Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Hivi ni wewe ambae ulisema kama watu wangeandamana hata vyumbani mwao wangeiona cha mtema kuni kwenye yale maandamano ya Mange?

Nasikia uliniapiza kwa kung’ata midomo ya chini kuwa ulikuwa tayari kwa lolote kwa atakae thubutu kuandamana!

Je Haya ni ya kweli?

Hivi kuadhibu wananchi kwa kutumia askari na wanajeshi huoni ni jambo lenye kuhitaji subra kubwa ili kuhakikisha maisha ya watu yanabaki kuwa salama?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Brother Mwigulu nakusalimia.

Swali langu ni je unadhani kuwa sababu ya wewe kuondolewa kwenye nafasi ya uwaziri inachangiwa na yale maandishi yaliyo tapakaa nchini kote kuwa Mwigulu ni rais 2015?
NAONESHA MSISITIZO [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]

In God we Trust
 
Kwa kuwa ni wazi kuwa maadui wetu walishawahi kutambuliwa kuwa ni pamoja na :
1. Ujinga
2. Magonjwa
3. Umaskini

Je kwa hali ilivyo sasa itakuwa sawa kwenye hiyo list ya maadui ikiongozwa namba 4. Ikawa wapinzani?

Au hapo unaonaje?

Nisaidie ili kama vipi tuwaepuke kabisa hawa jamaa wapinzani.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asan
Field Marshall, the BEST FIELD OFFICER. Rafiki yangu SHUGHULIKA NA NAFISI YAKO. KWENDA MBINGUNI HAKUNA MPIGA DEBE
Asante Sana Mkuu,unajua wewe ni Mtu maaraufu Sana ndani na nje ya Tanzania.Sisi watu wa mtaani,hua tunawaona nyinyi watu wa Level yako Kama sio binadamu wa kawaida.Kwamba hamsikii njaa,kiu,hamuumwi,hamchoki,hamkasiriki nk.

Swali langu Kama nilivyo kuuliza wewe miliwahi kumuuliza Padri mmoja kwamba kwamba hivi na wewe Padri hua unakasirika ama huwa unaijiwa na hisia za kimwili au tamaa ya kula tunda? Akanijibu ndio hisia hizo humpata lakini hushinda jaribu Hilo kwa maombi na kitubio.
 
the truecaller, Una matatizo makubwa sana, yani wewe unaona huyu Mwigulu ni mtu wa kutetewa kwa maasi yaliyofanyika chini ya utawala wake?
 
Mimi ningekuwa mwanasiasa ni ningeandaa mswada maalumu wa kufanya mapitio upya ya sheria ya kuanzishwa kwa vyama vingi.

Ili kuleta mjadala kuona kama bado tunahitaji kuwa kwenye mfumo huo au turejee kwenye mfumo wetu wa zamani wa chama kimoja.

Ili tuweze kuokoa gharama na nguvu kubwa zinazotumika katika kupambana nao!

Kuwa kwenye mfumo wa chama kimoja nako kuna faida zake nyingi tu lakini basi ijulikane kisheria kuwa tumerejea rasmi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Brother Mwigulu nakushauri hii njia uliyo amua kuitumia haitakusaidia kisiasa zaidi ya kukubomoa kulingana na mwenyekiti wako ambaye ndiye mteuzi hapo kwenu.

Jikalie kimya hiyo itakusaidia sana kukurudisha kwenye uongozi wa juu.

Huu ni ushauri wangu tu mh
Unatumia redio mbao wewe, USIMLISHE MANENO RAIS WANGU. Mhe RAIS wangu anashughulika na mambo MAKUBWA hajawahi KUSEMA hivyo Wala kuniambia binafsi. Hayo ni maneno ya kubuni ya watu kama wewe hivi

In God we Trust
 
1. Hili jibu halikusaidii Mheshimiwa, kama hutaki kutujibu hapa ondoka maana hatujakuita umejileta mwenyewe. Tulishazoea ndugu zetu wanauawa mnafurahi, Leo unaulizwa unakwepa eti watu wakutafute pembeni!!? Waambie Watanzania nini kilichotokea?

2. Tupe picha moja ukiwa Ilboru umevaa skafu vinginevyo huo ni uongo kama uongo mwingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli. Maana kila akiulizwa maswali nyeti anasema atafutwe. Sasa atatafutwa na wangapi wakati uwanja ndio huu?
 
@MwiguluNchemba kuna madai kuwa huwa hupokei simu za wapiga kura wako bila kujua wanataka kukupa habari gani, una lolote la kusema juu ya hili?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa majibu anayotoa, mimi nahifadhi maswali yangu kwake. Maana mie ndiye nilikiwa mtu wa kwanza kumpa ushauri wa aina ya siasa anayopaswa kufanya mara alipoingia bungeni. Hasa nilijibizana naye kwa muda mrefu sana baada ya kuchana hotuba ya Zitto bungeni.
 
elimisha wote huku jamvini mkuu maana mtu anapoanza kukutafuta ndo kumpoteza kunapoanza maana nyie kumwaga damu za watu mnaona ni jambo jepesi sana, ndo maana mnapopewa vyeo vya kuteuliwa mnakuwa vituko katika jamii mfano Kngi tu alikuwa kituko japo hata wewe ulikuwa na vituko vyako
Aaahahahahahaaaa, acha woga ndugu, Mkuu anataka kukutana na wewe faragha ili akuelimishe,halafu unamtolea maneno ambavyo huna uhakika nayo.Nenda bwana.
 
SIO KILA KITU KINAJIBIWA NA KILA MTU, NA KILA KITU NI PUBLIC
Hata hivyo inaonesha una siri nyingi zenye maumivu moyoni mwako. Nakushauri tena kama nilivyofanya kipindi kile unachana hotuba ya Zitto. Tekeleza yale ulioshauriwa na mmoja kati ya wachungaji wale uliowaita Dodoma baada ya tukio la Ndago. Utapata amani ya rohoni.
 
Tumekuelewa mheshimiwa,.nnachoamini Kuna baadhi ya mambo mtu inamlazimu kuyatekeza sio kwa kupenda ila Ni mfumo wa system ulivyo...nna imani na wewe kuwa ukipata nafasi kubwa zaidi unaweza kuyatekeleza kwa ufanisi mkubwa Yale uliyokusudia...kuwasaidia wananchi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NITAJIBU KILICHO MWAFAKA KUJIBU, HIYO NDIO KANUNI YA VIAPO, MIMI PAMOJA NA KUWA MWANA JF but NI MBUNGE
Mwaminifu kwa kushiriki maovu, kwa kuruhusu kutolewa uhai kwa watu wasio na hatia, kushindwa kukemea waovu, ulichoweza ni kuwa kibaraka wa boss wako ukasahau kanuni na taratibu za kazi ulizo pewa. Kiapo gani ulichoweza kukifuata.
 
Ameomba aulizwe maswali ajibu, sasa ninyi mmekomaa na 'misuto'. Wakati mwingine tumuulize kwa staha, huenda kuna mamho anataka kuyatolea ufafanuzi. Sidhani kwa staili hii ya mashambulizi anaweza kuwa kwenye nafasi nzuri kujibu.

Lakini pia tutambue kuwa siasa ni mabadiliko. Hakuna aliyedhani leo Simbachawene atakuwa hapo alipo. Haitoshangaza kuona Mwigulu, Nape na wengine wa aina yao wakirejea kwenye Baraza.
 
Back
Top Bottom