SERIKALI YARUHUSU WAFANYABIASHARA KUREJEA KARUME KWA MPANGO MZURI.
- Umati walipuka kumpongeza
Rais Samia Suluhu Hassan.
-
RC Makalla apokea taarifa ya ripoti ya Kamati iliyoundwa kuchunguza Chanzo Cha Moto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan ameruhusu Wafanyabiashara wa
Soko la Karume kurejea na kuendelea na Biashara kwa kuwekewa
Mpango mzuri ambapo Wafanyabiashara wa Soko hilo
wamepongeza uamuzi huo na kuishukuru Serikali.
Akizungumza wakati wa
mkutano wa hadhara na Wafanyabiashara hao Mara Baada ya kupokea
Taarifa ya ripoti iliyoundwa kuchunguza chanzo Cha Moto, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Mhe. Amos Makalla amesema
Rais Samia ameelekeza pia uwepo
utaratibu mzuri wa kuzuia Moto, kuhakikisha hakuna atakaedhulumiwa eneo lake na kutoa ruhusa kwa Wafanyabiashara kujenga Vibanda kwa gharama zao.
Kuhusu Ripoti ya chanzo Cha Moto,
RC Makalla amesema Kamati imebaini Moto huo ulitokana na
Mshumaa uliowashwa kwenye kibanda walichokuwa wanajihifadhi watumiaji wa dawa za kulevya "Mateja".
Aidha
RC Makalla amesema Baada ya kupokea
ripoti hiyo ataikabidhi kwenye Mamlaka za juu kwaajili ya utekelezaji wa maoni na Mapendekezo yote ya Kamati.
Miongoni mwa
Maoni na Mapendekezo ya Kamati hiyo Ni pamoja
Ujenzi wa Soko jipya linaloendana na Hali ya Sasa na
vizimba kutolewa kwa kipaombele kwa wazawa, uwepo wa
mfumo mzuri wa kuzuia Moto, Barabara za kuingia na kutoka, Ujenzi wa Majengo ya Muda mfupi,
Kila mfanyabiashara kuwa na bima.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo
Eng. Justin Lukaza amesema hasara iliyotokana na Kuungua Hilo ni zaidi ya Shilingi
Bilioni 7.2 ambapo idadi ya
Wafanyabiashara waliokumbwa na janga Hilo Ni 3,090.
Pia soma:
-
Shuhuda: Chanzo cha moto soko la Karume ni mateja, waliangusha mshumaa wakati wanatengeneza mihadarati (18/01/2022)
View attachment 2094094