, kutokuheshimiana n.k.

Afadhali leo tumepata watu wakutukumbusha kama hawa inamaana wanatupenda na sisi lazima tuone kwa nini kelele zimekuwa nyingi hivi?

Na hayo uliyoyataja hapo juu yatakuwa yametoka aidha kwa babu na bibi zao au kwa baba na mama zao. Wewe unafikiria maisha ya leo badala ya kesho. Mimi na wewe tunatakiwa tujenge nchi yetu sio tubaguane ili kizazi kinachotuangalia kituige.

Leo tunaweza kupambana mimi na wewe kwa mdomo lakini kesho vijana wetu watapigana kwa mapanga na risasi lwa akili ya madaraka. Roho yangu mimi na wewe itatusuta tutasema kwa nini hatukukaa tukawatengenezea hawa vijana maisha kama waliopita walivyotuandalia?

Ila inaonyesha una ubinafsi au ni mvivu wa kufikiri au unasoma kwa kukariri. Jaribu uwe na rafiki wa kizungu utabadilika.

Nakuombea hizo chuki zikutoke usije kupelekea kizazi chetu cha kesho maisha kama ya somalia.

Watanzania walishakubaliana ili kuondoa mzizi wa fitina nchi yetu hii katiba irekebishwe na kweli ikarekebishwa. Huyu aliyeificha anaitakia nini Tanzania au watoto wetu? Si anataka vita au?
 
CodeDesigner,
Swala la sheria sio la upande mmoja ni kwa pande zote Serikali na Wanachi kwa pamoja kuzingatia sheria na kanuni. Hivyo wote Ni muhimu kufuata sheria na sio kukandamiza upande mmoja
Ulichonena ni kweli: sasa ukiona upande mmoja unakosewa ni lazima wa pili ushike hatamu kudai haki yake ni sawa sawa wale wanaikosea serikali ni lazima serikali iwakumbuhse sheria na kuisimamia halikadhalika raia wataikumbusha serikali juu ya haki zao
 
Wako sahihi 100%, ila tatizo wazungu unafiki umejaa Na wanaendelea kuidhamini serikali inayokandamiza haki za binadamu
 
Hamia huko US au Ulaya wanakowabagua weusi la wala hutasikia ya Amnesty!

Ni bora huko wanawabagua wenye rangi tofauti na wao, hapa kwetu tumeanzisha ubaguzi wa vyama, itikadi na kabila nk. Kuna watu wanaonekana si lolote just because hawaipendi CCM kuna watu hawapelekewi maendeleo kisa walimchagua mtu wa chama tofauti na chama tawala. Tofauti yenu na hao ni nini?
 
Ushamba mzigo sana. So kwako kusafiri ulaya na marekani ni kipaumbile kuliko maslahi ya taifa lako.
Hii nchi ni maskini sana ikibanwa mbavu ndio mtaelewa haya ninayosema, Huyo Jiwe anawadanganya kwamba tuna utajiri hatuwezi kubembeleza mtu !!, waulizeni warusi na wakorea, vikwazo maana yake unazuiwa kununua na kuuza kwa uhuru
 
Hawa Amnesty siku zote wanatoaga ripoti za kuchonganisha watu.

Hebu watuache, watanzania tupo shwari hatuna shida na ripoti zao sio muhimu sana
 
@"Dalalims, post:

Tanzania tupo shwari kwa sababu hakuna ndugu yako ndani?
Au kwa kuwa wewe ni mnufaika na mfumo CCM?
 
Watoe mfano wa nchi yoyote duniani ambako kuna UHURU usio na mipaka na HAKI isiyo na kuwajibika.
Kama raia ukiona anapingana na report hiyo kuna mawili. Moja ni kuwa ni zuzu haelewi hata alisemalo au hiyo ripoti inasemaje au pili, ni mnufaika na serikali kwa hayo itendayo.
Unapaswa kujiuliza kwa nini lawama hizo na humu ndani zinalalamikiwa?
 
