Amsterdam and partners LLP wamlima barua Rais Magufuli na Jaji Mkuu, wabainisha njama zote zinazosukwa

Amsterdam and partners LLP wamlima barua Rais Magufuli na Jaji Mkuu, wabainisha njama zote zinazosukwa

Wangeanza na marekani, waje korea kaskazini, kisha wamalizie urusi hao unaowaita dunia.
Hujasikia Hilary clinton akilalamika matokeo yake yaliibiwa na mabosi wa dunia?? Ngoja tuone ngosha ataishia wapi.
 
There are international treaties as a nation we abide to those we have subscribed too.

Lakini ata wao wanajua kila nchi inasheria zake ambazo hawana mipaka nazo sio kwamba awaoni Lissu anavunja taratibu halali za nchi.
Nyimbo za kukaririshwa hizo. Taratibu zipi alizovunja? Sheria zipi kavunja?
 
NEC Website

Link hiyo hapo website yao it’s too slow for my patients

Mkubwa wewe si "wakili upande wa mashtaka?"

Sasa unathibitishaje mashtaka yako kisheria kwa kuwasilisha mbele ya Jaji kitabu kizima cha sheria badala ya ibara au kipengere kilichovunjwa/kiukwa?

Obviously, Hakimu/Jaji hatakuelewa na ataitupilia mbali kesi yako yote...!

Ndivyo unavyofanya wewe hapa. Unasema "....oooh, kuna shida...ooh amekiuka sheria ya uchaguzi na maadilii yake nk nk....."

Ukiulizwa kipengere gani kimevunjwa/kiukwa? Huna jibu specific rather unatoa website ya NEC...

This is ridiculous,........right?
 
Hifadhi maneno, yeye siyo yule wa namwachia Mungu. Maana mmezoea vya kunyonga.
Utofauti wenyewe tayari unawachnganya. Jinsi Lissu anavyoenda na wakati kila tukio linakuwa recovered as soon as it appear to be plotted
 
Sijui kama watu wanaelewa.

Nilisema mwaka mmoja uliopita kuwa maamuzi juu ya utawala wa awamu ya 5 yalikwishafanyika tangu mwakajana. Wanasubiriwa kwenye ncha 4, na moja tu itatosha implementation ya maamuzi.

Kama wanaotegemewa ni hawa wapiga majungu na mabingwa wa kuteka, hawataisaidia serikali, badala yake watu wataingia wazima wazima, kisha kuduwaa na kishangaa imewezekana vipi utekelezaji ukawa haraka namna hii.

Ukiwa na mshindani anayejua na anayetegemea namna utakavyofanya, halafu ukafanya vile vile kama alivyokuwa anategemea, ujue umeisha na umefeli kikamilifu. Ndiko watu wanakoelekea.

Amsterdam siyo wao bali ni jamii ya kimataifa. Barua hizi hazina lengo la kuonya wala kutisha bali kukamilisha hatua zote kama ilivyoamliwa namna ya kutekeleza.

Watakaoshindwa kuelewa, wasubirie. Kenge huwa hasikii mpaka atoke damu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa mkuu! You have sum up every thing. Observers tunaangalia tu, kwa kweli ni suala la muda tu.
 
Nyimbo za kukaririshwa hizo. Taratibu zipi alizovunja? Sheria zipi kavunja?
Lissu hajavunja sheria yoyote ya uchaguzi pale alikuwa anatembea na nakala yenye masharti kumi na sita kwa kila mgonmbea.
 
Magu hawezi kujibu HOJA za Lisu, kipi anaweza kujibu? Amiri Jeshi Mkuu miaka 3 vyombo vyako vya ulinzi na usalama vimeshindwa kupata ufumbuzi wa a daylight attack! Kipi JPM atajibu! Mwanyika mlimkuta na hatia ya uhujumu uchumi kuwa ameshirikiana na BARRICK, either kwenda jela miezi 4 au kulipa 1.5 bilioni chini ya utaratibu wa DPP, leo mmempa nafasi ya kugombea Ubunge, kipi JPM ataweza kujibu?!

Rais wetu anatatizo la 'kukurupuka', hana moyo wa kukabiliana na HOJA ni mtu wa visasi na malipizo.
Swala La Deo mwanyika limetia doa uwezo wa kufikiri wa Jpm
 
I can assure you those are not empty threats; with time you will know that Tanzania is not an island but part of a larger international community!! Hamuwezu kuachwa mnawadhurumu watu haki yao ya msingi ya kumchagua wantakae kwa kutumia dola halafu mkabaki salama!!
Mwenye sikio na asikie.
 
Kwenu Wana Lumumba,

Hakuna kitu kama hicho cha kuenguliwa, Tundu Lissu lazima agombee.

Mlisema hatakuja, kaja toka Belgium.

Mlisema msaliti hana mvuto wa kisiasa, imebainika siyo kweli.

Mlisema siku ya Sikukuu ya Nane Nane Ofisi ya Tume ya Uchaguzi Dodoma itakuwa imefungwa, Tundu Lissu alikuta ipo wazi.

Mlisema hati yake ya Kiapo haitasainiwa na Jaji wa Mahakama Kuu Dar es Salaam , jana fomu zake za kiapo zimesainiwa.

