Kasiano Muyenzi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,858
- 22,729
Hao mateja wametiwa mbaroni?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
SERIKALI YARUHUSU WAFANYABIASHARA KUREJEA KARUME KWA MPANGO MZURI.
- Umati walipuka kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan.
- RC Makalla apokea taarifa ya ripoti ya Kamati iliyoundwa kuchunguza Chanzo Cha Moto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameruhusu Wafanyabiashara wa Soko la Karume kurejea na kuendelea na Biashara kwa kuwekewa Mpango mzuri ambapo Wafanyabiashara wa Soko hilo wamepongeza uamuzi huo na kuishukuru Serikali.
Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara na Wafanyabiashara hao Mara Baada ya kupokea Taarifa ya ripoti iliyoundwa kuchunguza chanzo Cha Moto, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Rais Samia ameelekeza pia uwepo utaratibu mzuri wa kuzuia Moto, kuhakikisha hakuna atakaedhulumiwa eneo lake na kutoa ruhusa kwa Wafanyabiashara kujenga Vibanda kwa gharama zao.
Kuhusu Ripoti ya chanzo Cha Moto, RC Makalla amesema Kamati imebaini Moto huo ulitokana na Mshumaa uliowashwa kwenye kibanda walichokuwa wanajihifadhi watumiaji wa dawa za kulevya "Mateja".
Aidha RC Makalla amesema Baada ya kupokea ripoti hiyo ataikabidhi kwenye Mamlaka za juu kwaajili ya utekelezaji wa maoni na Mapendekezo yote ya Kamati.
Miongoni mwa Maoni na Mapendekezo ya Kamati hiyo Ni pamoja Ujenzi wa Soko jipya linaloendana na Hali ya Sasa na vizimba kutolewa kwa kipaombele kwa wazawa, uwepo wa mfumo mzuri wa kuzuia Moto, Barabara za kuingia na kutoka, Ujenzi wa Majengo ya Muda mfupi, Kila mfanyabiashara kuwa na bima.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Eng. Justin Lukaza amesema hasara iliyotokana na Kuungua Hilo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 7.2 ambapo idadi ya Wafanyabiashara waliokumbwa na janga Hilo Ni 3,090.
Pia soma:
- Shuhuda: Chanzo cha moto soko la Karume ni mateja, waliangusha mshumaa wakati wanatengeneza mihadarati (18/01/2022)
View attachment 2094094
Wamerudishwa? Soma vizuri statement yao, wanasema panajengwa soko la kisasa lenye hadhiMuhimu machinga wamerudishwa, nyingine zote porojo.
Wewe kama chanzo unakijua si ukiseme? Ilimradi uwe ndio ukweli na can be proved.Mmmmmmmh!Hii ngumu kumeza!
Mimi nimetilia mashaka tu hizo findings!Wewe kama chanzo unakijua si ukiseme? Ilimradi uwe ndio ukweli na can be proved.
Mwambieni Makala atusomee report nzima.
Kilichomo ni mhimu sana kukijua
Pure politics. Huko shuleni sijui watu walienda kusomea ujinga 😳 😳SERIKALI YARUHUSU WAFANYABIASHARA KUREJEA KARUME KWA MPANGO MZURI.
- Umati walipuka kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan.
- RC Makalla apokea taarifa ya ripoti ya Kamati iliyoundwa kuchunguza Chanzo Cha Moto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameruhusu Wafanyabiashara wa Soko la Karume kurejea na kuendelea na Biashara kwa kuwekewa Mpango mzuri ambapo Wafanyabiashara wa Soko hilo wamepongeza uamuzi huo na kuishukuru Serikali.
Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara na Wafanyabiashara hao Mara Baada ya kupokea Taarifa ya ripoti iliyoundwa kuchunguza chanzo Cha Moto, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Rais Samia ameelekeza pia uwepo utaratibu mzuri wa kuzuia Moto, kuhakikisha hakuna atakaedhulumiwa eneo lake na kutoa ruhusa kwa Wafanyabiashara kujenga Vibanda kwa gharama zao.
Kuhusu Ripoti ya chanzo Cha Moto, RC Makalla amesema Kamati imebaini Moto huo ulitokana na Mshumaa uliowashwa kwenye kibanda walichokuwa wanajihifadhi watumiaji wa dawa za kulevya "Mateja".
Aidha RC Makalla amesema Baada ya kupokea ripoti hiyo ataikabidhi kwenye Mamlaka za juu kwaajili ya utekelezaji wa maoni na Mapendekezo yote ya Kamati.
Miongoni mwa Maoni na Mapendekezo ya Kamati hiyo Ni pamoja Ujenzi wa Soko jipya linaloendana na Hali ya Sasa na vizimba kutolewa kwa kipaombele kwa wazawa, uwepo wa mfumo mzuri wa kuzuia Moto, Barabara za kuingia na kutoka, Ujenzi wa Majengo ya Muda mfupi, Kila mfanyabiashara kuwa na bima.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Eng. Justin Lukaza amesema hasara iliyotokana na Kuungua Hilo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 7.2 ambapo idadi ya Wafanyabiashara waliokumbwa na janga Hilo Ni 3,090.
Pia soma:
- Shuhuda: Chanzo cha moto soko la Karume ni mateja, waliangusha mshumaa wakati wanatengeneza mihadarati (18/01/2022)
View attachment 2094094
Na mateja yamesingiziwa kwa kuwa hayana uwezo wa kujitetea kitaalamuMshumaa Hapo Umetumika Kama Bangusiro (Kondoo Wa Kafara)
KabisaNa mateja yamesingiziwa kwa kuwa hayana uwezo wa kujitetea kitaalamu
A research is challenged with a research braza!Mimi nimetilia mashaka tu hizo findings!
Hiyo siyo research mkuu,umechanganya madesa!A research is challenged with a research braza!