Amri Kiemba: Hakukuwa na sababu ya msingi iliyopelekea kuahirishwa kwa derby ya tarehe 8 March

Amri Kiemba: Hakukuwa na sababu ya msingi iliyopelekea kuahirishwa kwa derby ya tarehe 8 March

Ndiyo maana nimekwambia masuala haya ya mpira hauyajui. Nimewahi kupitia makala zako nikagundua hilo. Kama uko serious na siasa, tafuta mshauri wa masuala haya akuelekeze kabla haujatia maoni au sera zako. Ni ushauri tu lakini una uhuru wa kuukataa.
Timu yako juzi jumatatu ilisema inasubiri report ya hukumu ya kilichotokea tarehe 7 kwa lugha nyingine hawana majibu bado ila wewe tayari una majibu swali umepata wapi majibu ilihali officially results haijatoka
 
Sijui kama kuna la kujadili hapo. Derby ipo 15/06 na Simba imesema itaenda kucheza mchezo huo. Simba imesema inasubiri na inataka ripoti itolewe ila siyo kama takwa la kucheza mchezo katika tarehe iliyopangwa.
 
Makomandoo wa Yanga sio sehemu ya kizuizi?

Hawa ni mara ngapi tunawaona wakiwa wameambatana na viongozi wa Yanga kwenye matukio mengi?

Hata ripoti ya TFF iliwatambua. Kwamba unataka tukubaliane huyo kiongozi hawa ni watu wake?
View attachment 3364800
Tff waseme sasa maana afisa habari wa Yanga kasema kutoka kwenye report ya Yanga kutoka kwenye kikao ni kigogo wa serikali hao makomandoo si atawewe unaweza kuwa komandoo wa Azam au Simba hawakati hawakujui
 
Kama hata hujui nukuu nimetoa wapi je hizo allegations ambazo unanihusisha nazo kwamba nimezitoa unaweza kunipa post namba zake ambazo nimeweka yale madai yanayosema " timu isipofanya mazoezi igomee mechi"
Wewe ndio useme umetoa wapi, Hizi allegations ni references ya comment yako au ww tena kazi yako sio kunukuu.
 
Ligi za kitoto zinaletwa na timu yako.

Unaanzaje kuidai TFF pesa ambayo haikuwa stahiki yako?
Yaani hela ya Ubingwa sio stahiki ya Yanga,kweli wewe zwazwa unaependa mabishano kama wakina mwajuma ndala ndefu.
 
Sijui kama kuna la kujadili hapo. Derby ipo 15/06 na Simba imesema itaenda kucheza mchezo huo. Simba imesema inasubiri na inataka ripoti itolewe ila siyo kama takwa la kucheza mchezo katika tarehe iliyopangwa.
Usikwepe swali jibu iweje wewe unamajibu ya march 7 ilihali timu yako haina Inasubiria report mpaka sahivi
 
Tff waseme sasa maana afisa habari wa Yanga kasema kutoka kwenye report ya Yanga kutoka kwenye kikao ni kigogo wa serikali hao makomandoo si atawewe unaweza kuwa komandoo wa Azam au Simba hawakati hawakujui
Makomandoo wa Yanga hawapo rasmi lakini ni ngumu kuwatenganisha na Yanga kusema hawahusiani na Yanga wakati events kibao tunaona wameambatana na viongozi wa Club.

Huyo Afisa Habari wa Yanga alimtaja kwa majina huyo kiongozi ni nani?

Isijekuwa mzigo wa punda ulikiwa unainekana ni mwepesi tu kwasababu umebebwa na Punda lakini alivyobeba mtu akaona ni unyanyasaji.

Sasa sijajua kwanini Afisa Habari wa Yanga alirudia makosa kwa kutomtaja.

Ugumu aliouona Afisa wa bodi ya ligi ndio ugumu ule ule ambao hata yeye Afisa Habari wenu aliuona na kushindwa kumtaja public wote tumjue ni nani.
 
Kwa hiyo Jemedari ndio anatakiwa aone na kuielewa sababu ndio ionekane sababu?
Jemedari ndio nani?

Mi nazungumzia taarifa rasmi iliyotolewa na bodi ya ligi kupitia nukuu zake.

Hayo ya Jemedari yamekujaje?
 
Isipofanya hakuna kanuni na adhabu zake?
Unafanya kosa kwa kujua adhabu iliyoandikwa kwenye sheria haiwezi kukudhuru?

Halafu kama unapenda consequences za adhabu ni lini mliwahi kulalamika kwa kutoadhibiwa kwa kosa la kutosajili timu ya vijana?

Hamjui kuwa consequences zake ni pamoja na kutoshiriki ligi kuu?
 
Wewe ndio useme umetoa wapi, Hizi allegations ni references ya comment yako au ww tena kazi yako sio kunukuu.
Nioneshe hizo comments nilizoandika hivyo

Nataka nipime level yako ya kujua kusoma.
 
Yaani hela ya Ubingwa sio stahiki ya Yanga,kweli wewe zwazwa unaependa mabishano kama wakina mwajuma ndala ndefu.
Ubingwa wa mwaka gani wa kombe la shirikisho ambalo prize yake ni milioni 200 kwa bingwa?
 
Sipendi watu wanaojifanya Kutumia Busara sehemu ya kufata Kanuni.