Mmepanga kumuita Kisutu tarehe 26 August 2020, Tundu Lissu hawezi kutokea kwa udhuru wa jambo muhimu ktk mchakato wa kuelekea uchaguzi 2020.

Mnasema tarehe 26 August 2020 hatatambuliwa kama mgombea rasmi wa Urais kupitia CHADEMA 2020, Tundu Lissu atatambuliwa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa na ndiyo itakuwa siku ya kusitisha tuhuma zote za mahakamani mpaka baada ya uchaguzi tarehe 28 Oktoba kumalizika.

Wagombea wanaotambuliwa na Tume ya Uchaguzi 26 Agosti tuhuma za mashtaka yao yatasitishwa kwa kinga maalum ili sisi waTanzania tuweze kushiriki kumpigia kura maana tuhuma ya kesi siyo kigezo cha kumuondolea haki yake kuchaguliwa kwani tuhuma siyo ukweli mpaka pale tu atakapo hukumiwa ndiyo sifa inakosekana.
Umemaliza kila kitu sina cha kuongeza
 
Hujasikia Hilary clinton akilalamika matokeo yake yaliibiwa na mabosi wa dunia?? Ngoja tuone ngosha ataishia wapi.
Ukisubiri uone utasubiri sana tu mzee..bora uendelee na shughuli zako za kutafuta ugali..mambo ya ngosha dunia yenyewe imenyoosha mikono..muulize balozi wa marekani aliyeondoka na yule balozi wa umoja wa ulaya aliyefungashwa.
 
Nyumbu bwana toka 2016 mnatamani Tanzania iwe Kama Zimbabwe, itengwe na jumuia ya kimataifa, inyimwe misaada na mikopo lakini haijatokea.

Kwenye korona mlitamani watu wafe kwa maelfu eti kisa Magufuli kakataa lockdown lakini Mungu katuokoa na hiyo dhahama.
Hata hili mnaloshabikia litapita tu Kama upepo, Tanzania yetu itabaki salama na Magufuli atamaliza miaka yake mitano kwa mujibu wa Katiba yetu.

Ukiangalia ki uhalisia Lisu amekuja kwa Shari na sio kwa nia njema ya kuwaletea watanzania maendeleo. Mikutano yote aliyofanya katika kutafuta wadhamini hajaelezea hata kidogo ilani ya chama chake, yeye sera yake ni kumtukana Magufuli na kukashifu maendeleo aliyofanya.

Lisu anasema endapo atashindwa atapeleka watu barabarani, kwa hiyo tayari ana wasiwasi Kama atashinda na njia pekee anayoona itamsaidia ni kuanzisha vurugu.

Huyu mtu ni hatari Kwanza hapo alipo amehakikishiwa uraia wa ubelgiji kuwa akiwasha Moto huku akiona hapakaliki yeye na familia yake wana mahala salama pa kuishi, sisi kwa ujinga wetu tunaweza kuingia kichwa kichwa na kuharibu amani yetu na hatuna pa kukimbilia.

ACHA KUPOTOSHA. PILI, KWANINI MLIMPELEKA HUKO UBELGIJI ? TATU, HAKI PEKEE HUZAA AMANI. ACHA KUPOTOSHA.
 
Huu sasa ubishi for the sake of ubishi kanuni zipo wazi kasome kuanzia section 40 imeelezewa jinsi campaign zitakavyo simamiwa msimu wa uchaguzi utakapoanza.

Mgombea pekee aliyevunja kanuni mpaka sasa ni Tundu Antipas Lissu.

Quate hiyo section weka hapa, ili tusome wote....

Kwani unashindwa nini kutoa utetezi wako kwa ukamilifu kabisa???

Problem mliyonayo in moja...

Hata ninyi ni "wajinga" tu, hamjui lolote si sheria wala kanuni.....

Hamuielewi sheria wala kanuni zake zinazoongoza mambo haya...

Na mbaya zaidi ni kuwa hata ikitokea kuziona, hamuwezi kuzitafsiri katika muktadha wake na ndiyo maana mnasumbuka kujitetea....

So long as, mmetumwa au mmejituma kuandika na kutetea msichokijua, basi mnafanya blindly tu na ndiyo mnashindwa kutetea hoja zenu....
 
ICC inafanya kazi kama ofisi za waendesha mashtaka wa serikali sawa sawa na ofisi ya DPP kwa Tanzania.

Kesi zao wanazitafuta wenyewe na wanakushitaki wenyewe hakuna mwanasheria independent anaweza kwenda kufungulia nchi au mtu kesi ICC.

Mambo mengine ni kufurahishana tu, kati ya Lissu na wafuasi wake lakini Amsterdam hana jurisdiction kwenye mambo ya ndani ya Tanzania.

Binafsi naomba Lissu asikatwe pamoja na kuvunja kanuni aachwe agombee baada ya kushindwa ndio watu wataelewa huyu mtu anahitaji psychological help.

Lissu kwa sasa anaamini yeye ni mtu untouchable, above the Tanzania laws, he has large group of followers ready to rebel at his whim and that belief is ever growing as days go by yote kwa sababu vyombo vya ulinzi wameamua ku entertain his thoughts tangia amerudi out of pity considering his plight, but at some point he needs to come down to earth.
Umeongea point muhimu sana lisu wamuache tu agombee na wampe ulinzi wote
 
Back
Top Bottom