Amri Kiemba wewe ni superstar hutakiwi kuishi Kigogo

Hao wamezaliwa huko kina Kihwelo na njohole family,miaka ya 60 nafahamu,
Mji ulikuwa mdogo sasa mji umekuwa,miaka hiyo Tabata ilikuwa na simba na swala ila kwa saaa jiji limetanuka hakuna haja ya kuishi kigogo
Jamhuri hadi anamaliza mpira wake alikuwa Kigogo, alihamia Kimara akiwa kocha, tena baada ya Mwigizaji Rose Ndauka kutikisa nyumbani kwake.

Ni kama aliamua kumweka mbali Mama Super na Rose Ndauka kwani wote ni wakazi wa huko Kigogo. Hiyo ni kabla ya Rose kusonga mbele.

Ova
 
hakuna mtu makini anaish nchi ya ulimwengu wa 3............kumbuka the whole africa continent contributes to about 1.7% of the global scientific knowledge ............... binadamu hatulingani huwez mpangia mtu pa kuishi et kisa staa mtu n mtu tuu watu wote wanathaman na hadhi sawa...........krb buza mkuu🤣😂
 
Unasema kweli aise kunasiku natoka mabibo sokoni nilimuona kiemba nadhani alitoka manzese tulikuwa nae kwenye daladala moja alipofika kigogo mwisho alishuka.
Da nilishangaa mtu maarufu kupanda daladala.
 
Nyie ndio mnafanya mastaa wakifulia wanajinyonga sasa mbagala kule anapoishi juma nature ni balaa kuna vibaka halafu kuuliwa nje
Ile baa namkutaga juma nature anqkunywa bia da nikamq ka grosary na mmiliki ni mchaga mmoja sijui mgonjwa yule maana tumbo halina ushirikiano na mwili.kuna biashara niliwahi fanya na juma nature alikuwa na rafiki yake bonge hivi ananywele nyingi
 
Tuoneshe nyumba anayoishi ili tucoment vizuri
 
Ile baa namkutaga juma nature anqkunywa bia da nikamq ka grosary na mmiliki ni mchaga mmoja sijui mgonjwa yule maana tumbo halina ushirikiano na mwili.kuna biashara niliwahi fanya na juma nature alikuwa na rafiki yake bonge hivi ananywele nyingi
Kule ni uswahilini haswa kila siku matukio na wamempa mtaa kabisa.
 
Acha kufuatilia maisha ya watu
 
Wanamichezo wafundishwe sana mambo ya fedha ili kuondoa aibu ndogondogo wakistaafu. Hilo group la kina Amri Kiemba, Amir Maftah na wengine wa enzi zao haliko sawa sana. Kusema kuwa anaishi maisha simple ni kutumia tu tafsida ila ukweli ni kwamba hayo ni maisha ya kimaskini. KUPANDA DALADALA KWA DSM NI UMASKINI. Tena likiwa daladala la Mbagala au Gongo la mboto ni umaskini promax.
 
Kweli asee Amir maftah tulisoma Wote Moshi Tech ila alitoboa alipokuwa Mtibwa then yanga....
Now yupo choka namuona sana kwenye daladala.
 
Unataka kutuaminisha wanaofilisika wote ni kwasababu walikosa elimu ya fedha? Sometimes mambo yanakugomea tu yanaanza kubuma bila kupenda.
 
Unataka kutuaminisha wanaofilisika wote ni kwasababu walikosa elimu ya fedha? Sometimes mambo yanakugomea tu yanaanza kubuma bila kupenda.
Endelea kukaza fuvu. Wanamichezo wengi wakishastaafu wanatumbukia kwenye umaskini. Kule Arusha kuna wanariadha walikuwa kila siku wako kwenye ndege kushiriki mashindano ila baada ya kustaafu wamefilisika chap. Wachache waliokuwa na akili za kuwekeza ndo wako vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…