ICC inafanya kazi kama ofisi za waendesha mashtaka wa serikali sawa sawa na ofisi ya DPP kwa Tanzania.
Kesi zao wanazitafuta wenyewe na wanakushitaki wenyewe hakuna mwanasheria independent anaweza kwenda kufungulia nchi au mtu kesi ICC...
Ushabiki ni upofu.
Binafsi kabisa huwa narudia sipendi mtu aonewe wala kufanyiwa madhara ya Mwili au uhai kama yaliyompata TL.
Pia natamani fairnesss kwenye uchaguzi. Lakini hii haipo kama katiba iliyopo haijawa amended.
Naamini Upinzani wa Tz ni wa kinjaa njaa tu wanisamehe kwa maana kuwa kama walikubali kuingia uchaguzi na Katiba hii wakubali matokeo kwa mujibu wa katiba pia.
Hii ya kutafuta raia waingie mtaani kuwatafutia vyeo HAIPO. Pia hii ya kutafuta nchi za kigeni kukutafutia cheo lazima utalipa sio wajinga wakuweke madarakani halafu hakuna faida. Waulize Israel ilipokuwa inahamisha raia wake wa Kiethiopia ilikuwa tayari kula dili na serkali za Sudani na Ethiopia chini ya Mosaad.
Naelewa kuwa ukiacha ushabiki wa uccm na ucdm hakuna nchi iliyo na mamlaka kushinikiza nchi nyingine wala hizo law firms, hii barua sio ya kwanza hata hao Human right waliandika, Ubunge la dunia (whatever) waliandika.
Nijuacho ni kuwa jumuia za Mataifa yanayotaka benefit kupitia uasi na migogoro watatumia intelligency secret securities kuandaa waasi ndani ya nchi kuwa fainancy, kuwapa training , silaha na yanayofafanana.
Labda hilo ndio ajenda kuu.
Nadhani hatujachelewa kama raia wema kutoa taarifa sahihi hata kwa hizo system zetu ambazo zinaonekana kuwa ni ccm agents kwa wanaosema hivyo, bado naamini ktk Jwtz security system hawa sio wanasiasa kabisa. Hata hivyo ingekuwa mimi bora nisiwe madarakani huku nchi ikiingia kwenye vurugu. Sio uoga.
Ningekywa tayari hata ku step down. Sio Aibu.
Lakini ningekuwa mkali kulinda haki, kweli ,rasilimali, uhai na utaifa ya Tz hata kama lolote.
Mungu wabariki wagombea wetu wote.
Roho ya utaifa, pasipo kununuliwa iwe juu yao.