TANZIA Amri Athuman (King Majuto) afariki dunia akiwa hospitali ya Taifa Muhimbili

TANZIA Amri Athuman (King Majuto) afariki dunia akiwa hospitali ya Taifa Muhimbili

TANZIA: Msanii wa vichekesho Mzee King Majuto amefariki dunia usiku wa leo Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu.

Msemaji wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema Mzee Majuto alipelekwa hospitalini hapo Julai 31 baada ya hali yake kubadilika.

“Hali yake ilibadilika majira ya saa tisa alasiri ya leo hivyo kuhamishwa kutoka jengo la Sewahaji kwenda ICU. Ilipofika saa 1.30 jioni hii hali yake ilibadilika zaidi na madaktari walijitahidi kuokoa maisha yale bila mafanikio. Ilipofika saa 2 usiku alikata roho,''
View attachment 830443
View attachment 830484
View attachment 830455
Rais Magufuli na Mama Janeth Magufuli waliopokwenda kumjulia hali King Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.

Pia soma >
Mzee Majuto: Tanzanian Movie and Comedy Legend
Mzee Majuto atangaza rasmi kuacha kuigiza, sasa kumrudia Mungu wake
Mwakyembe Kuivaa kampuni iliyomdhurumu Mil 25 Mzee Majuto.
Haya ndio maisha halisi anayoishi mzee Majuto
--
Wasifu
Amri Athuman’ King Majuto’ alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini, Tanga, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 9 akiigiza katika majukwaa Mzee Majuto maarufu kama King Majuto ni mtunzi, muigizaji,mwandishi wa mswada.

Na ndiye muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC) Kwa sasa King Majuto ni mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali.
 
mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu mzee wetu kipenzi na gwiji wa comedian Tanzania
 
Mungu awatie nguvu wafiwa wote.Awape faraja katika kipindi hiki kigumu
 
Wakuu bila shaka na nyinyi ni mashahidi tosha kwamba bwana yule au ukipenda muite Jiwe huwa haudhurii kabisa misiba yoyote ile yupo radhi akafungue hata tawi la benki au jambo lolote lile ambalo halina tija kwa wakati huo lakini si kuhudhuria misiba mpaka ikafika mahala watu wakaanza kumuhisi huenda ni mshirikina.

Lakini kwa maajabu kabisa bila kutarajia tumemuona jiwe akihudhuria msiba wa Amri Athumani Majuto kitu ambacho baadhi ya watu wameingiwa na mashaka kwamba huenda kuna kitu kimejificha maana si hali ya kawaida.

Tusubiri baada ya maziko kuna mambo makubwa yataibuka kama kipindi kile cha msiba wa Masaburi yalivyoibuliwa mambo yasiyojulikana hata na wana familia ila jiwe aliyaropoka jambo ambalo halikuwafurahisha wanafamilia.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Duh! Wanadamu kazi kweli-kweli, kwani mia unaanza kuhesabu toka wapi? Kwa hili hapana hapana
 
Wakuu bila shaka na nyinyi ni mashahidi tosha kwamba bwana yule au ukipenda muite Jiwe huwa haudhurii kabisa misiba yoyote ile yupo radhi akafungue hata tawi la benki au jambo lolote lile ambalo halina tija kwa wakati huo lakini si kuhudhuria misiba mpaka ikafika mahala watu wakaanza kumuhisi huenda ni mshirikina.

Lakini kwa maajabu kabisa bila kutarajia tumemuona jiwe akihudhuria msiba wa Amri Athumani Majuto kitu ambacho baadhi ya watu wameingiwa na mashaka kwamba huenda kuna kitu kimejificha maana si hali ya kawaida.

Tusubiri baada ya maziko kuna mambo makubwa yataibuka kama kipindi kile cha msiba wa Masaburi yalivyoibuliwa mambo yasiyojulikana hata na wana familia ila jiwe aliyaropoka jambo ambalo halikuwafurahisha wanafamilia.
Mbwa ni mbwa tu inaonesha ww tena ni jibwa kubwa hasaaa usie na fadhila Sasa kiongozi kwenda ktk msiba ni kosa gani??
 
Waislam huwa "hawamuangalii" marehemu wanapotoa heshima za mwisho.
 
Back
Top Bottom