Nimeisoma hii barua mpaka mwisho...
Barua imeandikwa kiweledi haswa na imebeba amri na maelekezo....
Halafu inaeleza mambo ya ndani hasa kiasi cha mtu kujiuliza nani anawataarifu hawa kinachoendelea ktk corridor za usalama za Ikulu ya Magufuli?...
Ukisoma barua hii NENO kwa NENO utagundua kuwa, hawa watu wana dhamira ya kweli kwa njia zozote kumlinda mteja wao....
Na ni kama Amsterdam & Partners LLP ni waanzisha varangati tu, lakini watendaji halisi wako sehemu wala hawajapanua mdomo....
Kwa akina sisi, tumejua hata ambayo tulikuwa hatuyajui kwa kweli katika sakata hili....
Kumbe kesi yake ya "sedition - uchochezi" ya trh 26/8 imepangwa hiyo tarehe kwa makusudi kabisa na ndani yake kukiwa na nia ovu au "collusion" kati ya Ikulu (serikali), Mahakama na NEC...!!
Na kumbe pingamizi la "Ugombea Urais wa Tundu Lissu" tayari lipo, lilikwisha kuandaliwa siku nyingi.....
Na kwamba, siku hiyo hiyo atakayokuwa mahakamani, ndiyo siku hiyo hiyo atatakiwa na NEC kuja kujitetea kwa nini asiondolewe sifa za ugombea Urais kwa sababu watakazokuwa nazo waweka pingamizi wake....
Na huko mahakamani tarh 26/8 kumbe wamepanga kumuweka ndani (under detention) kwa siku kadhaa ili tu ashindwe kwenda kujitetea Dodoma kwenye NEC dhidi ya pingamizi lake, na muda uwe umekwisha kisha wanamwachia...
Baada ya muda kwisha wa kujitetea, NEC hawatakuwa na kizuizi tena kumwondoa ktk orodha ya wagombea kwa sababu watasema "hukuja kujitetea dhidi ya pingamizi lako"....
Loooh, huu ni ujinga na upumbavu wa kiwango cha juu sana ambao mamlaka za serikali ya Tanzania zinafanya eti kwa sbb ya mtu mmoja anayeitwa - Magufuli....
Nyuma ya mpango huu kwa kweli hakuna sababu zozote za kutaka kumzuia Tundu Lissu kutumia haki yake ya kiraia ya kuchaguliwa. Ni kwa sababu tu Magufuli hataki changamoto, hataki ushindani na hususani ushindani wa mtu sampuli ya Lissu....!!
Need we say more?
Absolutely nothing!!
Mimi sina shaka kuwa, hili jaribio nalo tayari limeshashindwa vibaya sana....!!!