Waambieni hao amnesty international kuorights watch kuwa waende spain wakawasaidie wale viongozi wa catalonia wanaotaka kujitenga walioko ndani mpaka sasa watoke ndo waje huku tz na izo haki za wazitakazo.

Kama wanashindwa kuwaambia ukweli wazungu basi wafunge mabakuli yao mana hayana maana yoyote kwetu zaidi ya kumpigia mbuzi gitaa
Hao hao mnaosema wafunge mabakuli yao, ndiyo hao hao ambao mnatembeza MABAKULI yenu kuomba misaada!
 
Serikari ya Rais John Magufuli, imeshauriwa kubadili mwelekeo wake, ikiwa ina dhamira ya kweli katika kuimarisha uhuru na demokrasia nchini.

Pia, serikali imetakiwa kuimarisha ulinzi wa haki za binadamu, sambamba na kuacha kutumia sheria kandamizi dhidi ya haki za binadamu.

Ripoti ya Shirika la Kimataifa la Kutetea haki za Binadamu la Amnesty, iliyotolewa leo tarehe 28 Oktoba 2019, imeeleza udhaifu katika kusimamia demokrasia na uhuru wa kujieleza nchini.

“Amnesty inaitaka Serikali ya Tanzania kuacha kutumia sheria kandamizi, kukiuka haki za binadamu. Haki ya uhuru wa kujieleza, kupokea na kutoa taarifa, haki ya kukusanyika na mikutano ya amani,” imeeleza ripoti hiyo.

Shirika hilo Limeitaka serikali kuwaacha huru bila masharti, washtakiwa wa kisiasa, wanaharakati na wanahabari.

Waliotajwa kwenye ripoti hiyo ni Zitto Kabwe, Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo; Freema Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema); Dk Vincent Mashinji, Katibu Mkuu Chadema; Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Chadema Bara.

Wengine ni Peter Msigwa, Iringa Mjini; Esther Matiko, Tarime Mjini; Halima Mdee, Kawe; John Heche, Tarime Vijijini; Ester Bulaya, Bunda Mjini pamoja na wanahabari Erick Kabendera na Maxence Melo.

Shirika hilo limemshauri Rais Magufuli kuhakikisha mamlaka zilizoko chini yake, zinawapa uhuru watetezi wa haki za binadamu, wanasiasa, wanahabari na makundi mengine, kutumia haki zao za msingi, ikiwemo uhuru wa kujieleza, uhuru wa kukusanyika pasina hofu.

“Rais ahakikishe mamlaka zinaruhusu kila mmoja, ikiwemo wanasiasa wa upinzani, wanahabari, watafiti, watetezi wa haki za binadamu, kutumia haki zao, ikwiemo haki ya uhuru wa kujieleza, uhuru wa kukusanyika.

“Kuhakikisha mamlaka zinaondoa zuio la mikutano ya vyama vya siasa, na kuwapata uhuru kila mmoja kufurahia haki yake, kukusanyika na kufanya mikutano ya amani.”

Amnesty imeitaka Serikali ya Tanzania kuimarisha haki za binadamu kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa 2020.

“Tunatoa wito, kurekebisha Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Takwimu, Sheria ya Uhalifu wa Mtandao, Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari na Mashirika yasiyo ya kiserikali NGO,” imependekeza ripoti hiyo.

Wakati huo huo, Amnesty imetoa wito kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuondoa sheria zinazokinzana na misingi ya haki za binadamu.

“Mapendekezo kwa Bunge, kuondoa sheria zote zinazokandamiza haki binadamu kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu wa 2020.

“Wito kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha vyombo vya habari vinafanya kazi zake kwa uhuru na kufurahia uhuru wa kujieleza na kufanya kazi zao pasipo hofu,” imependekeza Amnesty.

-Mw
Washitakiwa-wa-kisiasa-620x309.jpeg
 
Back
Top Bottom