Simba alikua na Sababu zake kukataa kucheza Tare 8, Na alikua sahihi kwa upande wake, Yanga walikua sahihi kwa upande wao kuleta timu Uwanjani ila TFF ndo alikua wrong kuhairisha mechi mda mchache kabla ya Tukio.

Hivyo mpaka sasa Yanga wanacho dai wako sahihi
 
AMRI KIEMBA

"Ukitumia kanuni kwenye sehemu ambayo ulitumia busara ndicho ambacho kinawachanganya Bodi ya Ligi hivi sasa Mimi nadhani Yanga wapo tayari kucheza na kumalizia Ligi kwa mechi zote 30 kama tu yale yote ambayo wanahisi haikuwa haki yatapatiwa ufumbuzi

Kunawezekana kuna mengine yanaweza kuwa sio ya kupatiwa ufumbuzi kwa msimu labda ni kwa misimu inayokuja lakini yale wanayoweza kuyapatia ufumbuzi na kuyatolea ufafanuzi wanaweza kuyajibu na yale yanayohitaji muda mrefu wanaweza kuyaweka kwenye Panel yakashughulikiwa

Lengo la Yanga sidhani kama ni kukomoa ni kujaribu kutengeneza mifumo ambayo itakuwa imara isiwe kila mtu akila akiamka anasema mechi hakuna Yani kuwe na utaratibu ambao kila mtu atauheshimu na kuufata

Mfano kuhairishwa kwa mchezo nguvu ambayo imetumika kupanga ratiba ya tarehe 15 Juni kama wangeitumia June 8 Leo tulikuwa hatuzungumzi kwa sababu ingekuwa mchezo ule ulishaisha kwa maana ya kuchezwa au haukuchezwa ila ulishaisha kwa kufata taratibu na kanuni ambazo wanasema wanazitumia sasa hivi

Mimi nadhani hakukuwa na haja ya kutunishiana misuli ilihitajika busara ili kuweza kuendelea jambo lililoanza kwa busara kulimaliza kwa busara, nasema kwa Busara kwa sababu mpaka saa nne Mapka saa nne anahojiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi anasema mechi ipo maandalizi yaendelee kwahiyo unaona kwa kiasi gani baadae zilikuja busara sio tena zile kanuni na taratibu ambazo wanadai wanazisimamia".

Maneno ya mchambuzi na mchezaji wa zamani Amri Kiemba kuhusu Mgogoro unaoendelea wa Kariakoo Dabi.
Amri Kiemba kigeugeu.
 
Amri Kiemba sio lazima hadi yeye aone na kuielewa sababu ndio ionekane ni sababu.
Madondocha wa mudi mnahisi kila jambo linahitaji ushabiki takataka nyie
 
Sipendi watu wanaojifanya Kutumia Busara sehemu ya kufata Kanuni.

Simba alikua na Sababu zake kukataa kucheza Tare 8, Na alikua sahihi kwa upande wake, Yanga walikua sahihi kwa upande wao kuleta timu Uwanjani ila TFF ndo alikua wrong kuhairisha mechi mda mchache kabla ya Tukio.

Hivyo mpaka sasa Yanga wanacho dai wako sahihi
Unajua haya mambo ukiyatazama kwa jicho la sheria ni msaafu hivyo ifuatwe kama ilivyoagizwa unaweza kuwaona TFF wanakosea.

Lakini tukianza kuchambua baadhi ya favors ambazo hizi Clubs zimekuwa zikifaidika na TFF ndio utajua no body respect law.

Ishu ya Kambole unaikumbuka? Yanga walikuwa na wachezaji 13 wa kigeni idadi ambayo ndio ukomo.

Lakini wakati dirisha dogo linakaribia kufungwa walikuwa na mpango wa kumsajili Tuisila Kisinda.

Yanga wakawa na mpango wa kumtoa kwa mkopo Kambole ili wamsajili Kisinda. Mchakato huo haukufanikiwa kwa wakati na hivyo wakatoa statement ya uongo kuwa wamempeleka kwa mkopo timu ya Uganda.

TFF ilifahamu kila kitu na kuamua kuwalinda ili tu wafanikishe adhma yao.

Kambole akawa anashinda kwenye kambi yao kule Avic Town na hata humu kuna uzi ukiwahi kuketwa kujadili uongo huo.

Kambole alikuja kuonekana tena kwenye mashindano ya Zanzibar akiwa kama mchezaji wa Yanga.

Huko kote ni busara tu zilitumika.

Na kabla ya huu msimu kuanza pia Yanga ilikuwa haijakamilisha usajili wa wachezaji wa timu ya vijana na hivyo kwa sheria ya TFF hawakupaswa kushiriki ligi kuu.

Lakini busara ikatumika na Yanga leo hii ndio anaongoza ligi.

Kwa hiyo hicho unachokisema ni busara na hakipaswi kutumika. Ukasema utumie kanuni sikufichi hakuna timu itayoweza ku survive.

Kuna mambo mengi mengine yapo nyuma ya pazia TFF inazikingia kifua hizi timu kwenye maswala mengi mno.
 
Ubingwa wa mwaka gani wa kombe la shirikisho ambalo prize yake ni milioni 200 kwa bingwa?
Kumbe mnashadadia vitu msivyovijua,nenda katafute video au audio ya Mkurugenzi wa CRDB ndugu Nsekela wakati wanatoa hizo 255ml matumizi yake yalikuwa ni yapi.
 
Back
Top Bottom