Amri Kiemba: Hakukuwa na sababu ya msingi iliyopelekea kuahirishwa kwa derby ya tarehe 8 March

Frank Wanjiru

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,686
Reaction score
46,842
AMRI KIEMBA

"Ukitumia kanuni kwenye sehemu ambayo ulitumia busara ndicho ambacho kinawachanganya Bodi ya Ligi hivi sasa Mimi nadhani Yanga wapo tayari kucheza na kumalizia Ligi kwa mechi zote 30 kama tu yale yote ambayo wanahisi haikuwa haki yatapatiwa ufumbuzi

Kunawezekana kuna mengine yanaweza kuwa sio ya kupatiwa ufumbuzi kwa msimu labda ni kwa misimu inayokuja lakini yale wanayoweza kuyapatia ufumbuzi na kuyatolea ufafanuzi wanaweza kuyajibu na yale yanayohitaji muda mrefu wanaweza kuyaweka kwenye Panel yakashughulikiwa

Lengo la Yanga sidhani kama ni kukomoa ni kujaribu kutengeneza mifumo ambayo itakuwa imara isiwe kila mtu akila akiamka anasema mechi hakuna Yani kuwe na utaratibu ambao kila mtu atauheshimu na kuufata

Mfano kuhairishwa kwa mchezo nguvu ambayo imetumika kupanga ratiba ya tarehe 15 Juni kama wangeitumia June 8 Leo tulikuwa hatuzungumzi kwa sababu ingekuwa mchezo ule ulishaisha kwa maana ya kuchezwa au haukuchezwa ila ulishaisha kwa kufata taratibu na kanuni ambazo wanasema wanazitumia sasa hivi

Mimi nadhani hakukuwa na haja ya kutunishiana misuli ilihitajika busara ili kuweza kuendelea jambo lililoanza kwa busara kulimaliza kwa busara, nasema kwa Busara kwa sababu mpaka saa nne Mapka saa nne anahojiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi anasema mechi ipo maandalizi yaendelee kwahiyo unaona kwa kiasi gani baadae zilikuja busara sio tena zile kanuni na taratibu ambazo wanadai wanazisimamia".

Maneno ya mchambuzi na mchezaji wa zamani Amri Kiemba kuhusu Mgogoro unaoendelea wa Kariakoo Dabi.
 
Watu wote wenye akili timamu wanajua hakukua na sababu ya ku ghairisha mchezo zaidi ya kuinusuru Moja ya timu na kipigo kizito.
Tff/ Bodi walikuja na sababu za usalama na Rushwa, Jana imefahamika wazi Kuna kigogo alipiga Simu ili Simba wasifanye mazoezi
Ripoti ya uchunguzi ipo, Tff/Bodi wanaizuia kwakua jina la kigogo litaweka wazi.
Inamaana Malumbano yote aya yanaendelea ili Kigogo asi anikwe hadharani.
Tff/Bodi hawakuwai kuomba radhi kwa hasara na vifo vilivyo tokea march 8.
Mpaka Leo hawataki kuelezea umma Ripoti wanayo ikalia.
Hii ni zaidi ya Kiburi na dharau kwenye taasisi ya umma.
Ni zaidi ya mambo ya kiswahili.
 
Eti watu wote timamu
 
KAMA JAMBO LINAHUSU WEWE NA MKEO AU MUMEO KWELI SIO LAZMA MTU AONE SABABU YA NYINYI KUACHANA ILA SIO KWENYE HILI LA TAREHE 8,HILI NI JAMBO LINALOHUSU UMMA MZEE
Kwani umma ni lazima Amri Kiemba aelewe?

Ikiwa ripoti ya CAG kuhusu matumizi holela ya fedha inatolewa kwa UMMA lakini wa Adzabe wameshindwa kuielewa je hiyo itafanya ripoti hiyo ionekane ya uongo kwasababu kuna wa Adzabe hawajaelewa?
 
watu waelewe wasielewe weka vitu kwenye utaratibu ili kuepusha haya yanayoendelea,kwani wachache tu wanaoelewa wanaweza kulifanya jambo kuwa gumu kama ilivyo sasa,ni hao watu wachache tu wakiamua mambo yanakuwa magumu kama ilivyo sasa
 
Moja ya utaratibu ni timu pinzani kufanya mazoezi.

Huo utaratibu mliufuata?
 
Amri Kiemba sio lazima hadi yeye aone na kuielewa sababu ndio ionekane ni sababu.
Amri kiemba ni professional kaongea ukweli najua ulitegemea awaponde Yanga ndo maana mimi naamini wachambuzi wa mpira wawe wamecheza mpira sababu wanajua uhalisia wa mpira wa watanzania

Lilikuwa ni kosa kuhairisha mechi tarehe 8 sababu hakukua na sababu za msingi
 
Moja ya utaratibu ni timu pinzani kufanya mazoezi.

Huo utaratibu mliufuata?
ila utaratibu hauruhusu kugomea au kuaghirisha mechi kisa hujafanya mazoezi siku moja kabla ya mechi...naweza kubeti na wewe hata milioni kwa jiwe kwamba kamwe hautakuja kusikikia bodi ya ligi wanakuja na sababu ya namna hiyo kwenye swala la kuaghirisha mechi
 
Pamba vs simba siku moja kabla ya mechi simba walifanyiwa vurugu kabla ya mechi na mkuu wa mkoa wa mwanza kuna baadhi ya viongozi wa Simba waliwekwa ndani na mkuu wa mkoa ilikuwa chaos

Ila cha ajabu ile mechi simba hawakugomea walicheza despite ya kufanyiwa zengwe na vurugu swali kwanini ugomee mechi ya Yanga ambayo hakuna ushahidi wa vurugu ila uliyofanyiwa vurugu ulicheza
 
Amri kiemba ni professional kaongea ukweli najua ulitegemea awaponde Yanga ndo maana mimi naamini wachambuzi wa mpira wawe wamecheza mpira sababu wanajua uhalisia wa mpira wa watanzania

Lilikuwa ni kosa kuhairisha mechi tarehe 8 sababu hakukua na sababu za msingi
Kucheza mpira sio tiketi ya kujua sheria.

Kuishi karibu na mahakama sio kujua sheria

Wewe kabla ya leo uliweza kuamini kuwa kuna CEO wa timu kubwa hajui kiasi cha pesa anachopata mshindi wa CRDB?
 
Umeanza kuleta siasa uzi unahusu kuhairisha mechi wewe unarukia kwenye mambo ya mshindi wa CRDB jikite kwenye uzi
 
ila utaratibu hauruhusu kugomea au kuaghirisha mechi kisa hujafanya mazoezi siku moja kabla ya mechi...naweza kubeti na wewe hata milioni kwa jiwe kwamba kamwe hautakuja kusikikia bodi ya ligi wanakuja na sababu ya namna hiyo kwenye swala la kuaghirisha mechi
Ila hiyo sio sababu iliyotajwa ya mechi kuahirishwa.

Hapa ndipo napoona Amri Kiemba amewachota.
 
Back
Top Bottom