Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, ambaye pia ni Mfadhili wa zamani wa Bendi ya FM ACADEMIA, Pedeshee Amos Makalla mkazi wa Mvomero, Morogoro, ametamka hadharani kwamba tangu enzi na enzi CCM haijawahi kuiba kura, Kama haitoshi amemshutumu Tundu Lissu kwamba aache kutisha na kupotosha Wananchi
Habari kamili hii hapa
---
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amesema chama hicho hakijawahi kuwaza wala kufikiria kuiba kura wakati wa uchaguzi.
Makalla amemuonya Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, Tundu Lissu kuacha kuwatisha Watanzania kwa lugha za kichochezi.
Mwenezi huyo amesema hayo leo Jumanne, Juni 4, 2024 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Bomang'ombe, Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro.
Makalla yupo katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi ya kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi na kuangazia maandalizi ya uchaguzi ujao wa serikali za mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.
Ukiwa kama Mtanzania unayeona Chaguzi za Nchi hii pamoja na ule 2015 na ile ofisi ya Masaki iliyokuwa chini ya Mzee Kinana, na ule wa 2020 ambao ulisimamiwa na Dkt Mahera na Dar es Salaam ikiwa na RPC aliyeitwa Lazaro Mambosasa, TOA MAONI YAKO