Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 53,537
- 133,017
Sio fadhila.Kwahiyo kwa upande wako kosa la Yanga ni kutorudisha fadhila??
Wao wanafanyiwa favour ila ikija zamu yao wanasigina??
Basi kwa hili ni muda sasa wa bodi ya ligi kuanza kutumia kanuni ipasavyo na sio busara.
Hizo busara zao zinafanya wanatikiswa daily.
Yani ni kuishi kwenye ile definition ya "kabla ya kuona kibanzi kilicho kwenye jicho la mwingine, kwanza utoe boriti iliyoko kwenye jicho lako".
Pale unapopinga busara kutumika katika maeneo ambayo hayaendi kukufaidisha wewe na ku demand sheria itumike ilihali wewe mwenyewe una mambo kibao umekingiwa kifua kupitia hizo hizo busara.
Ni sawa na malalamiko ya Yanga waliyoyatoa kwenda bodi ya ligi yenye kurasa 170 kuhusu marefa wanaoonekana kuzibeba baadhi ya timu kwenye maamuzi ya viwanjani.
Halafu kwenye hiyo list hakuna sehemu yeyote ambayo Yanga imetaja matukio ya wao kunufaika na makosa hayo ya waamuzi.
Huo unakuwa ni unafiki.